Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Zifahamu kwa Undani Hizi Hapa Sifa na Bei ya Infinix Hot 7

Hii hapa ndio simu mpya kutoka kampuni ya Infinix
Sifa na bei ya Infinix Hot 7 Sifa na bei ya Infinix Hot 7

Kama mpuni ya Infinix hivi karibuni iltangaza ujio wa simu yake mpya ya infinix Hot 7, simu hii ni toleo la maboresho la simu za Infinix Hot 6 na Hot 6 Pro ambazo zilizinduliwa rasmi hapo mwaka 2018.

Kwa upande wa Infinix Hot 7 simu hii inakuja na maboresho kadhaa ikiwa pamoja na kioo cha inch 6.2 ambacho kinakuja na resolution ya 720 X 1500 pixels. Kioo hicho kimetengenezwa kwa teknolojia ya IPS LCD pamoja na teknolojia ya High Definition Plus (HD+).

Advertisement

infinix Hot 7

Kwa upande wa Processor, Infinix Hot 7 ina endeshwa na processor ya MediaTek MT6580P yenye CPU yenye kasi hadi 1.3 GHz, Processor hiyo inasaidiwa na RAM ya GB 2 pamoja na ukubwa wa ROM wa GB 32 ambao unaweza kuongezwa kwa kutumia Memory Card hadi ya GB 128.

Kwa upande wa kamera Infinix Hot 7 inakuja na kamera mbili kwa nyuma zenye Megapixel 13 kila moja na kwa mbele simu hii inakuja na kamera moja ya Selfie yenye uwezo wa Megapixel 8. Simu hii pia inakuja na Flash kwenye kamera ya mbele pamoja na kamera ya nyuma, Sifa nyingine za Infinix Hot 7 ni kama zifuatazo.

Infinix Hot-7 nyuma

Sifa za Infinix Hot 7

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.2 chenye teknolojia ya IPS LCD HD+ infinity display, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1550 x 720 pixels.
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo)
  • Aina ya Processor (Chipset) – MediaTek MT6580P Chipset.
  • Uwezo wa Processor (CPU) – Quad-core 1.3 GHz 4x Cortex MT 6580
  • Uwezo wa GPU – Bado haijajulikana
  • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina mbili moja ikiwa na GB 16 na nyingine ikiwa na GB 32 zote zikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 128.
  • Ukubwa wa RAM – GB 2 au GB 1
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele –  Megapixel 8, yenye LED Flash.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko mbili moja ikiwa na Megapixel 13 na nyingine ikiwa na Megapixel 13 huku zote zikiwa na uwezo wa phase detection autofocus, LED flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 4000 mAh Battery.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 4.2, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, 3.1, microUSB 2.0, USB On-The-Go.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi moja ya Purple.
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Aina za Sensor – Fingerprint scanner; Face recognition; Gyroscope; Proximity; e-Compass; Light; G-sensor.
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint  (Kwa Nyuma), Inayo ulinzi wa Face Unlock.

Bei ya Infinix Hot 7

Kwa upande wa bei ya Infinix Hot 7, Simu hii inatarajiwa kuuzwa kwa Rupee ya Pakistan 14,999 PKR ambayo ni sawa na Tsh 251,000 kwa toleo lenye RAM ya GB 1 pamoja na ROM GB 16. Kwa toleo lenye RAM ya GB 2 na ROM ya GB 32 bei yake bado haijajulikana hivyo endelea kutembelea Tanzania Tech tutakujuza zaidi pale bei ya simu hiyo itakapo Tangazwa.

Kwa sasa simu hii bora ya Infinix tayari imeshafika hapa Tanzania, unaweza kupata simu hii kwa bei kati ya Tsh 260,000 hadi Tsh 360,000 inategemea na ukubwa wa ROM wa simu husika pamoja na mahali unapo nunua simu hii.

13 comments
  1. Maoni* nipo Arusha naomba bei ya infinix hot 7 nijuze tafadhali. mawasiliano mengne #0672191930 Ahsanten

  2. Naomba kuuliza bei ya infinix hot7 rom 32 nipo arusha nijulishe tafadhali mawasiliano mengine 0672191930

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use