Tofauti Kati ya Mfumo wa Android Go na Android Kawaida

Hizi ndio Tofauti za mfumo wa Android Go na Mfumo wa kawida wa Android
android go android go

Hivi karibuni kampuni ya Google ambayo ndio watengenezaji na wamiliki wa mfumo wa Android walizindua mfumo mpya wa Android Go. Mfumo huo ni maalumu kwa simu zenye uwezo wa chini yaani simu zenye uwezo wa chini ya RAM ya GB 1.

Pamoja na ufafanuzi huo bado kumekuwa na maswali mengi sana kuhusu mfumo huo mpya. Moja ya maswali hayo ni pamoja swali linalo uliza kuwa “kuna utofauti gani kati ya mfumo wa Android Go na mfumo wa kawaida wa Android. Kujibu swali hili leo nitaenda kukueleza utofauti uliopo baina ya mifumo hii miwili ikiwa pamoja na kukupa mifano kadhaa ambayo itakusaidia kwenye uelewa.

Ni nini Android Go

Kwanza kabla ya kuanza ni vyema tukajua ufafanuzi kidogo wa Android Go, pamoja na Mfumo wa Android wa kawaida. Sasa ili uweze kuelewa zaidi, tutarudi nyuma kidogo mwaka 2014. Mwaka huo Google ilianzisha mfumo mpya wa Android One, mfumo huu ulikuwa unalenga soko la India na hii ilikuwa ni kwaajili ya simu zenye uwezo mdogo au simu zenye uwezo wa kawaida. Lakini baadae mfumo huu ulibadilishwa na kuwa mfumo wa kawaida wa Android.

Advertisement

Android Go ni nini

Android Go ni mfumo ambao hutumika zaidi kwenye simu za Android zenye uwezo mdogo wa RAM kuanzia GB 1.

Sasa wazo la mfumo wa Android Go lilitokana na mfumo wa Android One na hii yote ikiwa ni jitihada za Google kuhakikisha watu wote wanaweza kutumia simu za Android hii ikiwa pamoja na simu za bei rahisi. Sasa tofauti na Android ya kawaida Android Go ni mfumo ambao hutumika hasa kwenye simu za bei rahisi ikiwa pamoja na simu zenye uwezo mdogo. Sasa tuangalie uwezo wa Android Go.

Uwezo wa Android Go

Android Go inaweza kutumika kwenye simu yoyote ile, lakini halisi mfumo huu umetengenezwa kwaajili ya simu zenye RAM kuaznia GB 1 kushuka chini. Lakini haishi hapo, mfumo wa Android Go unaweza pia kufanya kazi kwenye simu zenye ukubwa mdogo wa ndani hii ikiwa ni kuanzaia GB 8 na kushuka chini. Zaidi ni kuwa mfumo wa Android Go unakuja na programu za kipekee ambazo hizi zitakusaidia kuweza kutumia ukubwa mdogo wa ndani wa simu yako tofauti na programu au App za kawaida za Android.

Mfano wa programu ambazo ni maalumu kwa mfumo wa Android Go ni pamoja na YouTube Go, Google Go, pamoja na programu nyingine nyingi kutoka Google. Sasa utofauti wa programu hizi za Android Go na Android ya kawaida ni kuwa programu hizi za Go ni ndogo kwa ukubwa na pia kuna baadhi ya vitu ambavyo ambavyo vimeondolewa kwenye programu hizo ukilinganisha na programu za kawaida za Android.

Sifa za Android Go

Sasa kwa upande wa sifa za Android Go hapa ningependa ujue ni sifa gani ambazo utarajie kwenye simu zenye mfumo huu wa Android Go tofauti na mfumo wa kawaida wa Android. Kitu cha kwanza ambacho ni kikubwa na ambacho ndio lengo la mfumo huu ni Bei rahisi, Popote unapo taka kununua simu yenye mfumo wa Android Go ni wazi kuwa simu hiyo lazima itakuwa inauzwa bei rahisi. Kitu kingine ni kuwa tengemea kukuta ukubwa wa ndani mdogo, hii ni kwa sababu nilizo sema hapo juu kuwa mfumo huu umetengezwa maalum kwa simu zenye ukubwa mdogo wa ndani.

Kitu kingine cha mwisho ni kuwa, lazima simu hizi utakuta zina RAM ndogo au ya wastani yaani sio zaidi ya GB 1.5. Sasa mfumo sio kwamba ni lazima utakuwa kwa sifa hizo bali tukiangalia kiutengenezaji mfumo huo ndio umetengenezwa kwaajili ya simu zenye sifa kama hizo hapo juu, kifupi ni kuwa mfumo huu unalenga soko la simu za Android za bei rahisi yani kuanzia Tsh 100,000 na kuendelea.

Hitimisho

Sasa hapa kujibu swali hapo juu ni kuwa, mfuo wa Android Go ni maalum kwaajili ya simu za bei rahisi na bei rahisi maana yake ni sifa au uwezo wa kawaida au mdogo. Hivyo unapo nunua simu yenye mfumo huu wa Android Go usitegemee kupata simu yenye uwezo mkubwa kama vile inavyokuwa kwenye simu zenye mfumo wa kawaida wa Android.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use