Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Samsung Galaxy S9 Vs Apple iPhone X Ipi Bora..?

Unataka kunuanua Simu Hizi, hakikisha unasoma makala hii kwanza
Samsung Galaxy S9 vs Apple iPhone X Samsung Galaxy S9 vs Apple iPhone X

Ni wazi kuwa watu wengi wamekua wakijaribu kulinganisha Samsung Galaxy S9 Vs Apple iPhone X, na hii ni kwa sababu simu hizi zimekuwa washindani kwa muda mrefu sana na kutokana na kupata maswali mbalimbali kuhusu simu hizi sasa nimekuja na uchambuzi ambao kwa namna moja ama nyingine utaweza kupenda kwa kujua simu ipi ni bora.

Kwa kuanza nitapenda kukujulisha hapa Tanzania Tech tunafanya uchambuzi tofauti kidogo na tuna hakika mpaka mwisho wa makala hii utakuwa umepata chaguo la kujua ni simu gani ya kununua kutokana na mazingira uliyopo. Kama unataka kujua sifa za samsung galaxy S9 unaweza kusoma hapa na pia sifa za iPhone X zinapatikana hapa.

Advertisement

  • Ubora wa Kutokuingiza Maji

Wote tunajua kuwa, Samsung Galaxy S9 inakuja na uwezo wa kuzia maji vilevile hata iPhone X pia inayo uwezo wa kuzuia maji, lakini hvi ni simu gani ambayo inaweza kuzuia maji kwa muda mrefu na endapo umeangusha simu yako kwenye maji ni kwa muda gani mpaka simu yako iharibike basi majibu ya maswali hayo haya hapa.

  • Ubora pale Simu Inapokuwa Kwenye Joto Kali

Sasa kwenye video hii utaona jinsi simu za S9 na iPhone Xzikipitia kwenye majiaribio ya kuwekwa kwenye maji ya moto na hapa utaweza kujua ni simu gani ya kuwa nayo pale unapokuwa unaishi kwenye sehemu zenye joto kali, japo kuwa simu hizi zimepitia majaribio ya kuzidi kiwango lakini n vizuri sababu ya kupata mshindi na kujua ni simu ipi ambayo ni bora.

  • Ubora Pale simu Inapo Anguka

Sasa iwapo tatizo lako kubwa ni kuangusha simu mara kwa mara basi ni nyema ukangalia majaribio yanayofuata kwani hii inatokea mara nyingi sana na inawezekana hili ndio tatizo linalokufanya usiweze kununua simu hizi za iPhone X na Galaxy S9.

  • Ubora wa Kamera

Hapa najua pia ulikuwa unataka kujua, tunajua kuwa S9 imetengenezwa ikizingatia ubora wa kamera lakini pia iPhone X inasemekana kuja na kamera nzuri sana. Sasa ni wakati wa kujua ni kamera ya simu gani ambayo inachukua picha vizuri..?

  • Ubora wa Kufanya Kazi kwa Haraka

Tukija kwa upande mwingine wa ubora wa kufanya kazi haraka hapa tutaenda kuangalia simu gani inafanya kazi haraka, kumbuka video hii itaonyesha ni simu gani inafanya vitu kwa haraka na hii ni kwa wale ambao wanapenda simu zenye kufanya mambo kwa haraka.

  • Ubora Simu Ipi inaisha chaji kwa Haraka

Linapo kuja swala la chaji hapa kila mtu lazima atakuwa na hamu ya kujua, sasa kwenye video hii utaweza kuona simu nyingi lakini angalia simu ya Galaxy S9 na iPhone X pekee, simu zingine zilizoko kwenye video haziusiki kwenye uchambuzi huu. Hivyo angalia simu za Galaxy S9 na iPhone X Pekee.

  • Ubora wa Kujaa Chaji kwa Haraka

Tumeshaona simu hizi ni ipi yenye kuisha chaji kwa haraka lakini kabla ya kufanya uamuzi wa kwenda kununua simu uliyo ipenda labda nikwambie pia kujaa chaji kwa haraka ni moja ya vitu vyenye kuwa na umuhimu mkubwa tena ukizingatia maisha ya sasa ambayo yanakuitaji kufanya kazi kwa haraka wengi wetu hatuna muda wa kusubiri simu kujaa chaji hasa wakati wa mchana.

Nadhani mpaka hapo utakuwa umejua ni simu gani ya kununua pale unapotaka kununua simu yako kati ya hizi mbili kati ya Galaxy S9 pamoja na iPhone X. Mengine ya kuzingatia ni kama bei pamoja na sifa kulingana na aina ya simu unayo itaka. Kwa sasa iPhone X tayari ipo tanzania na vilevile Galaxy S9 nayo ipo hapa Tanzania unaweza kupata simu zote hizi kupitia hapo chini.

4 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use