Je ni Simu Gani Nzuri Kuwa Nayo Kati ya Tecno na Infinix

Fahamu yote ya muhimu kuhus simu za Tecno na Infinix
Simu ipi bora kati ya Tecno na Infinix Simu ipi bora kati ya Tecno na Infinix

Moja kati ya swali ambalo mara nyingi nimekuwa nikikutana nalo ni kuhusu simu bora kati ya Tecno na Infinix, kama wote tunanvyojua simu zote hizi zinazotoka kwenye makapuni ambayo yanafanana, pia simu hizi zinakuja zikiwa zinauzwa kwa bei nafuu na pia zinatumiwa sana hapa Afrika pengine kuliko sehemu nyingine duniani.

Sasa Jumatatu ya leo nimeona nikupe angalau kidogo mawazo yangu ya juu ya swali hili ambalo mpaka mwisho wa makala hii labda unaweza kukubaliana na mimi kuhusu simu zipi ni bora kati ya simu kutoka kampuni ya Tecno na simu kutoka kampuni ya Infinix. Kwa kuanza ili tuweze kuelewana vizuri kwenye makala hii tunalinganisha Brand na sio simu, katika hali yoyote ili kusudi tuweze kulinganisha Brand ni muhimu kuangalia mambo yafuatayo.

Sasa bila kupoteza muda twende tukaangalie mambo yote haya na bila shaka mwishoni pia wewe utaweza kutoa maoni yako kuhusu simu za Tecno pamoja na Infinix.

Advertisement

 • Umaarufu wa Brand Kati ya Tecno na Infinix

Tukianza na umaarufu wa Brand, ni kweli kuwa simu za Infinix na Tecno zinatumiwa sana hapa Afrika, lakini kila moja inaongoza kutumiwa sana kwa maeneo au nchi tofauti tofauti hapa Afrika. Kwa mfano nchini Nigeria mwaka 2017, kwa mujibu wa tovuti ya Pulse, brand ya Tecno ndio iliyokuwa inaongoza kwa kutumiwa sana nchini humo huku ikiwa imeshikilia nafasi ya pili kati ya brand tano za simu zinazoongoza kutumiwa sana nchini Nigeria. Hata hivyo kwenye list hiyo Brand ya Infinix ilikuwa inashikilia nafasi ya 4.

Sasa kwa hapa Tanzania mambo sio tofauti sana na Nigeria, ni wazi kuwa idadi kubwa ya watanzania wanatumia sana simu za Tecno kuliko simu za Infinix na hii ndio sababu kwenye kipengele hichi cha Umaarufu wa Brand kati ya Tecno na Infinix kampuni ya Tecno inashikilia namba moja.

 • Muundo wa Bidhaa na Kanuni Kati ya Tecno na Infinix

Kwenye ulimwengu huu wa simu janja nimefanikiwa kushika simu mbalimbali za Tecno toka mwaka zilipoingia hapa Tanzania, in fact.. Tecno yangu ya kwanza nilinunua kile kipindi kampuni ya Huawei inafanya promotion ya Smartphone pale Mlimani City. Nakumbuka kulikuwa na mistari ya watu wengi sana pale palipokuwa ofisi za Vodacom wakinunua simu za Huawei pamoja na Tecno..anyway wahenga wenzangu nadhani mtaikumbuka hiyo..

Sasa kwa kipindi hicho chote cha kutumia simu za Tecno na baadae kufanikiwa kutumia simu za Infinix nimekutana na maneno mengi sana kwa watu mbalimbali iwe mtandaoni au tukiwa kwenye mikusanyiko mbalimbali. Ni wazi kuwa utasikia watu wengi sana wakisema simu hizo zinakuja na muundo wa kawaida na wakufanana sana, vilevile sifa hizo nyingi zinakuja na sifa za kawaida kulinganisha na simu nyingine za bei hiyo. Kifupi baadhi ya watu wanasema unaweza kukisia Tecno inakuja na bidhaa ya namna gani na yenye sifa gani hata kabla ya bidhaa hiyo haijazinduliwa rasmi.

Moja kati ya kitu ambacho hadi kufikia sasa Tecno imekua ikijitahidi kuboresha ni kwenye uwezo wa kamera tu na sio kwenye uwezo wa simu zenyewe pamoja na muundo bora zaidi wa simu hizo. Kwa upande wa simu za Infinix simu hizi zinazingatia zaidi muoenekano pamoja na sifa, ukweli ni kuwa muundo wa simu za Infinix umekuwa wa tofauti sana kulinganisha na simu za Tecno toka simu za Infinix zilipo ingia sokoni ndio maana kwenye kipengele hichi cha muundo wa bidhaa na kanuni kampuni ya Infinix Inaongoza.

 • Ubora wa Bidhaa Kati ya Tecno na Infinix

Sasa tukija kwenye kipengele cha Ubora najua kila mtu atakuwa na mawazo yake kutokana na matumizi ya bidhaa kutoka kampuni husika, Lakini haya yafuatayo ni mawazo yangu binafsi baada ya kutumia brand zote mbili pamoja na kupata mawazo kutoka kwa watu mbalimbali.

Kwa upande wangu nimeshajaribu kutumia simu za Tecno Phantom 5, Tecno Boom J8 na pia nimejaribu kutumia simu za Infinix Hot 2 na Infinix Zero 5. Kwa muda wote nilio wahi kutumia simu zote hizi nilikuwa najisikia vizuri zaidi kutumia simu ya Infinix kuliko simu za Tecno. Mbali na kujisikia vizuri ukweli ni kwamba simu za Infinix kwa upande wangu ni simu nzuri kwenye ubora wa hardware na software kuliko simu za Tecno. Sijui labda kwa sababu zijapata nafasi zaidi ya kufanya uchunguzi, ila kwa muda mchache nilio wahi kutumia simu za Tecno nimekutana na matatizo mengi mbalimbali kama vile matatizo ya battery, matatizo ya kuto fungukwa kwa programu mbalimbali na matatizo mengine mengi ya kimfumo.

Hata kwa upande wa mfumo wa uendeshaji, Japo kuwa simu zote zinatumi mfumo wa Android lakini mfumo wa Infinix umekuwa ni mfumo bora kwangu kwa kipindi chote cha kutumia simu hizo, kuliko mfumo wa Tecno. Kwa ufupi kwa upande wa ubora wa hardware pamoja na ubora wa bidhaa kwa upande wangu nadhani simu za Infinix ni bora zaidi.

 • Ushirika wa Brand Kati ya Tecno na Infinix 

Ninaposema ushirika wa brand hapa nina maana ya vitu vyote ambavyo watu wanapenda kuhusu bidhaa husika yaani ni sawa na kusema, Kati ya Tecno na Infinix ni brand gani ambayo watu wanapenda kujihusisha nayo zaidi.

Japo kuwa kipengele hichi kinahitaji uchunguzi zaidi na wa muda mrefu, Lakini ni wazi kuwa kampuni ya Tecno imekuwa machoni mwa watu wengi zaidi kuliko kampuni ya Infinix. Hata hivyo sina uhakika sana kuhusu sababu halisi, pengine hii inachangiwa na ukongwe wa brand hiyo miongoni mwa watumiaji wake. Hata hivyo nimegundua kuwa ni rahisi zaidi kwa watumiaji wa simu za Infinix kuongelea zaidi kuhusu simu zao kuliko watumiaji wa simu za Tecno kuongelea kuhusu simu zao. Watumiaji wa simu za bei ghali kutoka kampuni hizo huwa na uwezo wa kuongelea zaidi simu zao kwa kuwa mara nyingi simu hizo huja kwa bei nafuu na huwa na sifa nzuri kulinganisha na simu za Tecno ambazo huja na sifa hizo hizo nzuri lakini kwa bei ghali zaidi.

Japokuwa simu hizi za Infinix ni bei nafuu pamoja na kuwa na sifa nzuri lakini ni wazi kuwa kutokana na umaarufu wa brand ya Tecno ni wazi kampuni ya Tecno inaongoza kwenye kipengele hichi cha ushirika wa bidhaa.

 • Hitimisho Simu Bora Kati ya Tecno na Infinix

Baada ya kuangalia mambo yote hayo, najua bado simu za Tecno zinaweza kuongoza kwa sababu ya kutumiwa na watu wengi zaidi na pia kwa sababu ya kuwepo kwa muda mrefu kuliko simu za Infinix, lakini mawazo yangu yako tofauti sana na watu wengine… Mimi binafsi naona simu za infinix ni bora zaidi kutokana ubora wake wa hardware pamoja na software pamoja na uwezo wa kudumu na chaji.

Najua wewe utakuwa na mawazo yako binafsi, hebu tuambie kwenye maoni yako hapo chini.. Hivi unadhani kati ya simu za Tecno na Simu za Infinix ni simu gani bora kuwa nazo, Tuambie kwenye maoni hapo chini… Najua maoni yako yatasaidia watu wengi zaidi na pia yatasaidia kampuni husika kuweza kujua nini cha kufanya kuweza kuboresha bidha zao kwaaji yako.

19 comments
 1. Simu za Tecno ndio zinapendwa na wengi sana, hata mimi mpaka naandika maoni haya natumia tecno L9 Plus, ila sijawahi kutumia simu nyingine tofauti na Nokia, simu za nokia ndio zilikuwa kwenye damu yangu, niliacha kutumia nokia baada ya kuona tangazo la whatsapp kusitisha huduma yao kwenye baadhi ya simu ikiwemo nokia. Sasa muda si mrefu nitarudi nilipokuwa tangu zamani kwenye simu janja za NOKIA.

   1. Binafsi simu ya tecno haina uwezo linganisha na simu ya inifinix kwani hata baadhi ya program hushindwa kufungua simu ya tecno, sema watumiaji upenda unafuu wa bei pia kikubwa zaidi picha upande wa camera.

 2. Tecno huenda inaongoza sababu ya ukwengwe sokoni,lakini Infinix bado changa lakini imepokewa vizuri,so ndani ya miaka 5 ijayo Tecno wasipokuwa makini watakuwa kama Nokia

 3. Kiukweli tecno inafanya vizuri kwa hapa kwetu mm binafsi nimetumia p5,y3,w4 na hadi ss bd natumia camon CX

 4. Kiukwel me nimetumia tecno xana mpaka xaxa ninayo ila kwaxaxa natumia infinix cm hizi zipo bomba xana sema tatizo bado hawana cm za hali ya chini kama tecno

 5. Nimewahi kutumia simu za Tecno H6, C8, na baadae Phantom 5 na 6. Na baadae nimeweza kutumia pia infinix NOTE 3 NOTE 4 NOTE 4 PRO na sasa Zero 5 kimsingi kunasifa nyingi kati ya simu za Tecno na Infinix lakini kwa ujumla hasa ukizungumzia ubora na mwonekano Infinix ni bora zaidi kuliko Tecno. Simu za Tecno zinakua nakero nyingi kwenye baadhi ya program na sidhani kama nitawahi kutumia Tecno baadae ya kutumia Infinix nadahni nitachagua brand nyingine.

 6. ninatumia infinix hot 6, infinix nna miez m3 naitumia ila nimeipenda kwanza haijawahi kustack katka matumiz yangu yote, haichemki kwa vyovyote. nmetumia tecno p5,m7, na camon cx, lakin zote zlkua na tabia ya kchemka napokua nmewasha data kwa mda mrefu, ukiizima data tecno kwa mda ukiwasha haiwez kuhandle ile background apps znazotumia netwek mwishoe inakua nzito kwa mda kama dakika kadhaa ndo inarud kwenye hali yake ya kawaida

 7. unajua kipendacho moyo mm nimetumia cm aina tofauti lakini unacho angalia ni utendaji wa kazi yake uharaka kama hivi sasa natumia tecno (phantom 8) ipo fastar data

 8. Kwakweli Mimi binafsi nimetumia simu aina nyingi ikiwemo techno c8 cammon, lakini mwisho wa simu hizo hasa techno zinatabia ya Ku stack, kuchemka hata unapoongea, uki charge kwakweli ina kero nyingi sana, sasa sijui kwa infinix maana ndo nimeinunua tu sijaanza kupata Kero ki ukweli inaonekana ni nzuri kwa mwonekano, hata unapoongea hutumii nguvu nyingi na ipo faster sana kufunguka, ina mambo mengi mazuri, nzuri hata ukiishika mkononi, ila bei ni balaa, ya kwangu ni x 05, bei ni kubwa sana, bei ya chini ni 350000, Mungu awabariki watumiaji wooote wa simu na aziponye

 9. Tecno inastack sana kwenye program zake wakati mwingine hadi inajirestart yenyewe.. Kinachokera zaidi nikiwasha wifi hotspot kisha nikaiweka simu muda mrefu bila kuishikashika data connection kwenye pc na simu inakuwa inactive hii inanikera sana. Naplan kuhamia brand nyingine

 10. mim nipo techno BT kiukweli inazingua sana coz inachemka vibaya mno nikifungua data sas ninajichangachanga niweze kuhamia infinix nw nahitaji ushaur infinix gan ni nzur sana coz plan zangu natka infinix hot8

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use