Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Maana ya VPN na Jinsi ya Kutumia Kwenye Simu au Kompyuta

Fahamu maana ya VPN na jinsi ya kutumia programu za VPN
Maana ya VPN na Jinsi ya Kutumia Kwenye Simu au Kompyuta Maana ya VPN na Jinsi ya Kutumia Kwenye Simu au Kompyuta

Ni wazi kuwa wote tunatumia Internet, hata hapa unaposoma makala hii unatumia Internet ndio maana leo ningependa kukwambia kidogo kuhusu matumizi bora na salama ya Internet na ili uweze kuelewa matumizi bora na salama ya Internet basi ni lazima kuongelea kuhusu maana ya VPN na jinsi ya kutumia kwenye simu au kompyuta yako.

Nini Maana ya VPN

Sasa kwa kuanza labda kwanza tujue maana ya VPN, VPN kirefu chake ni Virtual Private Network maana yake kwa kiswahili ni mtandao wa kibinafsi wa kidigital, mtandao huu unakuwa wa kibinafsi kwa sababu data zinazotumwa kutoka kwenye mtandao huo zinakuwa ziko encrypted.

Advertisement

Sasa ili kuelewa zaidi labda ni kwambie kidogo kwanini utumie VPN. Muda huu unapotumia internet kampuni zinazokupa huduma hizo za internet (ISP) zinakuwa na uwezo wa kuona vitu kadhaa kuhusu matumizi ya huduma hiyo, moja kati ya vitu wanavyoweza kuona ni pamoja na tovuti gani unayo tembelea na mara ngapi unatembelea tovuti hiyo, pia kampuni hizo zinaweza kuona baadhi ya data zingine kama vile mahali ulipo au mahali kifaa chako kilipo pamoja na kuonyesha matumizi mengine ya Internet kwenye kifaa chako.

Mara nyingi kampuni hizo zinazotoa huduma za Internet uweza kukusanya data za mteja kwaajili ya kujua tabia ya mteja mtandaoni, hivyo kupitia njia hii wanaweza kujua ni jinsi gani unahitaji kutumia Internet zaidi au kuweza kudhibiti matumizi ya Internet kwenye kifaa chako.

Sasa mara nyingi unaweza kutembelea tovuti kama Spotify.com na ukaona inakupa ujumbe kuwa huduma hii bado haipo Tanzania, moja kati ya vitu ambavyo vinaweza kutumika kujua ulipo ni pamoja na kupitia kampuni zinazokupa huduma hizi za Internet (ISP). Sasa ili kuweza kutumia tovuti kama hizi ambazo zimezuiliwa hapa Tanzania ni lazima kutumia programu za VPN.

Kwa sababu sasa naamini umejua kidogo kuhusu VPN, nadhani ni wakati wa kukwambia kwanini utumie VPN kwenye kifaa chako. VPN ni programu maalum ambayo inaweka ulinzi kati yako wewe na kampuni inayokupa huduma ya Internet. Kwa njia hiyo kampuni za simu hazitoweza kuona data zako za muhimu kama vile matumizi yako ya Internet pamoja na mambo mengine ya msingi kama vile mahali ulipo pamoja na tovuti unazo tembelea.

Jinsi Programu za VPN Zinavyofanya Kazi

Programu za VPN zinakupa uwezo wa kutembelea internet bila mtu yoyote kuweza kujua mahali halisi ulipo, programu hizi zinabadilisha matumizi yako ya Internet na kuyapitisha matumizi hayo  kwenye Server mbalimbali na hapo matumizi yako yanakuwa encrypted na kisha kurudishwa kwenye kampuni inayokupa huduma za Internet na kwa kufanya hivyo kampuni hizo hazitoweza kupata kuona matumizi yako ya internet pamoja na eneo ulilopo.

Kwa kutumia programu hizi za VPN unaweza kutembelea tovuti mbalimbali bila kuwekewa kikomo na pia utakuwa unaweza kutembelea tovuti hizo bila mtu yoyote kuweza kujua kuwa umefanya hivyo.

Kwanini Programu za VPN ni Muhimu

Ni wazi kuwa kampuni zinazokupa huduma za Internet zina uwezo mkubwa wa kuangalia data zako ikiwa pamoja na tovuti unazotembelea, pia ni wazi kuwa unahitaji ulinzi unapotembelea tovuti mbalimbali na hii ndio moja ya sababu kubwa na muhimu kwanini hutumie VPN unapo tembelea tovuti yoyote ile.

Nadhani mpaka hapo lazima utakuwa unajua ni kwanini ni muhimu kuwa na programu ya VPN kwenye kifaa chako pale unapotumia Internet, unaweza kupata programu za VPN kwa kutafita kwenye Google kwa kuandika Free VPN Download au pia unaweza kufafuta kwenye Play Store kwa kuandika hivyo hivyo, pia fanya hivyo kama unatumia iOS. Kitu cha muhumu kujua ni kuwa zipo programu za bure na za kulipia hivyo hakikisha unatafuta programu kwa kuandika neno Free.

Hadi hapo nadhani utakuwa umejua yote ya muhimu kuhusu VPN, kwa habari zaidi na mengine mengi kuhusu teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.

3 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use