Tofauti Kati ya Simu za Tecno Camon X na Camon X Pro

Hizi hapa ndio tofauti za simu mpya za Tecno Camon X pamoja na Camon X Pro
Tofauti Kati ya Simu za Tecno Camon X na Camon X Pro Tofauti Kati ya Simu za Tecno Camon X na Camon X Pro

Hivi karibuni huko nchini Nigeria kampuni ya Tecno ilizindua simu mpya za Tecno Camon X pamoja na Camon X Pro, simu hizi ni mmoja kati ya simu za Tecno zilizotoka mwaka huu (2018) zinazokuja na teknolojia mpya ya kioo cha Full Display pamoja na sifa na muonekano mpya kabisa.

Pamoja na kuwa na muonekano mzuri unao fanana simu za Camon X pamoja na Camon X Pro zinautofauti mkubwa sana ambao pengine huwezi kujua kwa kuangalia muonekano wa kawaida wa simu hizi, sasa leo kwenye makala hii tutendea kuangalia kwa undani utofauti kati ya simu hizi mbili za Tecno Camon X pamoja na Tecno Camon X Pro. Naimani mpaka mwisho wa makala hii utaweza kujua ni simu gani uweze kununua kwa sasa kulingana na utofauti ulio uona.

  • Muundo

Tukianza na muundo, Simu hizi mbili za Tecno Camon X na X Pro zinafanana kwa sura ukiangalia kwa haraka haraka, kila kitu kilichopo kwa nje kwenye Camon X na kwenye Camon X Pro kipo hivyo hivyo, lakini tofauti pekee iliyopo kwenye simu hizi ni mkanda wa rangi ya gold ulioko kwenye simu ya Tecno Camon X Pro. Mkanda huu umezungushwa moja kwa moja kwenye simu hiyo kama inavyo onekana kwenye picha hapo juu.

Advertisement

Kwa upande wa Camon X, yenyewe inayo mkanda wa Gold kwenye sehemu ya kwenye ukingo wa kamera pekee kama inavyo onekana kwenye picha hapo juu. Tofauti na hapo simu hizi zinafanana kwa muundo kila kitu hadi urefu pamoja na upana.

  • Sifa

Kwa upande wa sifa simu hizi zinakuja na utofauti kwa kiasi kikubwa kwani Camon X Pro inakuja na RAM ya GB 4 wakati Camon X inakuja na RAM ya GB 3, Camon X Pro ina ukubwa wa ndani wa GB 64 wakati Camon X ina ukubwa wa GB 16. Kamera ya mbele ya X Pro ni Megapixel 24 wakati kwa Camon X ni Megapixel 20. Vilevile uwezo wa Kioo cha Camon X Pro ni mkubwa kuliko uwezo wa Kioo cha Camon X kwani, X Pro inakuja na kioo chenye resolution ya 2160×1080 wakati Camon X inakuja na kioo chenye resolution ya 1440×720.

Kuweza kutofautisha kwa urahisi resolution ya kioo cha Camon X na X Pro ni sawa na kusema, X Pro inayo uwezo wa kuonyesha Video za 1080p, wakati Camon X ina uwezo wa kuonyesha video za 720p Pekee. Kama inavyo onekana kwenye picha hapo juu kama una angalia video kupitia mtandao wa YouTube, utaweza kuangalia video zenye uwezo wa 1080p60 kwa Camon X Pro na Video za 720p60 kwa Camon X. Tofauti na hapo hakuna tofauti nyingine kwenye upande wa sifa.

  • Uwezo wa Kufanya Kazi kwa Haraka

Kwenye uwezo wa kufanya kazi kwa haraka ni wazi kuwa Tecno Camon X Pro ni lazima itakuwa inafanya kazi kwa haraka kuliko Camon X na hii ni kutokana na uwezo mkubwa wa RAM kwenye simu ya Camon X Pro. Kama unavyoona kwenye picha hapo juu Camon X Pro imefanikiwa kufungua Programu ya Instagram kwa haraka kuliko Camon X hivyo ni wazi kuwa, Camon X Pro itakuwa na uwezo wa kufungua apps na kufanya kazi kwa haraka zaidi kuliko Camon X.

  • Kamera ya Mbele

Kwa upande wa kamera ya mbele ni wazi kuwa Camon X Pro inakuja na kamera kubwa zaidi yenye uwezo wa Megapixel 24, lakini pamoja na kuwa na kamera kubwa kiasi hichi kwa upande wa Video bado naona kama kamera ya mbele ya Camon X Pro sio nzuri kuchukua video kwani inayo mwanga mkali zaidi na kufanya video zisiwe na rangi nzuri, lakini huo ni mtazamo wangu, unaweza kuangalia picha hapo juu na uniambie kwenye maoni hapo chini wewe unaonaje.

Tofauti na Camon X, kamera ya mbele ya simu hii inakuja na Megapixel 20 lakini tofauti na Camon X Pro, Video zinazo chukuliwa kwa kutumia kamera ya mbele ya simu hii zina mwanga mzuri zaidi hivyo kufanya video ziwe na rangi nzuri na iliyo kolea. Haya ni mawazo yangu tu unaweza kufanya majaribio zaidi ya simu hizi ili kuweza kujua zaidi kuhusu kamera za mbele za simu hizi.

  • Kamera ya Nyuma

Kwa upande wa kamera ya nyuma simu hizi zote mbili zinakuja na kamera zenye uwezo sawa, Camon X Pro inakuja na Megapixel 16 na vilevile Camon X inakuja na Camera ya Megapixel 16. Lakini kabla ya kuchukua uamuzi ni vyema ufanye uchunguzi zaidi sababu kwa upande wangu naona kama kamera ya nyuma ya Camon X Pro ni bora kuliko kamera ya nyuma ya Camon X kwa sababu Kamera ya X Pro inakuja na mfumo wa kamera stabilizer ambapo unaweza kuchukua video iliyo tulia hata kama wewe una tingishika, pamoja na picha za kamera ya nyuma ya Camon X Pro zinaonekana vizuri kuliko zilie za Camon X.

Kama unavyo weza kuona kwa upande wa kushoto ni Camon X ambayo picha zake zimefifia kidogo na kwa upande wa kulia ni Camon X Pro ambayo picha zake kama unavy ona zimekuwa na rangi ambayo ni nzuri zaidi.

Basi hiyo ndio tofauti liyopo kati ya simu hizi za Tecno Camon X pamoja na Tecno Camon X Pro, unaweza kuchunguza simu hizi zaidi kupitia maduka mbalimbali ya Tecno, kisha tuambie kwenye maoni hapo chini wewe umeonaje kuhusu tofauti kati ya Tecno Camon X pamoja na Camon X Pro. Kwa upande wangu naweza kusema, ni wazi kuwa Camon X Pro ni simu nzuri kuwa nayo kama unataka simu yenye uwezo mzuri wa sifa na vilevile yenye kufanya kazi kwa haraka zaidi.

5 comments
    1. kwa kweli mpo vizuri nimepata mwanga kwenye camon x na camon pro
      mimi namiliki camon x.Asante tupo pamoja

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use