Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Vodacom Yaja na Huduma ya Malipo ya Kujirudia Kupitia M-Pesa

Sasa fanya malipo yanayo jirudia kupitia Vodacom Tanzania M-Pesa
Vodacom Yaja na Huduma ya Malipo ya Kujirudia Kupitia M-Pesa Vodacom Yaja na Huduma ya Malipo ya Kujirudia Kupitia M-Pesa

Kama wewe ni mtumiaji wa mtandao wa simu wa Vodacom hapa Tanzania basi ni inawezekana tayari una fahamu kuhusu huduma ya Malipo ya kujirudia. Kama ufahamu kuhusu huduma hii basi kwenye makala hii nitakuelekeza jinsi ya kutumia huduma hii pamoja na faida zake.

Malipo ya Kujirudia ni nini

Malipo ya kujirudia au standing order ni huduma mpya ya Vodacom kupitia M-pesa, huduma hii inamuwezesha mteja kuweza kufanya malipo ya kujirudia bila kufanya miamala hiyo mara kwa mara. Kama wewe ni mmoja wa watu ambao hufanya malipo maalum kila mwezi, kila wiki au kila siku basi huduma hii inaweza kufaa sana kwa matumizi yako.

Advertisement

Kupitia M-Pesa mtumiaji ataweza kuchagua ni malipo gani angependa kurudia, malipo hayo yakiwa ni pamoja na malipo ya bili, Malipo ya kutuma pesa pamoja na malipo ya vingamuzi mbalimbali. Huduma zote hizi zinaweza kulipiwa kwa kujirudia kwa urahisi kabisa kupitia M-Pesa.

Kwa sasa huduma hii inapatikana kwa watumiaji wote wa mtandao wa  Vodacom nchini Tanzania na unaweza kuwezesha huduma hii kupitia menu ya mpesa kwa kufuata hatua zifuatazo.

Kuwezesha Malipo ya Kujirudia Kupitia M-Pesa

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao unafanya malipo ya kujirudia mara kwa mara basi unaweza kujiunga na huduma hii ya standing order ya Vodacom kwa kufanya hatua hizi.

  • Bofya *150*00#
  • Chagua namba 4 Lipa kwa M-Pesa
  • Chagua namba 8 Malipo ya Kujirudia
  • Chagua namba 1 Weka Malilpo ya Kujurudia
  • Chagua huduma uayotaka kuwezesha Malipo ya Kujirudia
  • Weka Kumbukumbu Namba
  • Chagua muda unaotaka Malipo yajirudie

Kwa kufuata hatua hizo utaweza kuwezesha malipo ya kujirudia au Standing order kupitia M-Pesa. Huduma hii ina faida nyingi lakini kwangu binafsi nimeona faida moja kubwa ambayo pengine inaweza kuwa ni msaada kwa watu wengine.

Kwa upande wangu naona huduma hii itanisaidia kununua umeme kwa wakati bila kusubiri kuambiwa kama umeme umeisha ndipo nianze kuangalia kama kwenye simu yangu kuna pesa. Pia inasaidia pale unapokuwa na bajeti ya kulipia kingamuzi kila mwezi hasa kipindi hichi ambapo watoto wapo nyumbani. Ukweli ni kwamba huduma hii inaweza kuwa msaada kwa namna nyingi sana inategemea na utumiaji wako wa huduma ya M-Pesa.

Hadi hapo natumaini upata urahisi wa kujua kuhusu huduma hii ya malipo ya Kujirudia au standing order kupitia M-Pesa. Kama umependa huduma hii basi endelea kutembelea Tanzania Tech kwani inawezekana Vodacom wakaleta huduma nyingine bora zaidi kwani hivi karibuni Vodacom Tanzania na Safaricom kwa pamoja vilifanikisha kununua haki za brand ya M-Pesa kutoka kampuni ya Vodafone ili kuendeleza zaidi huduma hiyo. Kweli yajayo yata furahisha!

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use