Jinsi ya Kufanya Smartphone Yako Ijae Chaji kwa Haraka

Njia hizi zinafanya kazi kwenye simu zote za Android na iOS
Jinsi ya Kufanya Smartphone Yako Ijae Chaji kwa Haraka Jinsi ya Kufanya Smartphone Yako Ijae Chaji kwa Haraka

Ni wazi kwamba teknolojia imezidi kuwa msaada mkubwa sana wa kuokoa muda, zamani ilikuwa ni lazima kutafuta maelezo fulani kwenye kitabu lakini kwa sasa tunazo smartphone ambazo zinatusaidia sana kupata maelezo yoyote kwa haraka na bila kupoteza muda.

Lakini kutokana na kuwa smartphone zimekuwa ni msaada mkubwa kwetu ni wazi tumekuwa tunahitaji kuwa nazo kila mara kiasi cha kukosa hata muda wa kuzichaji. Kupitia makala hii nitaenda kukwambia njia kadhaa ambazo zinaweza kukusaidia kuchaji simu yako kwa haraka bila kujali kama simu yako inayo teknolojia ya Fast Charging au haina. Kumbuka ni muhimu kujaribu kufuata angalau njia mbili au fuata njia zote ili kupata matokeo mazuri zaidi.

Weka Airplane Mode Wakati Unachaji Simu

Jinsi ya Kufanya Smartphone Yako Ijae Chaji kwa Haraka

Advertisement

Kama unataka simu yako ijae chaji kwa haraka basi hakikisha unaweka Airplane Mode kwani hii inaweza kusaidia sana simu yako kujaa chaji kwa haraka. Kwa kufanya hivi utazuia simu yako kutumia chaji hivyo chaji yote itakayo kuwa inaingia itakuwa inatuzwa kwenye battery moja kwa moja, njia hii inafanya kazi kwa simu zote zenye teknolojia ya Fast Charging na hata zile ambazo hazine teknolojia hiyo.

Usichaji Karibu na Dirisha au Mahali Kwenye Joto, Baridi

Jinsi ya Kufanya Smartphone Yako Ijae Chaji kwa Haraka

Mara nyingi watu huwa na tabia ya kuchaji simu karibu na dirisha na hii hutokana na sababu mbalimbali, lakini kwa mujibu wa tovuti ya times, kuchaji simu yako kwenye joto kali kunaweza kusababisha simu yako kupata joto zaidi na kuisha chaji haraka ikiwa pamoja na kuharibu battery ya simu yako. Mara nyingi ni vizuri kuchaji simu yako kwenye sehemu yenye hali ya hewa ya kawaida.

Tumia Chaji Original Inayokuja na Simu

Jinsi ya Kufanya Smartphone Yako Ijae Chaji kwa Haraka

Mara nyingi smartphone zote hupitia majaribio kabla ya kupelekwa kwa watumiaji wa kawaida, moja ya majaribio hayo ni kuhakikisha simu hizo zinafaa kwenye matumizi ya kawaida. Chaji za simu hiyo pia hupimwa kama zinaweza kuchaji battery iliyopo kwenye simu kwa haraka na kwa muda unaotakiwa. Hii ni moja kati ya sababu ambayo inayoonyesha ni muhimu kuchaji na chaji zinazokuja na simu kwani husaidia simu kujaa haraka kutokana na kutengenezwa maalum kwa ajili ya simu husika.

Ondoa Kava la Simu Kabla au Wakati Unachaji Simu

Jinsi ya Kufanya Smartphone Yako Ijae Chaji kwa Haraka

Mara nyingi imekuwa ni kawaida kuchaji simu zetu zikiwa na makava kama kawaida, lakini kutokana na sababu hapo juu joto kali ni adui mkubwa wa battery yako na simu yako kwa ujumla kwani huweza kusababisha simu yako kuharibika au wakati mwingine battery ya simu yako kulipuka kama simu yako itakuwa imezidiwa sana na joto. Mara nyingi pendelea kuondoa kava la simu yako kabla ya kuchaji kwani hii huweza pia kusaidia chaja yako kuingia vizuri kwenye tundu la kuchajia.

Usimalize Chaji Kabisa Hadi Asilimia 0

Jinsi ya Kufanya Smartphone Yako Ijae Chaji kwa HarakaMara nyingi ni muhimu kuhakikisha kuwa unachaji simu yako kabla ya kufika asilimia 0, hii ni muhimu kwa kuwa battery ambazo huchajiwa pale zinapofika asilimia 0 huwa na tabia ya kuharibika au kutojaa chaji kwa muda unaotakiwa. Ni vizuri kuhakiksha unachaji simu yako angalau kila inapofika asilimia 30 au 20. Hii husaidia battery kudumu na chaji na pia husaidia battery kuja kwa haraka zaidi. Kumbuka njia hizi zinaweza kufanya kazi kwenye simu zote za Android na iPhone ila kama unataka kujua njia za ziada za iPhone unaweza kusoma hapa.

Na hayo ndio baadhi ya mambo ambayo yanaweza kusaidia simu yako kujaa chaji kwa haraka, kama unataka kujifunza zaidi unaweza kusoma hapa kujua sababu zinazofanya simu yako kuisha chaji kwa haraka. Kwa makala nyingine kama hizi hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use