Mambo Yanayo Sababisha Kompyuta Kuwa (Slow)

Hizi ndio sababu kwanini kompyuta yako inakuwa Slow
Kompyuta kuwa Slow Kompyuta kuwa Slow

Habari na karibuni kwenye makala nyingine, Leo tutaenda kuangalia sababu kuu zinazo zababisha kompyuta yako kuwa slow au taratibu. Sababu hizi zinakwenda sambamba kwa watumiaji wa kompyuta za aina zote iwe unatumia Desktop au Laptop sababu hizi zinafanana.

Kwa kuanza labda niweke jambo moja wazi, endapo unatumia kompyuta yenye uwezo mdogo na kazi unazo zifanya kwenye kompyuta hiyo haziendani na uwezo wa kompyuta yako, basi ni lazima utaona kompyuta yako inafanya kazi taratibu sana na hiyo inatokana na utofauti wa uwezo kati ya programu unayo tumia na kompyuta yako.

Lakini kama unaona kabisa kompyuta yako inao uwezo wa kutosha kuendesha programu fulani lakini bado unaona inafanya kazi taratibu, basi ni vyema kusoma makala hii hadi mwisho pengine utapata sababu kwanini kompyuta yako inafanya slow.

Advertisement

Malware

Mambo Yanayo Sababisha Kompyuta Kuwa (Slow)

Malware ni aina fulani ya programu ambazo hizi zime tengenezwa maalum kufanya mambo mbalimbali yasiyo sahihi kwenye kompyuta yako. Programu hizi mara nyingi hupatikana pale unapo weka (install) programu zisizo aminika (Cracked) kutoka vyanzo mbalimbali.

Mara nyingi ili kuweka programu hizi kwenye kompyuta yako ni lazima utalazimika kuzima Antivirus ndipo uweze kuinstall programu hizi. Baada ya kuinstall programu hizi, hapo ndipo Malware huanza kazi ya kusafirisha data kutoka kwenye kompyuta yako kwenda kwa mdukuaji au wakati mwingine Malware hupachika matangazo mbalimbali kwenye kivinjari chako. Kama kompyuta yako imeadhiriwa zaidi na malware utaona kompyuta inakuwa Slow zaidi unapo unganisha Internet.

  • Jinsi ya Kutatua

Kama kwa namna moja ama nyingine kompyuta yako inafanya hayo hapo juu basi unaweza kufanya hatua hizi. Hatua ya kwanza hakikisha una programu ya kuzuia Malware na Virus na hakikisha programu hiyo iko kwenye toleo jipya (updated).

Hatua ya pili hakikisha una weka programu ambazo zina aminika kwenye kompyuta yako na usiweke programu kutoka vyanzo visivyo julikana. Hakikisha una itumia programu yako ya kuondoa virus na malware kikamilifu na jaribu angalau kila wiki kutumia programu hiyo.

Programu Kutozima Sawasawa

Mambo Yanayo Sababisha Kompyuta Kuwa (Slow)

Sababu nyingine ambayo hii uathiri sana kompyuta nyingi ni pamoja na kutozima programu sawasawa mara baada ya kumaliza kutumia. Mara nyingi hii hutokea kwenye kompyuta nyingi za sasa kwani mara nyingi unapo bofya kitufe cha kuzima programu unakuta programu hiyo haijizimi na inakwenda moja kwa moja hadi kwenye (background programs).

Mara nyingi sehemu hiyo huwezesha programu nyingi kuendelea kufanya kazi hata baada ya wewe kuifunga programu hiyo.

  • Jinsi ya Kutatua

Hapa inaitaji utaalam kidogo, ili kuahakikisha programu usizo zitumia zinazima kisawasawa kama unatumia kompyuta yenye mfumo wa Windows unaweza kubofya vitufe hivi kwa pamoja Ctrl + Alt + Delete, baada ya kubofya hivyo chagua Task Manager, baada ya hapo itafunguka programu yenye kuonyesha programu zote zinazofanya kazi kwenye kompyuta yako kwa wakati huo.

Chagua programu unayotaka kufunga kisha, Bofya kitufe cha kulia kwenye Mause yako kisha bofya sehemu iliyo andikwa End task. Kumbuka ni muhimu kufanya hivi endapo umemaliza kutumia programu hiyo na ume Hifadhi (Save) kazi zako ulizokuwa unafanya, bila kufanya hivyo kazi zako zote zitapotea baada ya kufunga programu husika kwa mtindo huu.

Kutozima na Kuwasha Kompyuta Mara kwa Mara (Restart)

Mambo Yanayo Sababisha Kompyuta Kuwa (Slow)

Unaweza kushangaa lakini hii ni moja kati ya sababu nyingine inayosababisha kompyuta kuwa slow. Sababu hii sio kwa kompyuta tu, hii ni mpaka kwenye simu za mkononi. Kutozima kompyuta yako kuna sababisha kompyuta yako kuifadhi mafaili ya programu ulizo tumia na hii inasababisha kumpyuta kuwa slow sana.

Kompyuta huifadhi mafaili ya programu ulizo zitumia ili kurahisisha pale unapotaka kutumia programu hizo tena uweze kuwasha programu hizo kwa urahisi na haraka.

  • Jinsi ya Kutatua

Hapa unatakiwa kuhakikisha unazima na kuwasha (Restart) kompyuta yako ngalau mara moja baada ya kutumia kwa zaidi ya siku moja. Hii itasaidia kompyuta kufuta mafaili yanayo limbikizana na kuweza kuhifadhi programu mpya ambazo utakuwa umeanza kutumia kwa muda huo. Ili kufanya hili kwa usahihi hakikisha una Restart kompyuta yako sio kuzima kabisa Shut down.

Kuacha Programu Zijiwashe Zenywe Unapo Washa Kompyuta

Mambo Yanayo Sababisha Kompyuta Kuwa (Slow)

Kutokana na maendeleo ya Teknolojia, wabunifu wengi sana wa programu wamekuwa wanatengeneza programu ambazo huwa na uwezo wa kujiwasha pale unapo washa kompyuta yako. Programu hizi mara nyingi uwenda zikawa salama au nyingine zikawa si salama. Sababu hii pia ni moja kati ya sababu zinazo changia sana kompyuta kuchelewa kuwaka pale inapowashwa.

Jinsi ya Kutatua

Hakikisha unapo Install programu kwenye kompyuta yako usiweke tiki kwenye maneno yaliyo andikwa launch on startup, ili kuweza kuona maneno haya hakikisha una install programu hatua kwa hatua uku ukiangalia maneno hayo.

Pia unaweza kuzima programu ambazo tayari zinaweza kujiwasha pale unapo washa kompyuta yako kwa kubofya vitufe vya Ctrl + Shift + Esc. Kisha bofya sehemu iliyoandikwa Startup, kisha angalia majina ya programu alafu mbele ya majina hayo angalia sehemu iliyoandikwa Status.

Hapo utaona maneno Enabled maana yake programu hiyo inaweza kuwaka pale unapowasha kompyuta yako, sasa kuzima bofya sehemu hiyo iliyo andikwa Enabled kisha bofya kitufe cha kulia kwenye Mouse yako kisha bofya Disable. Kumbuka baadhi ya programu ni muhimu kuwaka wakati unawesha kompyuta yako hivyo angalia programu ambayo kweli unaona haina umuhimu wa kuwaka wakati unawasha kompyuta yako.

Kutumia Kivinjari Chenye Programu Nyingi za Kuongeza (Extensions) 

Mambo Yanayo Sababisha Kompyuta Kuwa (Slow)

Sababu nyingine inayo sababisha kompyuta kuwa slow ni pamoja na kutumia Kivinjari chenye programu nyingi za kuongezewa. Programu za kuongezewa mara nyingi kujulikana kama Extensions, hizi kufanya kazi za ziada kwenye kivinjari chako. Ni muhimu kujua kuwa programu hizi za kuongezewa kufanya kazi kama programu nyingine zote na hufanya kompyuta yako kuwa slow kama unatumia programu hizi nyingi.

Jinsi ya Kutatua

Hakikisha unatumia programu chache za kuongezewa na hakikisha kama unaona programu fulani huitumii mara kwa mara na kama haina umuimu kwako basi unaweza kuondoa programu hizo kwenye kivinjari chako. Kama unatumia Google Chrome unaweza kufanya hivyo kwa kusoma hapa.

Na hizo ndio baadhi ya sababu ambazo zinaweza kufanya kompyuta yako kuwa slow kwa namna moja ama nyingine.

Unaweza kuendelea kujua zaidi mambo mengine kwa kuendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku. Kumbuka njia hizi zinaweza kufuatwa na watu wanaotumia kompyuta za aina zote iwe Desktop au Laptop au kompyuta zote zenye mifumo tofauti ya Windows au macOS.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use