Jinsi ya Kutengeneza Tovuti kama Twitter Ndani ya DK 10

Miliki tovuti yako inayo fanana na tovuti ya Twitter BURE kwa dakika 10 tu!
Jinsi ya Kutengeneza Tovuti kama Twitter Ndani ya DK 10 Jinsi ya Kutengeneza Tovuti kama Twitter Ndani ya DK 10

Kama unapenda kumiliki tovuti yako mwenyewe inayo fanana na Twitter basi huu ndio wakati wako, kupitia makala hii nita kuonyesha jinsi ya kutengeneza tovuti kama Twiiter ndani ya dakika 10.

Njia hii ni rahisi sana na unaweza kumiliki tovuti hii bure kabisa bila kuwa na domain wala hosting kwa urahisi na haraka. Basi moja kwa moja bila kupoteza muda twende kwenye makala hii.

Jinsi ya Kutengeneza Tovuti kama Twitter Ndani ya DK 10

Advertisement

Mfano wa Webiste Hapa

Mfano wa App Hapa

Baada ya kuangalia mfano na kuona kama ni kitu ambacho unahitaji sasa moja kwa moja twende kwenye hatu za jinsi ya kuinstall tovuti hii kwenye domain yako pamoja na hosting yako.

Kama kwa namna yoyote huna domain wala hosting basi unaweza kupata domain na hosting kwa urahisi kwa kufuta hatua hapa chini, hakikisha una anza kuangalia kuanzia dakika ya 7 na sekunde 34. Unaweza kubofya hapa na kuanza kuangalia video hiyo kwenye dakika hiyo.

Baada ya hapo unaweza kuendelea kwa kudownload file za tovuti hiyo ya Twitter hapo chini na kisha endelea kwa ku-upload file hizo kwenye domain yako kama ilivyo kwenye video hapo juu. Kumbuka unaweza kuanza kwa kuangalia kuanzia dakika ya 7 na sekunde 34.

Download Hapa

Baada ya kuweka file hizo sasa unaweza kuendelea kwenye hatua zifuatazo ambazo ni rahisi sana, hakikisha umetengeneza database na unazo password zake na username. Kisha sasa endelea kwenye hatua hizi.

Kupitia browser yako andika jina la domain yako kisha andika /install mbele yake, mfano tanzaniatech.one/install hakikisha una andika kama ilivyo kwenye mano huo. Baada ya kuandika hivyo utaweza kuona maelezo hayo hapo chini kwenye kioo cha simu au kompyuta yako.

Jinsi ya Kutengeneza Tovuti kama Twitter Ndani ya DK 10

Kubali vigezo na masharti kwa kibofya na kuweka tiki kwenye sehemu ya I gree kisha baada ya hapo bofya sehemu ya Continue na endelea kwenye maelezo yafuatayo.

Jinsi ya Kutengeneza Tovuti kama Twitter Ndani ya DK 10

Maelezo haya ni muhimu kwani yana hakikisha kuwa tovuti yako inafanya kazi kwa usahihi kwa kuwa na sifa zote zinazotakiwa, ni muhimu kuhakikisha kuwa sehemu zote zina tiki ya kijani kwani bila hivyo utaweza kuendelea ku-install tovuti hii. Kama ukikwama hapa tafadhali wasiliana nasi.

Jinsi ya Kutengeneza Tovuti kama Twitter Ndani ya DK 10

Baada ya hapo sehemu hii ni sehemu ya mwisho na sehemu hii inahitaji kuwa na umakini mkubwa kwani hapa unahitaji kujaza maelezo yote kwa usahihi. Unatakiwa kujaza sehemu hizi kama zifuatazo, hakikisha sehemu zote zimejazwa kwa usahihi.

  • SQL host name – weka jina la host name hapa mara nyingi inakuwa ni localhost kama ni tofauti utapewa data hizi wakati wa kutengeneza database.
  • SQL username – weka username ya database.
  • SQL password – weka password ya database.
  • SQL database name – weka jina la database.
  • Site url – weka link ya website yako.
  • Site name – Andika jina la website yako.
  • Site title – Jina la website yako unalotaka lionekane na watumiaji wengine wote hata kwenye (Google).
  • Site E-mail – andika email ya website yako (Hii ni barua pepe kuu ambayo ndio utatumia wewe kama admin.
  • Enter a password for admin – andika password yako wewe kama admin na hii ndio itakayo tumika kwako wewe kama admin.

Baada ya kujaza maelezo yote haya sasa endelea kwa kubofya install iliyopo chini upande wa kulia, subiri baada ya muda kidogo na tovuti yako kama Twitter itakuwa imekuwa installed.

Jinsi ya Kutengeneza Tovuti kama Twitter Ndani ya DK 10

Baada ya hapo andika email yako wewe kama admin pamoja na password kisha bofya Ingia, baada ya hapo sasa unaweza kuediti website yako kama admin. Baada ya hapo ukiwa umeingia bofya Mengine, kisha chagua Control Panel na hapo ndipo ambapo utaweza ku-edit kila kitu kama admin.

Jinsi ya Kutengeneza Tovuti kama Twitter Ndani ya DK 10

Sasa kupitia ukurasa huo kila kutu kinajieleza na unaweza kubadilisha jina la website, kuchagua maelezo unayotaka yaonekane kwenye Google pamoja na mambo mengine mbalimbali.

Jinsi ya Kutengeneza Tovuti kama Twitter Ndani ya DK 10

Mpaka hapo sasa utakuwa umeweza kumili website yako kama Twitter ambayo utaipata bila gharama yoyote. Kama unataka kujua zaidi unaweza kuwasiliana nasi kuipitia sehemu ya maoni hapo chini. Kama unataka kuona mfano hai wa tovuti hii unaweza kubofya pale juu.

Kama unataka kutengenezewa tovuti hii ikiwa pamoja na app yake ya Android unaweza kuwasiliana nasi na tuta kusaidia kutengeneza tovuti hii kwa gharama nafuu.

Kama unataka kujifunza zaidi hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku kwani sasa tutakuwa tunaweka makala nyingi zaidi kila siku. Kama unataka kujifunza hatua hizi kwa video hakikisha unajiunga nasi kupitia channel yetu ya Tanzania Tech hapa.

Kwa muajanja zaidi unaweza kusoma hapa kujua jinsi ya kuthibitisha malipo ya serikali kwa urahisi kupitia simu yako ya mkononi.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use