in

Mtandao wa Playboy Wafuta Ukarasa Wake wa Facebook

Baada ya Tesla na SpaceX sasa Playboy nayo yafuta ukurasa wake

Mtandao wa Playboy Wafuta Ukarasa Wake wa Facebook

Playboy ni gazeti la Marekani linalo husu maisha ya wanaume na burudani. Gazeti hilo Iilianzishwa mwaka 1953 huko Chicago nchini marekani na Hugh Hefner. Toka kipindi hicho mpaka sasa gazeti hilo limekuwa kubwa sana na kwa sasa Playboy ni moja kati ya gazeti tajiri zaidi nchini marekani.

Sasa hapo jana kampuni inayo simamia gazeti hilo Playboy Enterprises, ilitoa ripoti kwa waandishi wa habari kuwa imeamua kufuta ukurasa wake wa Facebook ambao ulikuwa na wafuasi zaidi ya milioni 25. Hatua hiyo inakuja wakati kampeni ya #DeleteFacebook ikiendelea kwenye mtandao wa Twitter na kusababisha kampuni kubwa kama Tesla na SpaceX nazo pia kufuta kurasa zake za Facebook.

Kwenye ripoti yake kampuni ya Playboy Enterprises imesema kuwa, imeamua kufuta ukurasa wake huo kutokana na kutokuaminika kwa facebook kwani ni watu wengi sana wanawasiliana na kampuni hiyo kupitia ukurasa huo wa facebook ambao, kutokana na kuamua kuficha siri za watumiaji wake wameamua kusitisha matumizi ya mtandao wa Facebook.

Jinsi ya Kuanzisha Podcast kwa Urahisi na Bure (100%)

Facebook bado inaendelea kushutumiwa kwa uvujishaji wa data za siri, huku nchini Kenya Raila Odinga nae akisema, ataishtaki kampuni hiyo kutokana na kutumia jina lake kuendesha kampeni ya kuchochea uhasama wa kikabila kwa lengo la kuhujumu azma yake ya kuwa rais katika Uchaguzi Mkuu wa Kenya mwaka 2017.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

One Comment