Tumekuwa tukiongelea sana kuhusu App za kujaribu kwenye simu ya Android, lakini je vipi kuhusu Game..? Well kama wewe ni mpenzi wa game basi unasoma makala sahihi. Hata hivyo list hii haitahusisha game za kawaida bali itahusisha game za kutumia akili na game ambazo hata mtu mzima anaweza kucheza ili kupoteza muda au kuboresha ufanisi wa ubongo wako katika kufikiria.
- 1Line Puzzle Mania Brain Trainer
Kwa wale wahenga, najua utakuwa unakumbuka ule mchezo wa shule ya msingi wa kuchora nyota bila kuondoa mkono wakati nachora, sasa game hii ndio inahusu hivyo lakini sasa hapa utaletewa maumbo mbalimbali uchore bila kuondoa mkono. Game hii ni nzuri na ukweli kabisa itakufanya ucheze kila wakati unapokua na nafasi lakini kumbuka sio rahis..
- Dancing Line
Tofauti na game nyingi game hii inakuitaji ucheze kwa kusikiliza yaani kwa kutumia sauti ya milio inayotokea kwenye game hizo unatakiwa kubofya kwenye kioo cha simu yako kwa kufuatilia biti ya nyimbo unayo sikia. Kwa kufanya hivyo utakuwa unacheza game huku unasikiliza muziki mzuri. Ukweli ni kuwa game hii inaweza kukupunguzia mawazo na kumbuka game hiyo sio rahisi hata kidogo inahitaji usikivu zaidi kuliko kutumia akili.
- Duet
Duet ni game nyingine ya kuumiza kichwa kidogo, Game hii inakuitaji uweze kukwepesha vidoti viwili ambavyo vinapita kwenye ulimwengu wa matofali matofali mengi game hii ni ngumu sana. Uniamini…! jaribu sasa ujionee.
- Brain It On! – Physics Puzzles
Kama jina la game hii linavyosema game hii inakuitaji kutumia akili sana, unacho hitajika kufanya ni kuchora maumbo kadhaa ambayo yanaweza kufanya mambo ambayo unaelekezwa. Game hii ni ngumu sana na inakuhitaji uwe unatumia akili sanaaaaa.
- Cut the Rope 2
Hii ni moja kati ya game nzuri na za kuumiza kichwa sana, unachotakiwa ni kukata kama kwa wakati maalumu ili uweze kufikia zawadi maalum. Game hii ni ya siku nyingi kidogo kama bado ulikua huja anza kuicheza anza sasa game hii ni nzuri na ni lazima utumie akili.
Na hizo ndio game ambazo nimekuandalia leo ambazo ni lazima utumie akili, natumaini kuwa utazipenda.. kama unajua game yoyote ngumu ambayo ungependa tushiriki na wengine tuandikie kwenye maoni hapo chini nasi tutaziongeza kwenye list hii.