Kwa wale wapenzi wa Game za XBox na PS4 nakuendelea najua jina PUBG sio jina geni kwani game hii ni moja kati ya Game ambazo zinachezwa sana mpaka sasa. Game hii inahusisha kikundi cha watu wanne ambapo mnapambana Live ama mubashara kuweza kuishi katika mazingira mbalimbali, kupambana huko unatumia silaa mbalimbali ambazo ni lazima uzipate kwanza.
Kwa wale ambao tayari wamesha cheza Game hii kwenye vifaa vya PS4 na Xbox, lazima utakua unajua raha ya kucheza game hii. Sasa raha imeongezeka zaidi kwani game hii sasa imetangazwa kuja rasmi kwenye simu za mifumo yote yaani mifumo ya Androd pamoja na iOS.
Kwa watumiaji wa Android itakubidi uwe na simu yenye ukubwa wa ndani angalau GB 2 na ni lazima simu yako iwe inatumia angalau Android 5.1.1 na pia hakikisha simu yako ina RAM angalau GB 2. Kwa watumiaji wa iOS Game hii inaweza kufanya kazi kwenye vifaa vya mfumo wa iOS kuanzia iOS 9 na inafanya kazi kuanzia kwenye simu za iPhone kuanzia simu ya iPhone 6 na kuendelea.
Unaweza kupakua Game hiyo sasa kwa kubofya hapo chini kulingana na mfumo wa uendeshaji wa simu yako unayotumia.
- PUBG Mobile – Mfumo wa Android
- PUBG Mobile – Mfumo wa iOS
yakwangu tecno w3 lite vip lita play
Haijalishi aina ya simu Muhimu Ram na Android Version.
Nataka nijue jinsi ya kutuma pesa kwenye akaunti yangu ya pubg ili ninunue royal pass
Tumia Mpesa Mastercard au Airtel Money Mastercard