Jiandae na Msimu Mpya wa Game Kutoka Kampuni ya EA

Jiandae na Game mpya kutoka EA Games
Game mpya kutoka EA Game mpya kutoka EA

Mkutano wa E3 2018 au Electronic Entertainment Expo 2018 unao tarajiwa kuanza rasmi hapo kesho tarehe 12 hadi tarehe 14 siku ya alhamisi, kwenye mkutano huo kampuni mbalimbali za burudani kupitia Video game hupata nafasi ya kuonyesha yote mapya yanayokuja kwa mwaka 2018 kwenye upande mzima wa Michezo mbalimbali ya Video Game, Vifaa vya kuchezea game na mambo mengine mbalimbali yanayohusu michezo au Game.

Kwa mwaka huu, kampuni ya EA ambayo ni maarufu kwa utengenezaji wa Video Game bora imeshafanya mkutano wake wa EA Play 2018, mkutano unaofanyika kila mwaka kabla ya mkutano wa E3 2018. Mwaka huu kampuni ya EA inakuja na game mpya mbalimbali ambazo na uhakika wapenzi wa game watapenda kujua zaidi kuhusu game hizo, basi bila kupoteza muda twende tuka-angalie game hizo mpya ambazo zinatarajiwa kuja kutoka kampuni ya EA.

Anthem

Advertisement

Kwa wale ambao ni wapenzi wa game basi ni lazima watafurahia hii, Game mpya ya Anthem  inakuja naitakuwa ni moja kati ya game nzuri sana kucheza kwa wale wapenzi wa game za Sci-fi. Game hii inatarajiwa kuja rasmi kuanzia tarehe 22 mwezi wa pili mwaka 2019.

Battlefield V

Kwa wale wapenzi wa game hii ya vita ya Battlefield, Natumaini watapenda kusikia kuwa toleo jipya la game hii ya Battlefield V inakuja na mfumo wa Multiplayer au Battle Mode. Hapa utaweza kucheza game hii na marafiki zako na kupigana nao kivita ili kuwashinda na kubaki mwenye na mshindi kama ilivyo kwenye game ya PlayerUnknown’s Battlegrounds.

Unravel 2

Kwa wale wanaopenda game za puzzle basi lazima utakuwa unafahamu game hii ya Unravel, msimu huu kampuni ya EA imekuja na toleo la pili la game hii ambayo sasa inakuja na Yarny (vijitu viwili vilivyo tengenezwa kwa uzi) wawili ambao unaweza kucheza wewe na rafiki yako au unaweza kuendesha vijitu hivyo vyote viwili wewe mwenye. Game hii sasa inapatikana kwa watumiaji wa vifaa vya PC, PlayStation 4, na Xbox One.

Mbali na game hizi, game zingine zinazo tarajiwa kutoka EA ni pamoja na game ya Sea of Solitude, ambayo inategemewa kuja mapema mwaka 2019, pamoja na game nyingine ya Star Wars Jedi: Fallen Order, ambayo bado haija tangazwa rasmi tarehe ya kutoka kwake.

Na hizo ndio baadhi tu ya Game ambazo zinatarajiwa kuja kutoka kampuni ya EA, bado kutakuwa na game nyingine nyingi ambazo zitakuwa zinatagazwa kupitia mkutano wa E3 2018 hapo kesho hivyo endelea kutembelea Tanzania Tech kujua zaidi kuhusu game hizo.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use