Kama wewe ni mpenzi wa Game ni wazi kuwa mara nyingi una cheza game kwa kutumia simu yako ya mkononi, kuliona hilo leo nimekuletea list ya game nzuri za kucheza kwenye simu yako ya Android, game hizi ni nzuri zaidi kwa wale wanaopenda game za kupigana na silaha kama vile bunduki na kadhalika.
Game hizi zote zinapatikana kwenye soko la Play Store na zote zinapatikana bure kabisa, kama unataka kudownload game husika unaweza kufanya hivyo kwa kubofya jina la Game ambalo linakuja na link maalum itakayo kupeleka kwenye soko la Play Store. Najua unahamu ya kujua game hizi hivyo basi bila kupoteza muda twende tukaangalie game hizi.
1. West Gunfighter
West Gunfighter ni game nzuri ya kupigana kwa bunduki, game hii inakupa uwezo wa kutatua vigezo mbalimbali ambavyo vipo ndani ya game hii ikiwa pamoja na kushindana na wenzeko moja kwa moja. Game hii inapatikana play store unaweza kudownload kwa kutumia link iko hapo juu.
2. Six Guns: Gang Showdown
Game nyingine ambayo ni nzuri kujaribu kwenye simu yako ya Android ni pamoja na Six Guns Gang Showdown, kama zilivyo game nyingine kwenye list hii game hii pia ni ya kupigana kwa bunduku. Lakini tofauti na game nyingine game hii inakupa uwezo wa kupigana kwa kutumia silaha za tofauti, unaweza kupata game hii kupitia app ya Play Store.
3. Modern Combat 5: eSports FPS
Kama wewe ni mpenzi wa game za kupigana kwa bunduki na bado hujacheza game hii basi unapitwa sana. Modern Combat 5 ni game nzuri sana na pia stori ya game hii ni nzuri sana. Unaweza kupata game hii kupitia Play Store kwa kubofya link hapo juu.
4. Guns of Boom – Online PvP Action
Kama ulishawahi kucheza game ya PUBG na ukaipenda basi lazima utaipenda game hii ya Guns of Boom. Game hii inakuruhusu kucheza na wenzako mtandaoni na kama ukibaki mwenyewe basi wewe utakuwa mshindi. Game hii ni nzuri sana ila inahitaji umahiri kuweza kucheza, unaweza kupata game hii kupitia Play Store.
5. Sniper 3D Gun Shooter: Free Shooting Games – FPS
Kama wewe unapenda game za kudungua basi game hii ya Sniper 3D Gun Shooter ni game nzuri sana kwako. Game hii inakupa uwezo wa kucheza kupitia level mbalimbali. Mbali na hayo game hii ina muonekano mzuri sana. Unaweza kuipata game hii kwa kudownload kupitia link hapo juu.
Na hizo ndio game nzuri nilizo kuandalia kwa siku ya leo, game hizi unaweza kuzipata kupitia soko la Play Store kwa kubofya link hapo juu. Kujua Game nyingine nzuri za kucheza kwenye simu ya Android unaweza kusoma makala yetu iliyopita. Kwa habari zaidi za teknololojia hakikisha unatembelea Tanzania Tech kila siku.