in

Jinsi ya Kujua Mtu Anachati Sana na Nani WhatsApp

Tumia njia hii kujua mtu unaechat nae sana kupitia kwenye WhatsApp

Jinsi ya Kujua Mtu Anachati Sana na Nani WhatsApp

Ni kweli kwamba kuna wakati tunajikuta tunapoteza muda mwingi sana kwenye mitandao ya kijamii kiasi kwamba baadae tunashindwa kujua muda ulikwenda wapi. Lakini mambo haya yanaweza kuepukika na kwa kuanza leo nimekuleta njia mpya na rahisi ya kukusaidia wewe kujua mtu unae chati nae sana kupitia programu ya WhatsApp au kama ni mtu mwingine basi utajua mtu anachati na nani sana kwenye programu yake ya WhatsApp.

Kitu cha muhimu ni kuwa, hakikisha hutumii njia hii vibaya na pia usitumie njia hii kwa watu wazima, unaweza kutumia njia hii kwaajili ya mtoto ili kuangalia tabia zake hasa mtandaoni.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Njia hii inaweza kukusaidia kujua mtu unae chati nae sana kwenye programu yako ya WhatsApp ikiwa pamoja na kuona namba zake za simu moja kwa moja hata kama ulifuta namba hizo au hata kama namba hizo hazipo kwenye phonebook yako. Njia hii ni rahisi na haitaji ujuzi wowote, basi bila kupoteza muda twende moja kwa moja kwenye makala hii.

Hatua ya kwanza – Ingia kwenye programu ya WhatsApp kisha fungua na bofya sehemu ya Settings.

Jinsi ya Kujua Mtu Anachati Sana na Nani WhatsApp

Hatua ya Pili – Kwenye ukurasa wa Settings bofya sehemu ya Data and storage usage inayopatikana karibia na mwisho wa ukurasa huo wa Settings.

Jinsi ya Kujua Mtu Anachati Sana na Nani WhatsApp

Hatua ya Tatu – Bofya sehemu ya Storage usage au Manage Storage inayopatikana kwenye ukurasa wa Data and Storage usage uliofungua awali, sehemu hii ni ya pili kwenye ukurasa huo.

Jinsi ya Kujua Mtu Anachati Sana na Nani WhatsApp

Jinsi ya Kujua Mtu Anachati Sana na Nani WhatsApp

Hatua ya nne – Baada ya hapo sasa utaweza kuona list ya majina, namba za simu pamoja na size ambazo zitakuwa zimepangwa. Hapo kwenye list hiyo ndipo utakapo weza kujua mtu unaechati nae sana kwa kuangalia namba iliyopo juu ya list hiyo. Namba hizo zimepangwa ya kwanza hadi ya mwisho na ndivyo ilivyo kwa watu unao chati nao sana.

Jinsi ya Kujua Mtu Anachati Sana na Nani WhatsApp

Kwa kufuata hatua hizo na imani kabisa unaweza kujua mtu unaechati nae sana kwenye programu yako ya WhatsApp. Kumbuka njia hii inafanya kazi kwenye simu za aina zote na unaweza kufanya kwenye simu yako yoyote kwa kufuata hatua hizo.

Hayo ndio maujanja niliyo kuandalia kwa siku ya leo, kama unataka kujifunza zaidi kwa vitendo unaweza kujiunga nasi kwenye channel yetu ya Tanzania Tech hapa. Kwa maujanja zaidi unaweza kusoma hapa kujua tovuti zitakazo kusaidia kusoma meseji za mtu bila yeye kujua.

Jinsi ya Ku-sign na Ku-edit PDF Kupitia Smartphone

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.