in

Zuia Mtu Kusoma Meseji Zako za WhatsApp Bila Wewe Kujua

Fuata hatua hizi kuweza kumzuia mtu kuchungulia meseji zako za WhatsApp

kuzuia mtu kusoma meseji za WhatsApp

Linapokuja swala la faragha ni wazi kuwa hapa Tanzania tech tumekuwa tukisisitiza jambo hili kupitia makala zetu mbalimbali, sasa kuendeleza harakati hizi leo tumakuandalia maujanja mapya kabisa ambayo yataweza kufanya mtu yoyote asiweze kusoma meseji zako za WhatsApp.

Sasa ili kusudi uweze kuelewa vizuri ni vyema tuanze mwanzo kabisa ili uweze kujua ni namna gani unavyoweza kuzuia mtu kusoma meseji zako.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Kwa siku ya leo kwenye makala hii tunazungumzia meseji za WhatsApp zile zinazo tokea juu kabisa ya simu yako pale unapotumiwa meseji hiyo. Meseji hizo hutokea na kufanya mtu aweze kusoma meseji hiyo moja kwa moja bila kuifungua kwani huwa inasomeka kupitia sehemu hiyo.

Kama unavyo ona hapo juu, hivyo ndivyo inavyokuwa kama ukiwa umeshika simu yako na ghafla meseji ya WhatsApp inaingia na kusababisha hata aliyeko pembeni yako kuweza kusoma meseji hiyo moja kwa moja bila hata wewe kufungua meseji hiyo.

Sehemu hizi zinatofautina kwenye kila simu kwani simu nyingine zinapitisha meseji nzima kwa juu na zingine ndio huonyesha meseji kama hivyo.

Sasa ili kuondoa sehemu hiyo na kuwezesha kupokea meseji ya WhatsApp kimya kimya unaweza kufuta hatua hizi rahisi sana. Kwa kuanza tuanze na mfumo wa Android alafu tutafuta kwenye mfumo wa iOS.

Kupitia Mfumo wa Android

Fungua programu yako ya WhatsApp kisha nenda sehemu ya Settings inapatikana juu upande wa kulia kwenye vidoti vitatu, kisha chagua sehemu ya Notifications.

Baada ya hapo sogeza kurasa mpaka chini kidogo utaona sehemu imeandikwa Use high priority notifications, utakuta sehemu hii imewekewa tiki mbele yake hivyo bofya hapo kutoa tiki hiyo.

Baada ya hapo shuka tena chini kidogo utaona tena sehemu nyingine imeandikwa hivyo hivyo Use high priority notifications bofya hapo kuondoa tiki ili kuzima sehemu hiyo.

Kwa kufanya hatua hizi, kila mara meseji ya WhatsApp itakapo ingia itatokea tuu alama ya WhatsApp juu ya kioo chako kuashiria kama meseji mpya imengia kwenye simu yako.

Kupitia Mfumo wa iOS

Sasa baada ya kuangalia sehemu hii kwenye mfumo wa Android sasa tuangalie kwenye mfumo wa iOS.

Ingia kwenye programu ya WhatsApp, kisha bofya sehemu ya Settings iliyopo chini upande wa kulia, Baada ya hapo bofya sehemu ya Notifications, kisha shusha ukurasa huo chini kidogo na zima sehemu iliyo andikwa Show Preview.

Kwa kufuata njia hizi basi utaweza kutumia simu yako kwa uhuru hata kama uko na mtu yoyote na hatoweza kuona jina la mtumaji wa meseji au hata ujumbe wenyewe.

Njia hii ni nzuri sana guys na ukweli inasaidia sana hasa pale unapokuwa kwenye daladala unakuta mtu anatolea macho simu yako kama vile ni chakula….

Anyway i hope maujanja haya yameweza kukusaidia kwa namna moja ama nyingine, kama kuna mahali umekwama usisite kutuandikia kupitia sehemu ya maoni hapo chini nasi tutaenda kukusaidia moja kwa moja. Kwa habari zaidi na maujanja tembelea channel yetu hapa kujifunza kwa vitendo.

Code za Siri za Smartphones Mbalimbali (Njia Rahisi)

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

8 Comments