Kampuni ya Motorola hivi leo imezindua simu yake mpya ya Motorola Edge 70 Pro, simu hii ni ingizo jipya la matoleo ya Edge 70 na Edge 70 Fusion ambayo yalizinduliwa rasmi mwaka jana 2025.

Motorola Edge 70 Pro inakuja na sifa zaidi huku ikiwa na CPU ya Octa-core (1×3.4 GHz Cortex-A725 & 3×3.2 GHz Cortex-A725 & 4×2.2 GHz Cortex-A725) huku ikiwa na chipset ya MediaTek Dimensity 8500 Extreme ambayo ilizinduliwa rasmi mwanzoni mwaka huu 2026, ambayo pia ni bora kwa wapenzi wa Game.
Kwa upande wa Uhifadhi wa ndani, Edge 70 Pro inakuja na chaguo moja la uhifadhi wa GB 256, bila kuwa na uwezo wa kuongeza kwa kutumia Memory Card. Simu hii pia inakuja na machaguo ya RAM kati ya GB 8 au GB 12.
Kwa upande wa kamera, Edge 70 Pro inakuja na kamera mbili za nyuma zenye uwezo wa Megapixel 50 kila moja, pamoja na kamera ya mbele selfie yenye Megapixel 50 pia.

Simu hii inaweza kuchukua video za hadi 4K kwa kamera zake za nyuma na mbele, huku zikiwa na uwezo wa HDR.
Kwa upande wa Battery Edge 70 Pro inakuja na battery ya 6500 mAh ambayo inaweza kufanya simu hii kudumu na chaji ndani ya siku nzima kulingana na matumizi yako.
Kwa sasa bado hakuna taarifa kama toleo hili la Motorola Edge 70 Pro litapatikana hapa Tanzania, lakini kulingana na takwimu tarajia kupata simu hii kwa hapa Tanzania kwa kuanzia TZS 1,750,000 hadi TSZ 1,850,000 pamoja na kodi.

