Kampuni ya Honor imekuwa ni kinara wa simu za daraja la kati kwa muda mrefu, hivi karibuni kampuni hiyo imezindua matoleo mapya ya simu zake za Honor 600 ambayo inajumisha Honor 600, 600 Pro na 600 Lite.

TABLE OF CONTENTS
Sifa na Bei
Simu zote zinakuja na sifa bora huku Honor 600 Pro ikiwa na sifa bora zaidi, kwa kuwa na chipset ya Snapdragon 8 Elite huku ikisaidiwa na RAM ya GB 12, huku Honor 600 ikiwa na chipset ya Snapdragon 7 Gen 4, 600 Lite ikiwa na Dimensity 7100 Elite na RAM kati ya GB 8 au GB 12.
Kwa upande wa storage simu hizi zinakuja na machaguo tofauti kati ya GB 256GB/512GB/1TB kwa 600 Pro, na 128GB/256GB/512GB kwa Honor 600, pamoja na 128GB/256GB kwa Honor 600 Lite.
Kwa upande wa kamera, 600 Pro inakuja na kamera za nyuma tatu Megapixel 200, Megapixel 50 na Megapixel 12. Huku ikiwa na kamera moja ya selfie ya Megapixel 50.
Honor 600 inakuja na kamera mbili za nyuma zenye Megapixel 200, na Megapixel 12. Huku ikiwa na kamera ya selfie ya Megapixel 50.
Toleo la Honor 600 Lite linakuja na kamera mbili za nyuma yaani Megapixel 108, na Megapixel 5, pamoja na kamera ya selfie ya Megapixel 16.
Kwa upande wa upatikanaji tarajia kupata Honor 600 Pro kuanzia TZS 2,850,000 hadi TZS 3,000,000. Honor 600 Kuanzia TZS 1,900,000 hadi 2,000,000, na 600 Lite kuanzia TZS 1,080,000 hadi TZS 1,150,000.


