Kampuni ya Asus ambayo ni maarufu kwa utengenezaji wa vifaa mbalimbali vya electronic, hivi karibuni imetangaza rasmi kusitisha utengenzaji wa simu janja yani Smartphone, n.
Kwa mujibu wa ripoti, Asus haijataja sababu za kusitisha utengenezaji wa simu janja lakini ripoti huyo imethibisha kuwa kampuni hiyo imetoka rasmi kwenye ushindani wa kutengenza simu janja.
Hata hivyo kwa mujibu wa ripoti mbalimbali mtandaoni, inasemekana kuwa kampuni hiyo itajikita zaidi kwenye utengenezaji wa tablet zaidi, huku ikitarajia kuzindua tablet mpya hivi karibuni.
Kampuni ya Asus imekuwa ni kinara wa utengenezaji wa smartphone bora za Asus ROG Phone kwa ajili ya wapenzi wa Game.
Kwa sasa, bado hakuna ripoti kamili kama kampuni hiyo itaendelea na usambazaji wa simu zake za zamani au ni hatua gani ina fuata. Kwa taarifa zaidi endelea kutembelea Tanzania Tech.


