Sifa za Alcatel 1X Simu ya Kwanza Inayotumia Android Go

Hii ndio simu ya kwanza kuwa na mfumo wa mpya wa Android Go
Sifa za Alcatel 1X Sifa za Alcatel 1X

Hivi karibuni kampuni ya Simu ya Alcatel ilizindua simu mpya tano, moja kati ya simu hizo ni simu mpya ya Alcatel 1X. Simu hii ni moja kati ya simu za kwanza kabisa kuwa na mfumo mpya wa Android Go, mfumo ambao umetengenezwa maalumu kwa simu zenye uwezo mdogo.

Simu hii imekuwa gumzo zaidi mtandaoni kutokana na kuwa simu ya kwanza inayotumia mfumo huo pamoja na kuwa simu ya bei rahisi zaidi chini ya dollar $100. Aidha mbali na hayo simu hiyo kwa mara ya kwanza imetangazwa kuinga kwenye soko la marekani ikiwa bei ya chini zaidi.

Advertisement

Zifuatazo ndio sifa za Alcatel 1X pamoja na bei ya simu hii ambayo inawezekana kuanza kupatikana siku za karibuni hapa Tanzania na Sehemu nyingine duniani

  • Ukubwa wa Kioo – Inch 5.7 yenye kioo chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, yenye kuonyesha rangi milioni 16 na resolution ya 480 x 960 pixels, 18:9 ratio (~203 ppi density)
  • Mfumo wa Uendeshaji – Inatumia Android 8.1 Oreo Go
  • Uwezo wa Processor – Quad-core 1.3 GHz Cortex-A53
  • Uwezo wa GPU – PowerVR GE8100
  • Ukubwa wa RAM – Inayo machaguo mawili RAM GB 1 na RAM GB 2
  • Ukubwa wa Ndani – GB 16 nayoweza kuongezwa na memory card ya hadi GB 32
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Kamera ya mbele ni Megapixel 5 yenye LED flash pamoja na kuchukua video za 720p.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Kamera zina tofautiana kwenye simu hizi kwani zinakuja mbili simu (yenye model 5059D ) inakuja na megapixel 13  na nyingine inakuja na kamera ya nyuma ya Megapixel 8, zote zinakuja na teknolojia ya autofocus, pamoja na LED flash.
  • Uwezo wa Battery – Li-Ion 2460 mAh battery yenye uwezo wa kukaa siku moja kutokana na matumizi yako.
  • Viunganishi – Inakuja na Wi-Fi 802.11 b/g/n, Wi-Fi Direct, hotspot, Bluetooth 4.2, A2DP, LE mfumo wa GPS wa A-GPS, teknolojia ya NFC (kwenye simu yenye model 5059Y ).
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, pia inatumi sehemu ya USB ya microUSB 2.0.

Kwa upande wa bei simu hii inategemewa kuanza kuuzwa kwa dollar za marekani chini ya dollar $100 ambayo ni sawa na shilingi za kitanzania Tsh 225,600 kawa mujibu wa viwango vya kubadilisha fedha vya siku ya leo. Simu hizi zinakuja kwa model tofauti hivyo bei inaweza kubadilika kulingana na model. Hapa Tanzania bei inaweza kuongezeka zaidi kutokana na kodi.

Na hizo ndio sifa za Alcatel 1X, simu ya kwanza kabisa kutumia mfumo wa Android Go, mfumo ambao ni maalum kwaajili ya simu za bei nafuu na zenye uwezo mdogo.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use