in

Jina la Bluetooth Limetoka Kwa Mfalme wa Zamani Huko Denmark

Je wajua kuhusu jina la bluetooth lilipotoka..? Kama hujui soma hapa kujua zaidi.

Bluetooth Divice

Watu wengi tumesha zoea majina mbalimbali kutokana na kuyakuta au kutoku waza au kujiuliza majina hayo yalipotoka, hapa Tanzania Tech tutaendelea kukuletea historia fupi juu ya majina haya yalipotoka na jinsi yalivyokuja kuwa majina ya vitu hivyo, kwa mfano jina Wi-Fi najua unajua ila nataka kukujulisha zaidi kuwa jina hili limetoka kwenye neno “Wireless Fidelity.” anyway hii ni mada ya siku nyingine.

Kwa upande wa Bluetooth tumezoea kuiona hii kwenye smartphone zetu, kompyuta na hata vitu vingine vingi vya electronics lakini historia ya bluetooth ni tofauti na sehemu jina hili linapo tumika. Kwenye miaka ya 958 mpaka 985 kulikua na mfalme aliyekua akiongoza nchi ya Denmark pamoja na Norway, mfalme huyu alisifika kwa mambo mengi moja kati ya hayo ni kuunganisha nchi za Denmark na Norway chini ya utawala wake, mfalme huyo aliyekuwa anaitwa Harald “Blåtand” Gormsson.

Mfalme huyu pia alikua anajulika kwa kuwa na jino lake ambalo lilikua lina rangi nyeusi ya blue/na lenye ukijivu kidogo, jino lake hilo lilikua tofauti sana mpaka mfalme huyo alipewa jina la utani la “Blåtand” ambalo linatafsiriwa kutoka kwenye lugha ya Danish likiwa na maana ya “Bluetooth”, lakini najua utaniuliza je hii ndio sababu pekee ya bluetooth kuitwa bluetooth endelea kusoma ili kujua zaidi kuhusu teknolojia hii ya Bluetooth.

Fahamu Maana ya Alama Hizi Kwenye Vifaa vya Elektroniki

Hapa twende mbele mpaka kwenye miaka ya 1996 miaka 1000 toka utawala wa mfalme huyo, teknolojia ya wireless ndio ilikua iko kwenye miaka yake ya mwanzoni kampuni ya Intel ilikuwa na teknolojia yake mpya iliyoitwa Biz-RF kwa upande mwingine kampuni ya kampuni ya ki-swedish ya Ericsson nayo ilikua na teknolojia yake iliyoitwa MC-Link na pia kampuni ya Nokia nayo ilikua na teknolojia yake iliyokuwa inaitwa Low Power RF, kampuni hizi ziliamua kuchukua uamuzi wa kukaa pamoja ili kutengeneza teknolojia moja ambayo ingeweza kutumika na watu wote.

Mwezi December mwaka huo kampuni zote ziliamua kutoa wawakilishi ambao walikutana kwenye makao makuu ya kampuni ya Ericsson huko sweden, lengo kubwa lilikua ni kuanza kufanya michakato juu ya teknolojia hiyo mpya ambapo kabla ya kuanza wilitaka kutengeneza jina la awali ambalo linge kutumika kabla ya kukamilika kwa teknolojia hiyo. Mwakilishi kutoka kampuni ya Intel aliamua kupendekeza jina la “Bluetooth” na sababu zake zilikua ni kuwa mfalme huyo aliweza kuunganisha nchi za Sweden na Norway hivyo kutokana na umoja ambao kampuni hizo uliamua kuwa nao ili kutengeneza teknolojia hiyo basi jina hilo lingefaa sana.

Baadae baada ya teknolojia hiyo kukamilika kampuni hiyo ilianza kutafuta jina kwaajili ya teknolojia hiyo majina yaliyo kuwepo ni RadioWire (linalotoka kwa intel) na PAN (Personal Area Networking, kutoka kwa IBM). Baada ya kufanya uchaguzi wa muda mrefu jina PAN lilifanikiwa kuwa ndilo litakalo tumika lakini baada ya wiki moja toka kuzinduliwa kwa teknolojia hiyo kampuni hizo zilikutana tena kutokana na uchunguzi uliofanyika na kuonekana neno PAN halitofaa kuwa Tradmark kutokana na kuleta maana nyingi pale linapo tafutwa kwenye Internet. Kampuni hizo ziliamua kutumia jina la Bluetooth ambalo pekee ndio lilikua halipatikani kwenye Internet kwa kipindi hicho.

Fahamu Mwanzo wa Teknolojia na Makampuni Mbalimbali

Baada ya hapo sasa ilikuwa zamu ya kutafuta logo ya Bluetooth ambayo waty wengi hudhani kuwa ni B iliyoandikwa kwa font ya tofauti, lakini wataalm wanasema kuwa logo hiyo ilitoka kwenye magofu ya zamani ya nyumba ambazo alikua akikaa mfalme huyo wa zamani ambapo logo hiyo ilikua ikimaanisha “Blåtand”. Na hapo ndipo jina Bluetooth lilipozaliwa pamoja na logo yake.

Nadhani mpaka sasa utakuwa umejua kwa ukamilifu jina Bluetooth lilipotokea, kama unataka kujua zaidi kuhusu historia za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech kila siku pia usisahau kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari za teknolojia kwa haraka, pia usisahau kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja ya teknolojia kwa njia ya video.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.