Hivi karibuni shirika la mawasiliano Tanzania (TTCL) limekuwa likifanya maboresho ya huduma zake ikiwa pamoja na kuimarisha zaidi huduma za mawasiliano pamoja na internet, sasa kuptia akaunti ya Twitter ya Waziri Kindamba mbaye ni Kaimu ofisa mtendaji mkuu wa TTCL amesema kuwa laini za mtandao huo za simu zinatolewa bure na hazipaswi kuuzwa.
Mkurugenzi huyo aliandika tweet ifuatayo ikifuatiwa na picha ya tangazo hilo, “Epuka matapeli, Laini za TTCL in BURE kabisa, HAZIUZWI”.
TTCL sasa imekua ikijitahidi kuboresha huduma zake, ikiwa pamoja na kuanzisha huduma nyingi mpya za internet ili kuweza kukidhi mahitaji ya wateja wake kwa hapa Tanzania.


