Top 10 : YouTube Channel Maarufu Hapa Tanzania Mwaka 2018

Zifahamu hizi hapa ndio Channel za YouTube Maarufu zaidi kwa hapa Tanzania
channel za YouTube maarufu zaidi Tanzania channel za YouTube maarufu zaidi Tanzania

Zimebakia siku chache hadi kukamilisha mwaka 2018, katika kukamilisha mwaka hapa Tanzania Tech huwa tunakuletea Top 10 ya mambo mbalimbali na kwa kuanza leo tungependa kuanza na mtandao wa YouTube ambapo hizi ni channel 10 maarufu zaidi hapa Tanzania kwa mwaka 2018.

Kumbukua channel hizi zimechaguliwa kutokana na wingi wa Subscriber na sio views kwenye kila video, vilevile kumbuka kuwa data hizi zinatoka kwenye mtandao wa socialblade. Kwa channel ambazo zimekaribiana subscriber hadi kufika mwisho wa mwaka kabisa matokeo yanaweza kubadilika hivyo ni muhimu kujua hayo.

10. TIMUA TV

Subscriber 376,535 – Hadi Tarehe 28-11-2018

Advertisement

Kama wewe ni mpenzi wa kuangalia Video basi ni vyema kuifahamu channel ya Timua TV, Channel hii inakuletea video mbalimbali za vituko mbalimbali kutoka kwa wasanii chipukizi wa hapa Tanzania. Channel hii imeanzishwa mwaka 2016 na ina idadi ya video 67 hadi kufikia siku ya leo.

9. BONGO 5

Subscriber 402,113 – Hadi Tarehe 28-11-2018

Bongo 5 ni channel ya hapa Tanzania ambayo inakuletea habari mbalimbali za kutoka ndani na nje ya nchi, Channel hii ni maarufu zaidi kwa matukio ya Live pamoja na Habari mpya na matukio ya kila siku. Channel hii imeanzishwa mwaka 2006 na ina idadi ya jumla ya video 5,380 hadi kufikia leo.

8. DIRA TV

Subscriber 422,736 – Hadi Tarehe 28-11-2018

Dira TV nia channel ya matukio mbalimbali channel hii inakuja na mtindo wa kuweka video mbalimbali za matukio ya kushangaza kutoka ndani na nje ya Afrika na Tanzania kwa ujumla. Channel hii imeanzishwa mwaka 2017 na ina idadi ya video 375 hadi kufikia siku ya leo.

7. TEMU TV

Subscriber 423,274 – Hadi Tarehe 28-11-2018

Temu TV au StephanoTemuVEVO ni channel ya mtanzania na channel hii ina mkusanyiko wa habari mbalimbali za watu maarufu wa hapa Tanzania na nje ya Tanzania. Channel hii imeanzishwa mwaka 2016 na ina idadi ya video 914 hadi kufikia siku ya leo.

6. RAYVANNY

Subscriber 499,203 – Hadi Tarehe 28-11-2018

Rayvanny ni msanii wa kimataifa wa muziki wa bongo flava kutoka hapa Tanzania na ni mmoja wa wasanii walio sajiliwa chini ya kampuni ya Wasafi ambayo inaongozwa na Msanii Diamond Platnumz. Channel hii imeanzishwa mwaka 2016 na ina idadi ya video 332 hadi kufikia siku ya leo.

5. TOPTEN TV

Subscriber 605,999 – Hadi Tarehe 28-11-2018

TopTen TV ni channel ya Youtube ambayo inakupa mchanganyiko wa habari mbalimbali pamoja na video za kuonyesha dawa za asili na hatua za kujitibia magonjwa mbalimbali. Channel hii ilianzishwa mwaka 2012 na ina idadi ya video 272 hadi kufikia siku ya leo.

4. HARMONIZE

Subscriber 671,976 – Hadi Tarehe 28-11-2018

Harmonize ni msanii bongo fleva wa kimataifa na pia ni mmoja wa wasanii wa kwanza kusajiliwa chini ya lebo ya Wasafi ambayo inaongozwa na Diamond Platnumz. Channel hii ilianzishwa mwaka 2015 na kuanzia kipindi hicho hadi sasa ina idadi ya jumla ya video 329 hadi kufikia siku ya leo.

3. GLOBAL TV

Subscriber 1,179,202 – Hadi Tarehe 28-11-2018

Global TV au Global TV Online ni Channel inayokupa habari mbalimbali za kila siku kutoka ndani na nje ya nchini. Channel hii ilianzishwa mwaka 2011 na ni moja kati ya sehemu ya huduma zinazotolewa na Global Publisher, channel hii ina idadi ya video 14,414 hadi kufikia siku ya leo.

2. MILLARD AYO

Subscriber 1,502,695 – Hadi Tarehe 28-11-2018

Millard Ayo ni mmoja wa watangazaji maarufu wa kituo cha Clouds Media Group, kupitia channel yake hii utaweza kupata habari mbalimbali za kutoka ndani na nje ya nchi kila siku. Channel ya Millard ayo ilianzishwa mwaka 2012 na kwa muda wote hadi sasa channel hiyo ina idadi ya video 13,766 hadi kufikia siku ya leo.

1. DIAMOND PLATNUMZ

Subscriber 1,608,900 – Hadi Tarehe 28-11-2018

Channel ya kwanza maarufu zaidi kwa hapa nchini Tanzania ni channel ya mwana muziki wa kimataifa na msanii wa bongo fleva Diamond Platnumz. Channel yake iliyoanzishwa mwaka 2011 ina idadi ya video 527 hadi kufikia siku ya leo.

Na hizo ndio channel maarufu zaidi kwa hapa Tanzania, Kama unavyoweza kuona kwa Tanzania nzima channel zilizo fikisha idadi ya subscriber milioni 1 ni channel tatu tu, yaani channel ya Global TV, Millard Ayo pamoja na Diamond Platnumz. Anyway kama nilivyo sema hapo awali kwa channel zinazo karibiana subscriber mambo yanaweza kubalika ndani ya kipindi hichi chote hadi hapo itakapo fika kabisa mwezi wa mwisho wa mwaka huu 2018.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use