Video 10 Ambazo Hazipendwi Zaidi Kupitia YouTube 2018

Hizi ndio Video zinazoongoza kwa Dislike kwenye mtandao wa YouTube
Video ambazo hazipendwi Video ambazo hazipendwi

Wakati tukikaribia mwisho wa mwaka 2018 ni wakati mzuri sana wa kujitadhimini, ni kweli wapo waliofanya vizuri na pia wapo waliofanya vibaya sana. Kupitia makala ya leo hebu twende tukangalie list ya tofauti kidogo kutoka Wikipedia.

Leo tutaangazia Video ambazo zinashikilia chati kwa kuchukiwa zaidi kupitia mtandao wa YouTube, Kumbuka naposema kuchukiwa haimanishi video hizo zinachukiwa kwamba ni mbaya kwa ujumla au zina maadili mabaya hapana, bali hapa na maana zile video ambazo watu wengi zaidi wame bofya kitufe cha DISLIKE kuliko kitufe cha LIKE kupitia mtandao wa YouTube.

Baadhi ya Video kwenye list hii ni maarufu sana kutoka na kuwa kwenye list ya Video zinazo angaliwa zaidi. Nadhani kila mtu anataka kujua kwanini video hizi zinachukiwa ndio maana watu wengi zaidi wanazidi kuangalia video hizo anyway, bila kupoteza muda let’s get to it.

Advertisement

10. Masha and the Bear: Recipe for Disaster

Video 10 Ambazo Hazipendwi Zaidi Kupitia YouTube 2018

 • Kwa sasa haijapendwa (Dislike) Mara – Milioni 2.27
 • Kwa sasa imeangaliwa (Views) Mara – Bilioni 3.3

Video hii imetengenezwa na Studio moja ya nchini Urusi na video hii inahusu tamthilia ya katuni ambayo inahusu maisha ya msichana mmoja anayeitwa Masha pamoja na dubu au Bear.

9. Cortando o Botão do YouTube

Video 10 Ambazo Hazipendwi Zaidi Kupitia YouTube 2018

 • Kwa sasa haijapendwa (Dislike) Mara – Milioni 2.52
 • Kwa sasa imeangaliwa (Views) Mara – Milioni 26

Ukweli mpaka sasa bado binafsi sijajua hii video inahusu nini ila kwa mtazamo tu wa Thumnals ya video hii kweli hata mimi mwenyewe nisinge angalia kabisa sio hata ku-dislike mimi nisinge angalia ukizingatia bando nalo ni la kuunga unga hahah.. anyway hebu niambie wewe unaweza kuangalia video ya namna hiyo.? Tuambie kwenye maoni hapo chini.

8. How It Is (Wap Bap …)

Video 10 Ambazo Hazipendwi Zaidi Kupitia YouTube 2018

 • Kwa sasa haijapendwa (Dislike) Mara – Milioni 2.91
 • Kwa sasa imeangaliwa (Views) Mara – Milioni 55

Video hii ni nyimbo inaitwa “How it is” ya msanii kutoka nchini ujerumani anaitwa Bianca Heinicke au kwa jina lingine “Bibi”.

7. Friday

Video 10 Ambazo Hazipendwi Zaidi Kupitia YouTube 2018

 • Kwa sasa haijapendwa (Dislike) Mara – Milioni 3.37
 • Kwa sasa imeangaliwa (Views) Mara – Milioni 127

Video hii ni nyimbo ya msanii kutoka nchini marekani anayejulikana kwa jina la Rebecca Black, nyimbo hii iliandikwa na kutengenezwa na Clarence Jay kwenye studio zake huko Los Angeles.

6. Despacito

Video 10 Ambazo Hazipendwi Zaidi Kupitia YouTube 2018

 • Kwa sasa haijapendwa (Dislike) Mara – Milioni 3.69
 • Kwa sasa imeangaliwa (Views) Mara – Bilioni 5.7

Kweli penye wengi apakosi mengi, video ambayo pia inaongoza kwa kuangaliwa sana YouTube pia ni video namba 6 inayo kuchukiwa zaidi kwenye mtandao wa YouTube. Najua wote tunaijua Despacito hivyo sioni haya ya kukupa taarifa kuhusu video hii.

5. Can this video get 1 million dislikes?

Video 10 Ambazo Hazipendwi Zaidi Kupitia YouTube 2018

 • Kwa sasa haijapendwa (Dislike) Mara – Milioni 3.76
 • Kwa sasa imeangaliwa (Views) Mara – Milioni 15

PewDiePie ni YouTuber maarufu zaidi kupitia mtandao wa YouTube na pia jamaa huyu yupo kwenye list ya watu wanaolipwa zaidi kupitia mtandao wa Youtube. Video hii jamaa huyu alitengeneza na kuomba wafuasi wake kubofya kitufe cha kuchukia (Dislike) video hiyo zaidi kuliko kuipenda. Mhh kuna njia nyingi ambazo unaweza kuwa maarufu kupitia YouTube.

4. Call of Duty: Infinite Warfare Reveal Trailer

Video 10 Ambazo Hazipendwi Zaidi Kupitia YouTube 2018

 • Kwa sasa haijapendwa (Dislike) Mara – Milioni 3.78
 • Kwa sasa imeangaliwa (Views) Mara – Milioni 41

Kama wewe ni mpenzi wa game basi sidhani kama kuna haja ya kuelezea video hii, lakini kama wewe sio mpenzi wa game ni vizuri kufahamu game ya Call of Duty. Video hii ni Trailer ya video game hiyo.

3. It’s Everyday Bro

Video 10 Ambazo Hazipendwi Zaidi Kupitia YouTube 2018

 • Kwa sasa haijapendwa (Dislike) Mara – Milioni 3.76
 • Kwa sasa imeangaliwa (Views) Mara – Milioni 15

Video hii ni video ya muziki kutoka kwa YouTuber anaejulikana kama Jake Paul akiwa anashirikiana na kikundi cha muziki cha Team 10.

2. Baby

Video 10 Ambazo Hazipendwi Zaidi Kupitia YouTube 2018

 • Kwa sasa haijapendwa (Dislike) Mara – Milioni 9.93
 • Kwa sasa imeangaliwa (Views) Mara – Bilioni 2

Nadhani hapa sina haja ya kuandika maelezo marefu sana, kitu cha msingi cha kujua ni kuwa video hii ni ya pili sasa kwenye list ya video zenye dislike nyingi kupitia mtandao wa YouTube. Video hii ni ni video kutoka kwa Justin Bieber “Baby” aliyo mshirikisha msanii na muigizaji wa filamu Ludacris.

1. YouTube Rewind 2018: Everyone Controls Rewind

Video 10 Ambazo Hazipendwi Zaidi Kupitia YouTube 2018

 • Kwa sasa haijapendwa (Dislike) Mara – Milioni 10.52
 • Kwa sasa imeangaliwa (Views) Mara – Milioni 113

YouTube Rewind ni video zinazo tengenezwa kila mwaka na YouTube kwaajili ya kuonyesha watumiaji waliofanya vizuri zaidi kila mwaka. Video ya mwaka huu 2018 imechukiwa na watu wengi sana kwa muda mfupi ukilinganisha na video nyingine na video hii hadi leo ndio inayoongoza kwa kuchukiwa zaidi.

Na hizo ndio video ambazo hazipendwi zaidi kwenye mtandao wa YouTube, kama ulipitwa unaweza kuangalia list nyingine ya Channel za YouTube maarufu zaidi hapa Tanzania. Kama una maoni ushauri au maswali unaweza kuuliza kupitia sehemu ya maoni hapo chini.

Update Tarehe 13-12-2018 : Makala hii imeongezwa kuonyesha Video ya “YouTube Rewind 2018: Everyone Controls Rewind” Sasa inashikilia namba moja kwa kuwa video inayochukiwa zaidi.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use