Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Unatumia YouTube.? Ni Muhimu Kufahamu Kuhusu Article 13

Sheria mpya zinazo shinikiza watumiaji kuwa na haki miliki kwa asilimia 100
article 13 article 13

Mara baada ya GDPR, Katika siku za karibuni kumekuwa na mijadala mbalimbali ndani mtandao wa YouTube kuhusu sheria mpya za Article 13 na Article 11 sheria ambazo zinaweza kuja hivi karibuni. Sheria hizi zinaharibu kabisa jinsi watumiaji wa mtandao wa YouTube watakavyo kuwa wanatumia mtandao huo, ikiwa pamoja na mitandao mbalimbali ya kijamii kama Facebook na Twitter.

Nini Maana ya Article 13

Advertisement

Sasa labda tuanzie mwanzo kabisa ili uweze kuelewa umuhimu wa jambo hili. Siku za karibuni Bunge la Ulaya limepiga kura kwa ajili ya kupitisha kifungu cha sheria namba 13 sheria mpya ya hakimiliki ambayo inaweza kulazimisha makampuni za kiteknolojia kufanya mabadiliko ya kuzuia kuenea kwa vitu vya hakimiliki kwenye majukwaa yao. Sasa naposema vitu vya hakimiliki hivi ni vitu kama picha, video au chochote kile ambacho unatumia mtandaoni ambacho sio mali yako kwa asilimia 100.

Sheria hii mpya inalenga zaidi mitandao kama YouTube, Twitter na Facebook ambapo inahakikisha kitu chochote (picha au video) chenye hakimiliki akisambazwi ovyo mtandaoni bila idhini ya mtu au kampuni ambayo inamiliki kitu hicho kwa asilimia 100. Sasa sio kwamba sheria hizi hazikwepo bali Sheria hizi mpya zinaweka msisitizo zaidi na kuweka ugumu zaidi kwa kampuni hizo kuliko watumiaji wa mitandao hiyo tofauti na hapo awali.

Kwa mfano ukiangalia sheria hii ya haki miliki hivi sasa kwenye mtandao wa YouTube inakutaka pale unapoweka video yenye kitu cha mtu kupitia mtandao wa YouTube, YouTube uchukua hatua ya kutumia kwako ujumbe kutaka ujue kuwa mtu mwenye haki miliki ya kitu hicho amedai kuwa umetumia kitu hicho bila haki miliki yake hivyo mapato yatakayokuwa yanapatikana kwenye video hiyo yataenda kwa mtu mwenye hakimili na kitu hicho moja kwa moja.

Kumbuka hatua hizo zote zinafanywa kati ya watumiaji wa mtandao huo bila kampuni ya YouTube kuingilia kati kwani inawapa wote nafasi ya kuchagua kitu gani unachotaka kifanyike endapo utakuta mtu anatumia video au kitu chako chenye hakimiliki yako bila ruhusa. Vilevile kwa aliyetumia kitu hicho anapewa nafasi ya kuchagua kati ya kufuta video hiyo au kugawana mapato na mwenye haki miliki ya video au kitu hicho endapo video hiyo unaingiza mapato yoyote. Lakini sasa sheria hii mpya ya ya kifungu cha 13 (Article 13) inabadilisha nafasi kati ya watumiaji kuweza kuelewana na kuweka vikwazo kwa makampuni yanayo ruhusu vitu vyenye haki miliki kusambaa kwenye mitandao yako.

Yani kifupi ni kuwa YouTube yenyewe itaondoa au kuzuia video zote zilizopo na zitakazo wekwa zenye kitu chochote chenye haki miliki ya mtu au kampuni yoyote kutoka ulaya bila kutoa nafasi ya watu au kampuni kuelewana, yani ni sawa na kusema kama una video yoyote yenye kuonyesha logo, muziki au kitu chochote kile chenye haki miliki ya mtu au kampuni kutoka ulaya na endapo mswada huu ukipita na kuwa sheria basi tegemea vitu hivyo vyote vitaondolewa kwenye mtandao wa YouTube mara moja na havitaweza kuonekana na watu wa nchini ulaya bila kuruhusu mjadala wa aina yoyote.

Nini Maana ya Article 11 (Link Tax)

Tukija kwa upande wa Article 11 hichi ni kifungu kingine cha sheria ambacho kina hitaji kampuni kama Facebook na Twitter kuweza kulipa kiasi fulani cha pesa kwa kampuni ambazo zinashare link za habari mbalimbali kupitia mitandao yao. Sasa sheria hii ni ngumu zaidi kwani inahitaji wewe kulipia kiasi fulani cha pesa endapo utaweka link yoyote yenye haki miliki kwenye website yako au hata kupitia kwenye akaunti zako za mitandao yako ya kijamii.

Sasa kifungu hichi kitalazimisha mitandao mbalimbali kuacha kupokea link kutoka kwa watumiaji wa mitandao hiyo wa nchini ulaya, kwa mfano kupitia Facebook kama uko kwenye nchi za ulaya utaweza kuona link ambazo hazija thibitishwa kuwa na hakimiliki kwa asilimia 100 na pia hata twitter pia haitaweza kupokea link yoyote kutoka ulaya ambayo haijadhibitishwa kwa asilimia 100 hakimiliki yake, kifupi ni kwamba unapoenda ulaya au kwenye nchi za ulaya hutoweza kushare link au video yoyote kwenye mtandao wa YouTube mpaka utakapo hakikisha kila kitu kwenye video hiyo ni cha kwako kwa asilimia 100.

Sheria Hizi Zikipita Zina Maana Gani Kwako

Sheria hizi zikipitishwa maana yake ni kuwa mitandao mbalimbali ya kijamii pamoja na tovuti mbalimbali hazitoruhusu mtu yoyote anaishi ulaya kutumia link au video ambayo hana haki miliki nayo kwa asilimia 100. Hii ni sawa na kusema kama unategemea traffic ya ulaya kuweza kujipatia pesa basi inakubidi kutafuta kitu kingine kwani link, video au picha ambazo sio za kwako kwa silimia 100 hazitoweza kuonekana kwa nchi wanachama wa umoja wa ulaya.

Sasa Nini Kifanyike

Kwa sasa sheria hizi zinatarajiwa kupelekwa kwenye bunge la ulaya kwaajili ya kupigiwa kura kama sheria hizi zipite ama zisipite. Sasa Youtube yenyewe inapinga sheria hizi na imekuja na ukurasa maalumu ambao unakusaidia kujua zaidi kuhusu sheria hizi za Article 13 na jinsi itakavyo adhiri mtandao huo, unaweza kusoma maelezo hayo hapa.

Pia Youtube na makampuni mengine yameanzisha hashtag ya #SaveYourInternet kwaajili ya kupinga sheria hii kupita hivyo kama unaishi ulaya na ungependa kutembelea Tanzania Tech kila siku basi ni vyema kutumia hashtag hiyo, labda pengine unaweza kubadilisha mawazo hayo ya wabunge wa ulaya hapo january mwaka 2019.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use