in

Hizi Hapa Tovuti 10 za Tanzania Maarufu Zaidi Kwa Mwaka 2017

Hizi ndio tovuti za tanzania zinazotembelewa na watu wengi zaidi

Tovuti bora Tanzania 2017

Mwisho wa mwaka ndio huo unakaribia sasa ni wakati wa kuangalia kile kilichofanyika kwa mwaka mzima wa 2017.

Leo tunakuletea tena list ya tovuti 10 za Tanzania zilizotembelewa na watu wengi zaidi. Mwaka jana tuliona tovuti ya Millard Ayo ikiwa ndio namba moja ikiwa imeshika namba 4 kwa Tanzania Nzima huku ikiwa na asilimia 90% ya watumiaji wake kutoka Tanzania, vipi mwaka huu..?

Moja kwa moja twende tuka angalie tovuto hizi 10 ambazo zimevunja rekodi ya kuwa na watu wengi zaidi hapa nchini Tanzania.

10. Mpekuzi Huru

Namba 10 Kwenye List – Tanzania Nzima Namba 35

 • Imetembelewa na Asilimia 90 ya Watanzania
 • Asilimia 5.1 Qatar
 • Asilimia 1.7 Denmark

Tovuti hii imeshuka kiwango kwa kuwa na idadi chache kulinganisha na mwaka jana, kwani mwaka uliopita 2016 tovuti hii ilikuwa namba 8 kwenye list hii huku ikiwa namba 27 kwa Tanzania Nzima.

9. Mwananchi

Namba 9 Kwenye List – Tanzania Nzima Namba 30

 • Imetembelewa na Asilimia 67.9 ya Watanzania
 • Asilimia 11.9 Japan
 • Asilimia 9.7 China

Mwananchi inaonekana kuendelea kushikilia kiwango chake kwani mwaka 2016 tovuti hii ilikuwa namba 9 kwenye list hii pamoja na kuwa namba 30 kwa Tanzania nzima, hongera sana kwa mwananchi limited.

8. Udom.ac.tz

Namba 8 Kwenye List – Tanzania Nzima Namba 24

 • Imetembelewa na asilimia 90.7 ya Watanzania
 • Asilimia 5.2 China
 • Asilimia 1.8 Denmark

Tovuti hii ni ya chuo kikuu cha dodoma na imeonekana kutembelewa sana mwaka huu 2017, tovuti hii haikwepo kwenye kumi bora lakini mwaka huu imeonekana kuwepo labda kutokana na udahili kuhamia kwenye vyuo sasa.

7. Necta.go.tz

Namba 7 kwenye List – Tanzania Nzima Namba 23

 • Imetemblewa na asilimia 89 ya Watanzania
 • Asilimia 5.8 United Kingdom
 • Asilimia 0.6 South Africa

Pengine sasa kuna muamko mkubwa wa elimu kuliko mwaka jana sijui kwani tovuti ya Necta nayo haikuwepo kwenye list ya kumi bora lakini mwaka huu inaonekana kushika namba 23 kwa kutembelewa Tanzania nzima.

6. Millard Ayo

Namba 6 kwenye List – Tanzania Nzima Namba 19

 • Imetembelewa na asilimia 71.4 ya Watanzania
 • Asilimia 18.8 China
 • Asilimia 1.9 Iran

Tovuti hii ya millard ayo inaonekana kushuka sana, kwani mwaka jana tovuti hii ilikuwa namba moja kwenye list hii huku ikiwa namba 4 kwa Tanzania Nzima. Haya ni mabadiliko makubwa sana na kwa mujibu wa alexa bado tuvuti hiyo inaendelea kushuka.

5. Heslb.go.tz

Namba 5 kwenye List – Tanzania Nzima Namba 16

 • Imetembelewa na asilimia 97 ya Watanzania
 • Asilimia 1.2 United Kingdom

Tovuti hii inaonekana kupanda kwa sababu mwaka jana bodi ya mikopo ilikuwa namba 7 kwenye list hii huku ikiwa namba 25 kwa Tanzania Nzima, inaonekana uhitaji wa mikopo umekuwa mkubwa.

4. M Bet

Namba 4 kwenye List – Tanzania Nzima Namba 13

 • Imetembelewa na asilimia 95 ya Watanzania
 • Asilimia 1.9 Netheland
 • Asilimia 1.8 United Kingdom

Tovuti hii inaonekana kupanda kwani mwaka jana tovuti hii ilikuwa namba 5 kwenye list na kwa Tanzania nzima ilikuwa namba 21. Inaonekana watanzania wengi sasa wanapambana na hali hii kwa ku-bet kwenye mtandao huu…

3. Zoom Tanzania

Namba 3 kwenye List – Tanzania Nzima Namba 12

 • Imetembelewa na asilimia 90.2 ya Watanzania
 • Asilimia 2.7 Nethland
 • Asilimia 2.0 United Kingdom

Tovuti ya zoom tanzania inaonekana kushikila nafasi yake ya 3 kwenye list hii huku ikishuka  kiwango kwa Tanzania nzima kwani mwaka jana ilikuwa namba 10 kwa Tanzania nzima.

2. Ajira.go.tz

Namba 2 kwenye List – Tanzania Nzima Namba 11

 • Imetembelewa na asilimia 94 ya Watanzania
 • Asilimia 2.6 Netharland
 • Asilimia 1.9 United Kingdom

Kwa sasa tovuti hii ni namba mbili kutembelewa na watu wengi zaidi kwa Tanzania nzima huku ikiwa ndio mara ya kwanza kwa tovuti hii kushika nafasi hii kwani mwaka jana haikwepo.

1. Jamii Forums

Namba 1 kwenye list – Tanzania Nzima Namba 7

 • Imetembelewa na asilimia 69 ya Watanzania
 • Asilimia 17.0 China
 • Asilimia 1.7 Japan

Hongera sana kwa mtandao wa Jamii Forum kwani kwa mwaka huu imeshika namba moja kwani mwaka jana ilikuwa namba mbili na sasa imeishinda tovuti zote za Tanzania. Hongera sana.

Na hizo ndio tovuti kumi bora ambazo zimetembelewa na watu wengi zaidi, list hii itakusaidia kujua ni sehemu gani ambayo unaweza kufanya matangazo yako pamoja na mambo mengi kwa wenye mitandao hii kujua kuwa wanahitaji kuongeza bidii. Kumbuka list hii ni kwa mujibu wa tovuti ya alexa.com.

Nini maoni yako unaona ni kitu gani kilicho changia tovuti ya Millard Ayo kushuka kutoka namba moja mwaka 2016 hadi namba 6 mwaka huu 2017..? tuambie kwenye maoni hapo chini.

Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App ya Tanzania Tech kupitia Play Store pia usasahau kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kupata habari zote za teknolojia kwa njia ya Video.

Fuatilia Mpira Yote Tanzania na Duniani Kupitia Simu

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

4 Comments