Sasa WhatsApp Kuruhusu Admin Kuweka Maelezo ya Group

Sasa utaweza kuandika maelezo kuhusu group lako
WhatsApp Group WhatsApp Group

Hivi karibuni WhatsApp ilikuwa ikifanya majaribio ya sehemu yake mpya ambayo itaruhusu admin wa group kuweka maelezo ya Group yaani Group Description. Hivi leo baada ya majaribio ya muda mrefu sehemu hiyo imetangazwa kuja rasmi kwenye programu zote za WhatsApp za Android na iOS.

Sehemu hii itakuwa inapatika kwenye magroup yote ambapo sasa watumiaji wa group wataweza kuona maelezo machache kuhusu group kabla na hata baada ya kujiunga na Group ndani ya programu ya WhatsApp. Hata hivyo maelezo ya Group au Group Description hayataweza kubadishwa mtu mwingine yoyote isipokuwa admin pekee.

Advertisement

Sehemu hii imeanza kutoka kwenye programu zote za WhatsApp na kama bado hujaipata endelea kusubiri utaweza kuona sehemu hiyo kwenye siku za karibuni.

Soma habari mbalimbali za teknolojia kutoka tovuti ya Tanzania Tech
Over 7,000 subscribers
1 comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *