in

Sehemu Mpya 5 Zinazokuja Kwenye Programu ya WhatsApp

Jiandae kutumia programu ya WhatsApp kwa namna ya Tofauti

Whatsapp

Wote tumeona sehemu nyingi mpya za programu ya WhatsApp, lakini zifuatazo ni moja kati ya sehemu ambazo bado hazijatoka au zinategemewa kutoka hivi karibuni kwenye programu ya WhatsApp.

  • Kubadili Meseji Uliyo tuma Kabla Haija Somwa

Habari kutoka kwenye mitandao mbalimbali zinasema kuwa whatsapp inafanyia kazi sehemu mpyaambayo itakupa uwezo wa kubadilisha meseji uliyotuma kabla mlengwa uliye mtumia hajaisoma, sehemu hii itafanya kazi pale ambapo meseji hiyo haijaweka tiki mbili za blue.

  • Video za Youtube Kucheza Ndani ya Programu ya WhatsApp

WhatsApp tayari imesha wezesha majaribio ya sehemu hii kwenye mfumo wa iOS kwenye programu ya WhatsApp Beta na hivi karibuni tuna tegemea kuona sehemu hii kwenye programu ya WhatsApp ya Android. Jinsi sehemu hii inavyofanya kazi ni kuwa mtu atakapo tuma link ya video basi mtu ataweza kuangalia video hiyo ndani ya programu hiyo bila kupelekwa kwenye app ya Youtube.

  • Kurudisha Meseji, Picha au Video Ulizotuma kwa Mtu

Sehemu hii ilisha onekana hapo mwaka jana kwenye programu ya Whatsapp beta ambapo mtu atapata dakika 5 za kurudisha meseji aliyotuma au picha. Yaani sehemu hii inafanana zaidi na sehemu ya kubadili meseji uliyoi tuma lakini utofauti ni kuwa sehemu hii utapewa dakika tano tu baada ya kutuma meseji.

  • Kuweka (Description) Maelezo Kuhusu Group 

WhatsApp ina tegemea kuleta sehemu ambayo unaweza kuandika maelezo kuhusu group, kwa mfano kama ukitengeneza group uta-weza kuandika maelezo ya group lina husu nini. Vile vile pia utaweza kuona maelezo hayo pale uta-kapo share link ya kujiunga na group hivyo watu wata pata nafasi ya kuona group lina husu nini kabla ya kujiunga.

  • WhatsApp Kuja na WhatsApp ya Kibiashara

Habari kutoka kwenye mtandao wa Wabetainfo ambao unatoa taarifa za programu ya whatsapp zinasema kuwa, hivi karibuni whatsapp imeanza kufanyia kazi programu mpya ya WhatsApp kwaajili ya biashara. Programu hiyo ambayo itaitwa Small and Medium Business App itaweza kutumiaka sambamba na programu ya WhatsApp lakini sasa programu hiyo ya biashara itakuwa na sehemu tofauti na programu ya WhatsApp ya kawaida. Pia programu hiyo itakuwa na sehemu ya kuonyesha uhakiki yaani tiki ya rangi ya kijani ili kuonyesha akaunti hiyo ime hakikiwa. Kawa taarifa zaidi soma hapa.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video.

Chanzo : Wabetainfo

Programu Muhimu Kuwa Kwenye Kompyuta (Windows)

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.