Apps # 19 Jaribu App Hizi Nzuri Kwenye Simu Yako ya Android

Hizi hapa app nzuri za kuweza kujaribu kwenye simu yako ya Android
app nzuri kwenye simu ya Android app nzuri kwenye simu ya Android

Habari na karibu tena kwenye makala nyingine ya App nzuri, Kama wewe ni mgeni kwenye makala hii basi ni vyema ufahamu kwenye makala hizi huwa tunapata nafasi ya kuangalia App mbalimbali za Android ambazo zinaweza kurahisisha matumizi ya simu yako au kufanya ufurahie kuwepo na simu yako hiyo ya Android.

Wiki hii tumefikia sehemu ya 19, kumbuka unaweza kusoma makala nyingine 18 kama hizi kupitia link mwishoni mwa makala hii na uhakika utapata app nzuri ambazo zitarahisha matumizi ya simu yako ya Android au kufanya uipende zaidi simu yako. Baada ya kusema hayo twende tukangalie app nzuri za siku ya leo.

1. Metal Detector

Metal Detector
Price: Free

Metal Detector hii ni app nzuri sana ya Android ambayo inauwezo wa kubadilisha simu yako ya Android kuwa kifaa cha kutambua chuma. Vifaa vya kutambua chuma mara nyingi hutumika sehemu kama bank au hata kwenye shopping mall mbalimbali ambapo unakuta kifaa hicho kinapitishwa sehemu mbalimbali za mwili wako ili kuangalia kama umebeba kitu chochote kisicho takiwa sehemu hiyo. App hii inauwezo huo na utaweza kutambua chuma kwa kuwasha app hii kisha anza kupitisha simu yako sehemu yenye chuma na utaona ikitoa mlio kuonyesha sehemu hiyo kuna chuma.

Advertisement

2. Runtastic Results Bodyweight Workout & Fitness

Najua kuwa kwenye soko la Play Store kuna app nyingi sana za mazoezi, lakini app hizo nyingi hazija tengenezwa kwaajili ya watanzania wa kipato cha kawaida hiyo ni kutokana na vifaa vinavyo itajika ili kuweza kufanya mazoezi. Hilo ni tofauti kwenye app hii kwani app hii itakupa uwezo wa kufanya mazoezi ambayo hayaitaji wewe uende GYM au kuwa na vifaa vya aina yoyote. App hii itakuonyesha mazoezi ya kawaida lakini yenye nguvu ambayo yatakusaidia kupata mwili mzuri na wenye afya.

3. Keepsafe Photo Vault: Hide Private Photos & Videos

Ni kweli kwamba kila mtu anahitaji usiri kidogo kwenye simu yake, iwe huna chochote cha kuficha au hata kama una vitu vya siri ambavyo hutaki watu waweze kuviona ni wazi kwamba usiri ni lazima hasa hasa kwenye sehemu ya picha. App hii ya keepsafe ni muhimu sana kuwa nayo kwani itakupa uwezo pekee wa kuficha picha. App hii haitoficha sehemu ya Gallery bali itaficha baadhi tu ya picha ambazo utakuwa unataka zifichwe na utaweza kuzifungia kwa kutumia fingerprint au hata password.

4. Android P Rotation

Dynamic Rotation
Price: Free

Kuna wakati unakuta unataka kuangalia video au picha ambayo ili kuiona vizuri ni lazima ugeuze simu yako, ili kufanya hivyo ni lazima uwashe sehemu ya ratationiliyoko kwenye pazia la taarifa juu ya simu yako. Lakini app hii itakusaidia kuweza kugeuza simu yako bila kuwasha sehemu hiyo, app hii itakupa uwezo wa kubofya kitufe maalum ambacho kitatokea kila mara utakapo zungusha simu yako kwaajili ya kuangalia video au picha kwa urahisi.

5. Notification Animations (No Root)

App nyingine nzuri na ya mwisho kwenye list hii ni Notification Animation, App hii itabadilisha muonekano wa jinis unavyopata taarifa au ujumbe kwenye simu yako, Utaweza kuchagua aina mbalimbali na nzuri za kupata ujumbe na uhakika utafurahia app hii ijaribu sasa.

Na hizo ndio application nzuri nilizokuandalia kwa siku ya leo, kama ulipitwa na makala iliyopita ya app nzuri unaweza kusoma makala hiyo hapa. Kwa app nyingine nzuri hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use