Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Zambia Yaja na Kodi Mpya Kupiga Simu Kwa Kutumia Internet

Kodi hiyo itatozwa kutokana na matumizi ya kupiga simu kwa internet
kodi ya simu za internet zambia kodi ya simu za internet zambia

Kama ulikuwa unadhani Uganda pekee ndio imefikiria kuleta kodi kwenye mitandao ya kijamii basi unakosea, Hivi karibuni huko nchini Zambia, Serikali ya nchini humo imetangaza kuleta sheria mpya ambayo itawataka watumiaji wote wa huduma za kupiga simu kwa kutumia Internet kama vile WhatsApp Call, Skype na nyingine kama hizo kuhakikisha wanalipa kodi kwa kutumia huduma hizo.

Kwa mujibu wa tovuti ya Techweez, hatua hiyo imefikiwa na serikali ya zambia baada ya asilimia kubwa ya wananchi wa nchini humo kuonekana wakitumia huduma za kupiga simu kwa kutumia internet, kuliko wanavyo tumia huduma zile za kupiga simu kwa kawaida yaani kwa kutumia mitandao ya simu ya nchini humo, kitendo kinacho sababisha serikali ya Zambia kupoteza mapato.

Advertisement

“Baraza la Mawaziri limebainisha kuwa kuna ongezeko la matumizi ya simu za internet dhidi ya simu za jadi na hii inatishia sekta ya mawasiliano na kazi katika makampuni kama vile Zamtel, Bharti Airtel na MTN Zambia, “alisema Waziri wa Habari nchini Zambia Dora Siliya.

Alisema kuwa baraza la mawaziri limeidhinisha utaratibu wa utendaji ambao utaona kuanzishwa kwa ushuru wa kila siku wa (30 ngwee) kwa kila simu ya internet ambayo ni sawa na Shilingi za Tanzania 69. Hata hivyo kwa mujibu wa serikali ya Zambia aslimia 80 kati ya watumiaji milioni 8 wa simu za mkononi wamekuwa wakitumia simu za internet ndio maana serikali ya nchini humo imeona ni muhimu kuanzisha kodi hiyo ili kuokoa pato la taifa.

Hata hivyo habari hii haijapokelewa vizuri na baadhi ya wananchi nchini humo huku wengine wakisema kuwa, “Nchi hiyo sio nchi bali ni Biashara”.

Hata hivyo Kodi hiyo mpya ya kila siku itakuwa inakusanywa kupitia kampuni zinazotoa huduma za internet kwa kukata kodi hiyo moja kwa moja, sawa na kodi ya matumizi ya mitandao ya kijamii inavyokatwa huko nchini Uganda. Zambia pia inasemekana kushulikia sheria mpya inayo wataka blogger na viongozi wa magroup ya WhatsApp kusajiliwa.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use