Popular Now
Samsung Will Discontinue its Messages app in July 2026 1

Samsung Will Discontinue its Messages app in July 2026

Samsung Yabadilisha Viwango Vya Faragha Ya Simu Duniani Kwa Kuzindua Galaxy S26 Ultra 2

Samsung Yabadilisha Viwango Vya Faragha Ya Simu Duniani Kwa Kuzindua Galaxy S26 Ultra

Sasa Unaweza Kutengeneza Muziki Kupitia Google Gemini 3

Sasa Unaweza Kutengeneza Muziki Kupitia Google Gemini

Tetesi : Picha za Muonekano wa Simu Mpya ya Galaxy Note 20 4

Tetesi : Picha za Muonekano wa Simu Mpya ya Galaxy Note 20

Wakati ikiwa imebaki miezi michache hadi kampuni ya Samsung kuzindua simu mpya ya Galaxy Note 20, hivi karibuni tayari tetesi zimeanza kusambaa mtandaoni zikionyesha muonekano wa simu hiyo mpya kutoka Samsung.

Kwa mujibu wa tovuti ya 9to5google, Galaxy Note 20 inatarajiwa kuzinduliwa mwezi wa nane mwaka huu 2020, ambapo inasemekana kuwa tamasha la uzinduzi wa simu hiyo linategemea kufanyika mtandaoni, hii ikiwa ni mara ya kwanza tangu kuanza kutoka kwa simu hizo. Hata hivyo inasemekana kuwa sababu ya kufanya tamasha hilo ikiwa ni kuepuka msongamano kutokana na maambukizi ya virusi vya corona yanayo sababisha ugonjwa wa COVID-19.

Tetesi : Picha za Muonekano wa Simu Mpya ya Galaxy Note 20 5
Mbali na hayo kwa mujibu wa tetesi zinazo sambaa kutoka tovuti mbalimbali mtandaoni, inasemekana kuwa picha hapo juu ndio inayo onyesha muonekano halisi wa simu mpya ya Galaxy Note 20 ambayo inatarajiwa kuzinduliwa mwezi wa nane mwaka huu 2020.

Kwa mujibu wa picha hiyo, inasemekana kuwa kwa nyuma Galaxy Note 20 itakuja na muonekano unaofanana kidogo na simu mpya ya Samsung Galaxy S20 Ultra ambayo inakuja na kamera za nyuma zikiwa kwenye mzunguko maalum kama inavyo onekana kwenye picha ya hapo chini.

Tetesi : Picha za Muonekano wa Simu Mpya ya Galaxy Note 20 6
Mbali na hayo, inasemekana kuwa simu hiyo itakuwa na kioo kikubwa cha inch 6.9 huku ikiwa na camera ya selfie ambayo itakuwa juu ya kioo kama zilivyo simu za Galaxy S20. Kamera hiyo inategemewa kuwa na uwezo mkubwa huku ikiwezeshwa na teknolojia mbalimbali kama Artificial Intelligence au AI na Face Unlock pamoja na teknolojia nyingine zitakazo kusaidia kupiga picha za selfie zenye muonekano bora.

Hata hivyo mbali na picha hiyo, ipo video ambayo imetengenezwa ikiwa ina onyesha muonekano wa simu hiyo kwa kuzingatia tetesi hizo. Unaweza kuangalia video hapo chini ila kumbuka hizi ni tetesi za awali za muonekano wa simu hiyo, mengi yanaweza kubadilika kadri muda wa uzinduzi wa simu (mwezi wa nane mwaka huu 2020) hiyo unavyozidi kukaribia.

Previous Post
Njia 4 Bora za Kusaidia Kukumbuka Password Yoyote (2020) 7

Njia 4 Bora za Kusaidia Kukumbuka Password Yoyote (2020)

Next Post
Klabu ya Michezo ya Simba SC yazindua Rasmi Tovuti Yake 8

Klabu ya Michezo ya Simba SC yazindua Rasmi Tovuti Yake