Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Jinsi ya Kutengeneza Pesa Mtandaoni Kupitia App ya Telegram

Njia hii imesha msaidia watu kutengeneza hadi dollar $91 kwa mwezi mmoja
Jinsi ya Kutengeneza Pesa Mtandaoni Kupitia App ya Telegram Jinsi ya Kutengeneza Pesa Mtandaoni Kupitia App ya Telegram

Ni wazi kuwa kadri siku zinavyokwenda njia za kutengeneza pesa mtandaoni zimezidi kuwa nyingi sana, hii ni kutoka na aina mpya mbalimbali za teknolojia ambazo huweza kuvumbuliwa na watu ili kurahisisha maisha, kifupi ni kwamba kadri teknolojia inavyokuwa ndivyo watu pia hufikiria njia mbalimbali za kutumia teknolojia hiyo katika kuwasaidia kuendesha maisha.

Kuliona hili siku ya leo nitaenda kukupa wazo au unaweza kuita maujanja ambayo yanaweza kukusaidia kutengeneza pesa kupitia mtandao wa Telegram. Njia hii ni rahisi na haitaji ujuzi wa aina yoyote na mtu yoyote anaweza kufanya kwa kutumia simu au hata kompyuta.

Advertisement

Kwa kuwa najua uko bize basi ngoja niende moja kwa moja. Kama unakumbuka nilishawahi kuonyesha njia ya kutengeneza tovuti ya kufupisha link kupitia blogger, tovuti hiyo ni ya bure kabisa kutengeneza na unaweza kupata maelezo kwa kuangalia video hapo chini. Unaweza kutengeneza tovuti hiyo bure kwa kutumia simu yako ya mkononi.

Unaweza kusoma hapa ili kudownload tovuti hii ya link moja kwa moja kupitia simu yako, kumbukua hatua hii ni ya muhimu sana na ndio msingi wa njia hii ya kutengeneza pesa kupitia telegram.

Baada ya kutengeneza tovuti hii sasa unaweza kuendelea kwa kuingia kwenye tovuti ya bitly na kutengeneza akaunti, pia unaweza kutumia app kwa ajili ya kurahisisha mambo kidogo.

Unknown app
Price: Free

Baada ya hapo sasa endelea kwa kutengeneza channel ya telegram, hakikisha hiyo ni channel na sio group. Kupitia channel hiyo unaweza kuweka link mbalimbali za watu kupakua movie au vitu vingine ambavyo ni muhimu, hakikisha unaweka maelezo kwa kiswahili ili watembeleaji waweze kujua kwa urahisi link hizo zina husiana na nini.

Kama kupitia channel yako unaweka link za movie, hakikisha unaweka na link za youtube yenye trailer ya movie husika. Link za YouTube kupitia telegram zinaonyesha ndani ya telegram hivyo mtu anaweza kuangalia trailer kabla ya kudownload movie husika.

Jinsi ya Kutengeneza Pesa Mtandaoni Kupitia App ya Telegram

Wakati unataka kuweka link ya kudownload movie hakikisha unatumia tovuti ya kufupisha link uliyo tengeneza kupitia blogger (kupitia video hapo juu), kisha fupisha link tena kwa kutumia app ya bitly. Kwa kutumia njia hiyo utaweza kutengeneza pesa kupitia telegram kupitia mtandao wa Google Adsense.

Jinsi ya Kutengeneza Pesa Mtandaoni Kupitia App ya Telegram

Njia hii inafanya kazi kwa watu wengi sana kwa sasa na hadi napo andika post hii tayari mtu mmoja ambae amefanya njia hii kuanzia tarehe 2 Octoba sasa amesha weza kutengeneza dollar $91 kwa mwezi huu kwa kutumia njia kama hii.

Kufupi ni kuwa njia hii inawezekana kukusaidia kutengeneza pesa mtandaoni kwa bila kuwa na website yoyote zaidi ya kuwa na blogger, pia kumbuka unatakiwa kutafuta follower ambao unaweza kuwapata kirahisi kupitia magroup mengine ya telegram. Ili kufanya tovuti yako ya kufupisha link ikubaliwe kwenye matangazo kwa haraka na urahisi unaweza kutengeneza custom domain ya .COM

Kama hapo pia panakuwa na ugumu kwako basi tunaweza kukusaidia lakini kupitia njia hii ni muhimu kuwa na hosting ambapo utawezakutengene zewa site yenye matangazo ya Google na pembeni yake kutakuwa na tovuti hii ya kufupisha link ambayo unaweza kuendelea kutumia kutengeneza pesa kupitia telegram.

Kama unataka msaada zaidi hakikisha una wasiliana nasi kupitia hapa, au kama una maswali au kuna mahali umekwama basi hakikisha una andika maswali hayo kupitia kwenye sehemu ya maoni hapo chini.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use