Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Tengeneza Pesa Mtandaoni Pale Picha Zako Zinapoangaliwa

Hii hapa njia mpya ya kutengeneza pesa mtandaoni kupitia picha
Tengeneza Pesa Mtandaoni Pale Picha Zako Zinapoangaliwa Tengeneza Pesa Mtandaoni Pale Picha Zako Zinapoangaliwa

Katika ulimwengu wa sasa wa teknolojia ni wazi kuwa zipo njia nyingi sana za kutengeneza pesa mtandaoni, lakini ukweli ni kwamba hadi sasa hakuna njia rahisi kama hii.

Kupitia makala hii nitaenda kuonyesha njia mpya ya kutengeneza pesa mtandaoni kwa kushare picha zako na pale zitakapo angaliwa utaweza kupata pesa mtandaoni kwa urahisi na haraka.

Advertisement

Uzuri wa njia hii ni kwamba, njia hii inaweza kukupa uwezo wa kutengeneza hadi $15 kwa mara moja na utaweza kuipokea moja kwa moja. Basi bila kupoteza muda twende kwenye njia hii.

Kwa kuanza tembelea tovuti hapo chini, baada ya kutembelea tovuti hiyo jisajili moja kwa moja kwenye tovuti hiyo kisha endelea kwenye hatua zinazofuata.

Tembela Tovuti Hapa

Baada ya hapo moja kwa moja tengeneza username pamoja na jina lako kamili, kisha bofya agree term and condition kisha endelea kwenye hatua inayofuata kwa kubofya Complete Registration.

Tengeneza Pesa Mtandaoni Pale Picha Zako Zinapoangaliwa

Baada ya hapo utapelekwa kwenye profile yako na sasa unatakiwa kujaza data za muhimu kama vile description ya profile yako, pia weka profile picture yako pamoja na header picture au wall picture ambayo itakuwa juu ya profile yako, baada ya hapo bofya Confirm.

Tengeneza Pesa Mtandaoni Pale Picha Zako Zinapoangaliwa

Baada ya hapo moja kwa moja utaplekwa kwenye ukurasa wa mwanzo ambapo sasa unaweza kuanza kuweka picha zako na pale mtu atakapo angalia utalipwa moja kwa moja. Ili kuweka picha bofya sehemu ya upload iliyopo juu upande wa kulia.

Tengeneza Pesa Mtandaoni Pale Picha Zako Zinapoangaliwa

Baada ya hapo utapelekwa kwenye ukurasa wa ku upload na hapo unaweza ku upload picha zako moja kwa moja, kitu cha muhimu hakikisha una upload picha ulizopiga wewe na hakikisha sio picha ambazo hazina maadili na pia hakikisha picha hizo zina quality nzuri.

Bila kufanya hivyo kwa mujibu wa tovuti hiyo utaweza kufungiwa akaunti yako moja kwa moja na hutoweza kulipwa hata kama ulisha anza kutengeneza kipato, hakikisha unafuata vigezo na masharti ili kupata pesa kwa urahisi.

Tengeneza Pesa Mtandaoni Pale Picha Zako Zinapoangaliwa

Baada ya ku-upload moja kwa moja endelea kusubiri watu waangalie picha yako pia unaweza kushare picha yako kwenye mitandao ya kijamii na pale watu watakapo angalia kwa muda wa sekunde 30 basi moja kwa moja utaweza kulipwa.

Tengeneza Pesa Mtandaoni Pale Picha Zako Zinapoangaliwa

Na hiyo ndio njia ya kutengeneza pesa mtandaoni niliyo waandalia kwa siku ya leo, kama unataka kujifunza zaidi njia nyingine za kutengeneza pesa mtandaoni unaweza kusoma hapa kujua jinsi ya kutengeneza pesa kupitia Telegram kwa urahisi na haraka. Kwa maujanja zaidi hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania tech kila siku.

4 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use