Kampuni ya HMD Global Yazindua Nokia 5.3 na Nokia 1.3

Fahamu yote ya muhimu kuhusu simu mpya za Nokia
Kampuni ya HMD Global Yazindua Nokia 5.3 na Nokia 1.3 Kampuni ya HMD Global Yazindua Nokia 5.3 na Nokia 1.3

Kampuni ya HMD Global ambayo kwa sasa ndio iliyopewa mamlaka ya kuzindua simu mpya za Nokia, hapo jana imezindua simu mpya za Nokia 1.3, Nokia 5.3, Nokia 8.3 pamoja na toleo jipya la 5310 Music Xpress (2020).

Kupitia makala hii tutaenda kuongelea simu mpya za Nokia 5.3 pamoja na Nokia 1.3 ambazo zote ni simu za daraja la kati kutoka kampuni hiyo. Kwa kuanza tuanze na Nokia 5.3.

TABLE OF CONTENTS

Nokia 5.3

Tukianza na Nokia 5.3, simu hii inakuja na kioo cha inch 6.55, kilicho tengenezwa kwa teknolojia ya IPS LCD. Kioo hicho kinakuja na uwezo wa kuonyesha picha zenye resolution ya hadi pixel 720 kwa 1600. Tukiwa bado kwenye upande wa mbele wa simu hiyo, Nokia 5.3 inakuja na kamera mmoja ya selfie yenye uwezo wa Megapixel 8 huku ikiwa ni wide lensi.

Advertisement

Kampuni ya HMD Global Yazindua Nokia 5.3 na Nokia 1.3

Kwa upande wa nyuma, Nokia 5.3 inakuja na kamera nne huku kamera kuu ikiwa na Megapixel 13 na nyingine ikiwa na Megapixel 5, huku nyingine mbili za mwisho zikiwa na Megapixel 2 kila moja. Kamera zote hizi kwa pamoja zina uwezo wa kuchukua video za hadi 1080p@30fps, huku zikiwa zinasaidiwa na teknolojia za AI, HDR, pamoja na Panorama ili kuchukua picha na video bora zaidi.

Kwa upande wa mfumo wa uendeshaji, Nokia 5.3 inatumia mfumo wa Android 10.0 huku ikiwa na muonekano maarufu kutoka Google wa Android One.

Nokia 5.3 inaendeshwa na processor ya Qualcomm Snapdragon 665 ambayo inakuja na uwezo wa CPU ya hadi Octa-core (4×2.0 GHz Kryo 260 Gold & 4×1.8 GHz Kryo 260 Silver). Uwezo huo wa CPU unasaidiwa na RAM ya kuchagua kati ya GB 3, GB 4 au GB 6 pamoja na uhifadhi wa ndani wa hadi GB 64. Uhifadhi huo unaweza kuongezwa na memory card hadi ya GB 512.

Tukija kwenye upande wa battery, Nokia 5.3 inakuja na battery ya 4000 mAh yenye uwezo wa kudumu na chaji siku nzima, ambayo pia inakuja na teknolojia ya Fast Charging hadi 10W.

Nokia 1.3

Tukiangalia upande wa Nokia 1.3, simu hii ni moja ya simu ya bei nafuu kutoka Nokia na inakuja na sifa za kawaida pamoja na mfumo mpya wa Android 10 (Go edition), mfumo ambao ni maalum kwa simu zenye RAM chini ya GB 1.

Kampuni ya HMD Global Yazindua Nokia 5.3 na Nokia 1.3

Hata hivyo Nokia 1.3 inakuja na kioo kikubwa cha inch 5.71, huku ikiwa na uwezo wa kuonyesha picha na video zenye resolution ya hadi pixel 720 x 1440. Kwenye kioo hicho kwa juu kuna kamera moja ya Selfie yenye uwezo wa Megapixel 5, huku ikiwa na uwezo wa kuchukua video za hadi 720p@30fps.

Kwa upande wa nyuma simu hii ya Nokia 1.3 inakuja na kamera moja ya Megapixel 8 yenye uwezo wa kuchukua video za hadi 720p@30fps, kamera hii pia inasaidiwa na teknolojia ya HDR pamoja na Flash ya LED ili kusaidia kuchukua picha na video angavu zaidi hasa wakati wa usiku.

Nokia 1.3 inaendeshwa na processor ya Qualcomm Snapdragon 215, processor ambayo inasaidiwa na CPU ya hadi Quad-core 1.4 GHz. Mbali ya hayo simu hii pia inakuja na uhifadhi wa ndani wa GB 16 pamoja na RAM yenye uwezo wa hadi GB 1. Kama unaona uhifadhi wa GB 16 haukutoshi, basi unaweza kutumia memory card ya hadi GB 400 kuongeza uwezo wa simu hii.

Kwa upande wa battery Nokia 1.3 inakuja na battery yenye uwezo wa hadi 3000 mAh, battery ambayo inaweza kudumu na chaji hadi siku nzima kutokana na matumizi yako. Simu hii pia inayo teknolojia ya Fast Charging yenye uwezo wa hadi walt 5.

Na hizo ndio simu mpya za Nokia 5.3 na Nokia 1.3, kama unataka kujua sifa kamili za simu hizi pamoja na bei zake unaweza kubofya link hapo juu utapelekwa kwenye ukurasa wenye sifa za undani za simu hizi pamoja na bei zake kwa hapa nchini Tanzania.

Kwa habari zaidi kuhusu simu mpya za Nokia 8.3 pamoja na toleo la maboresho la Nokia 5310 (2020), endelea kutembelea Tanzania Tech tutakuletea habari zote kuhusu sifa pamoja na bei za simu hizi ikiwa pamoja na lini simu hizi zitapatikana hapa nchini Tanzania.

1 comments
  1. Naomba picha za simu (smartphones)aina ya NOKIA na INFINIX ambazo ni toleo jipya na ambazo bei yake haivuki laki 3.
    Naomba pia anuani yenu na mahali mnakopatikana.

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use