Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Jiandae na Simu Mpya Zenye Kamera za Megapixel 192

Baada ya simu zenye uwezo wa megapixel 100 sasa jiandae na megapixel 192
Jiandae na Simu Mpya Zenye Kamera za Megapixel 192 Jiandae na Simu Mpya Zenye Kamera za Megapixel 192

Karibia mwaka mmoja uliopita, hapa hapa Tanzania tech tuliongelea kuhusu ujio wa simu zenye kamera za hadi megapixel 100. Hadi sasa zipo simu chache zenye uwezo wa kamera za Megapixel zaidi ya 100, baadhi ya simu hizo zikiwa kama vile simu mpya ya Xiaomi Mi Max Alipha na Samsung Galaxy S20 Ultra ambayo imezinduliwa hivi karibuni. Wakati tukiwa bado hatujazoea simu hizo zenye kamera kubwa, sasa mambo yanazidi kwenda mbele zaidi.

Kwa mujibu wa tovuti ya GSMArena, hivi karibuni tegemea kusikia uzinduzi wa simu mpya zenye kamera kubwa kuliko zote zenye uwezo wa hadi Megapixel 192. Kwa mujibu wa tovuti hiyo, simu hizo zinategemewa kuanza kuzinduliwa kuanzia mwaka huu 2020. Hata hivyo inasemekana kuwa,  baadhi ya simu hizo pia zitakuwa na processor mpya ya Snapdragon 765G (SM7250) ambayo ina ashiria kuwa simu hizo zitakuwa ni simu za daraja la kati.

Advertisement

Jiandae na Simu Mpya Zenye Kamera za Megapixel 192

Hata hivyo inasemekana kuwa baadhi ya kampuni ambazo zitakuja na simu zenye kamera yenye ukubwa huo ni pamoja na kampuni zinazo tengeneza simu za Xiaomi, Oppo, Vivo pamoja na Samsung. Hata hivyo kampuni ya Sony pia inasemekana kuja na simu yenye kamera kubwa, lakini inasemekana kuwa kamera hiyo itakuwa na uwezo wa Megapixel 100 pekee.

Kwa sasa bado hakuna taarifa zaidi za lini simu ya kwanza yenye kamera hiyo itazinduliwa, lakini ni vyema ukajua kuwa simu hizo zinakuja na zinaweza kuanza kuwepo kwenye simu mpya yoyote kuanzia mwaka huu 2020. Kama wewe ni mpenzi wa kamera basi kaa chonjo kwani simu hii lazima itakuwa na uwezo mkubwa wa kuchukua video pamoja na picha angavu.

Kupata taarifa zaidi kuhusu ujio wa kamera hii kwenye simu, hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku, pia hakikisha unapakua app ya Tanzania Tech kwani utapata notification ya simu mpya pindi zinapotoka tu na utaweza kujua sifa zake pamoja na bei zake za makadirio kwa hapa nchini Tanzania. Kama unatumia kompyuta unaweza kusoma hapa kujua simu mpya.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use