Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Mambo Usiyoyajua Kuhusu Simu Mpya ya Infinix S5 Pro

Haya hapa mambo yote ambayo unatakiwa kujua kuhusu Infinix S5 Pro
Mambo Usiyoyajua Kuhusu Simu Mpya ya Infinix S5 Pro Mambo Usiyoyajua Kuhusu Simu Mpya ya Infinix S5 Pro

Kampuni ya Infinix tayari imeingiza sokoni simu yake mpya ya Infinix S5 Pro, mbali ya muonekano bora wa simu hii, yapo mambo mengi sana ambayo huwenda ulikuwa huyaju kuhusu simu hii. Kupitia makala hii nitaenda kukujuza yote ambayo unatakiwa kujua kuhusu simu hii mpya ambayo imezinduliwa hapa Tanzania hivi karibuni.

Kabla ya kuanza ni vyema ukumbuke kuwa simu hii mpya ya Infinix S5 Pro ni simu ya kwanza kabisa kutoka kampuni ya Infinix ambayo inakuja na kamera ya mbele inayojificha maarufu kama pop up selfie camera, hivyo kwa sababu hii na nyingine nyingi basi tutaenda kuongelea zaidi uwezo, sifa pamoja na ubora wa kamera hii ya pop up selfie kutoka kwenye simu mpya ya Infinix S5 Pro.

Advertisement

Muundo wa Infinix S5 Pro

Kwa kuanza labda tuongelee muundo wa simu hii, Infinix S5 Pro ni moja ya simu bomba sana ambazo zinakuja na muonekano mzuri pengine kuliko simu zote za Infinix kwa mwaka uliopita. Muonekano huu ni moja kati ya muonekano wa kisasa ambao ukweli unafanya simu hii kuwa ya tofauti hasa pale unapokuwa umeishika.

Mambo Usiyoyajua Kuhusu Simu Mpya ya Infinix S5 Pro Mambo Usiyoyajua Kuhusu Simu Mpya ya Infinix S5 Pro

Ukweli ni kwamba simu hii ina muonekano mzuri sana tena ukizingatia na aina hiyo mpya ya kamera za nyuma ambazo zipo sambamba na sehemu ya kamera ya mbele yaani ukiangalia kwa haraka unaweza kusema kamera za nyuma ndizo zinapanda na kuwa selfie kamera.

Mambo Usiyoyajua Kuhusu Simu Mpya ya Infinix S5 Pro

Kwa pembeni Infinix S5 Pro inakuja na sehemu ya kuweka laini za simu pamoja na memory card huku ikiwa na na sehemu za kuongeza sauti na kupunguza kwa upande wa pili. Simu hii pia inakuja na sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama headphone jack, pamoja na sehemu ya kuchomeka USB bila kusahau sehemu ya fingerprint scanner ambayo ipo kwa nyuma.

Kioo cha Infinix S5 Pro

Kwa upande wa kioo simu hii inakuja na kioo cha kisasa ambacho ni Full HD+ chenye ukubwa wa  inch 6.53 kioo ambacho pia kinakuja bila ukingo mkubwa kutokana na kuondolewa kwa sehemu ya kamera ya mbele ambayo mara nyingi huwa juu ya kioo cha simu.

Mambo Usiyoyajua Kuhusu Simu Mpya ya Infinix S5 Pro

Kioo hicho pia kime tengenezwa kwa teknolojia ya kisasa 2.5D Curved Glass, pamoja na Scratch Resistant Glass ambayo inazuia simu hiyo kupata michubuko kwenye kioo. Vilevile kioo hicho kina uwezo wa kuonyesha video za HD hadi pixel 1080.

Kamera ya Mbele ya Infinix S5 Pro

Kama unavyojua matoleo ya simu ya “Infinix S” huwa ni matoleo maalum ambayo yanalenga zaidi upande wa kamera ya mbele (Selfie camera) na kupitia simu hii mpya ya Infinix S5 Pro kampuni ya Infinix imekuja na simu ambayo sio tu imetengenezwa kwa ajili ya Selfie bali pia inakuja na muonekano premium ambao pengeine ulitegeme kupatikana kwenye simu za bei ya juu. Kwa ufupi hadi sasa Infinix S5 Pro ndio simu ya bei rahisi ambayo inakuja na selfie ya Pop up camera.

Mambo Usiyoyajua Kuhusu Simu Mpya ya Infinix S5 Pro

Kamera hii ya mbele inakuja na uwezo wa Megapixel 40 huku ikiwa na teknolojia kama AI pamoja na HDR. Mfumo wake wa pop mechanism umejaribiwa zaidi ya mara 150,000 hivyo usijali kuhusu kufungua na kufunga kamera hiyo mara kwa mara.

Pia vievile kamera hiyo inakuja na teknolojia ya kugundua pale simu yako inapo anguka (Drop protection) ambayo husaidia kamera hiyo ya mbele kujirudisha ndani yenyewe pale simu yako inapo anguka au kuteleza. Infinix wameongeza teknolojia ya (Dust Protection) teknolojia ambayo huzuia vumbi kwenye kamera hiyo, pamoja na (Smash Protection) ambayo hurudisha ndani kamera hiyo pele itakapo hisi mgandamizo kwenye simu yako kwa namna yoyote.

Mambo Usiyoyajua Kuhusu Simu Mpya ya Infinix S5 Pro

Mbali na hayo, kamera hii inakuja na teknolojia ya kusaidia kufungua simu hiyo kwa uso, teknolojia ambayo ina uwezo wa kufanya kazi vizuri hata kama upo kwenye giza. Kifupi ni kwamba kamera hii inakuja na uwezo wa kutambua uso wako hata kama upo kwenye giza kubwa.

Mambo Usiyoyajua Kuhusu Simu Mpya ya Infinix S5 Pro

Mbali ya uwezo wake huo, kamera hii ya mbele inaweza kuchukua picha zenye ubora sana pamoja na video za HD hadi pixel 1080, hii ni sawa na kusema kuwa unaweza kutumia simu hii kurekodi video zenye ubora wa hadi 1080p@30fps.

Kamera za Nyuma za Infinix S5 Pro

Kwa upande wa kamera za nyuma simu hii mpya inakuja na kamera tatu ambazo zinakuja na Megapixel 48, Megapixel 2 pamoja na QVGA low light camera sensor. Kamera hizi kwa pamoja zinakuja na uwezo mkubwa sana wa kuchukua picha nzuri hasa kwako wewe mpenzi wa kamera.

Mambo Usiyoyajua Kuhusu Simu Mpya ya Infinix S5 Pro

Kamera kuu ambayo ni Megapixel 48 inakuja na uwezo wa kuchukua picha angavu zaidi na utaweza kuwasha kamera hiyo pale unapotaka kuchukua picha angavu zaidi kupitia app ya camera ndani ya simu hiyo. Sehemu hiyo inapatikana juu kabisa pale utakapo washa kamera hiyo utaweza kubofya hapo na mara moja utaweza kuchukua video au picha kwa kutumia kamera hiyo ya Megapixel 16.

Mambo Usiyoyajua Kuhusu Simu Mpya ya Infinix S5 Pro

Mbali ya hayo kwa pamoja kamera hizi zina uwezo wa kuchukua video za HD hadi pixel 1080 hii ni sawa na kusema kamera hizo kwa pamoja zina uwezo wa kuchukua video za 1080p@30fps. Mbali ya hayo zipo sehemu nyingi sana kwenye app ya kamera ya Infinix S5 Pro, kwa mfano ipo sehemu ya Short video ambayo hii inakusaidia kuchukua video fupi kwa ajili ya instagram stories na TikTok.

Pamoja na sehemu nyingine nyingi kama AI Cam, Beauty Mode, Bokeh Mode pamoja na sehemu nyingine nyingi sana. Kwa ujumla simu hii ina uwezo mkubwa sana wa kupiga picha zenye ubora pamoja na uwezo wa kuchukua video zenye ubora wa hali ya juu, unaweza kuangalia hapo chini kuona picha pamoja na video iliyo chukuliwa na simu hii mpya ya Infinix S5 Pro.

Sifa Nyingine za Infinix S5 Pro

Kwa upande wa sifa za ndani Infinix S5 Pro inakuja na mfumo wa Android 10.0 huku ikiwa na mfumo wa Infinix wa XOS 6.0 Dolphin. Kwa upande wa processor simu hii inakuja na processor ya Mediatek MT6765 Helio P35 ambayo ina speed ya CPU hadi Octa-core (4×2.3 GHz Cortex-A53 & 4×1.8 GHz Cortex-A53).

Kwa upande wa uhifadhi wa ndani simu hii inakuja na ROM kati ya GB 64 hadi GB 128, huku ikisaidiwa na RAM ya hadi GB 6. Hata hivyo unaweza kutumia memory card kuongeza ukubwa wa ROM kama unaona uhifadhi huo wa GB 64 au GB 128  haukutoshi.

Kwa upande wa battery Infinix S5 Pro inakuja na battery kubwa ya mAh 4000, battery ambayo inaweza kudumu na chaji hadi siku moja nzima kulingana na matumizi yako. Kama unataka kujua zaidi kuhusu sifa za Infinix S5 Pro unaweza kusoma hapa.

Bei ya Infinix S5 Pro

Kwa sasa tayari simu hii imesha ingia sokoni hapa Tanzania na unaweza kuipata kupitia maduka mbalimbali ya Infinix pamoja na Smart Hub hapa Tanzania. Unaweza kupata simu hii kwa bei kati ya TZS 500,000 hadi TZS 480,000. Kumbuka bei hii inaweza kubadilika kulingana na soko husika.

Fahamu zaidi kuhusu matoleo mengine ya simu mpya za Infinix S5 Pro yenye kamera ya mbele ya Megapixel 40, Infinix S5 Pro yenye kamera ya mbele ya Megapixel 32 na Infinix S5 Pro yenye kamera ya mbele ya Megapixel 16.

https://tanzaniatech.one/bei/infinix-s5-pro/

https://tanzaniatech.one/bei/infinix-s5-pro-40-mp/

https://tanzaniatech.one/bei/infinix-s5-pro-32-mp/

Hadi hapo natumaini utakuwa umefahamu vizuri simu mpya ya Infinix S5 Pro. Kwa habari zaidi za teknolojia na uchambuzi zaidi wa simu mbalimbali hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku tutakuletea habari mpya za teknolojia.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use