Jiandae na Infinix S5 Pro Hapa Tanzania (10 April 2020)

Kampuni ya infinix kuzindua simu mpya ya Infinix S5 Pro hapa Tanzania
Jiandae na Infinix S5 Pro Hapa Tanzania (10 April 2020) Jiandae na Infinix S5 Pro Hapa Tanzania (10 April 2020)

Kuna madai kwamba Infinix S5 Pro imechelewa kufika kwenye soko la Tanzania, chanzo kikijulikana kama janga la CORONA, sasa katika kuleta usawa bana ya wateja wa Infinix, Kampuni ya simu ya Infinix imeona ni vyema wadau wa simu za Infinix hapa Tanzania kupokea Infinix S5 Pro yenye sifa bora zaidi kuliko simu za Infinix S5 Pro zilizopo sokoni kwa sasa nchini India na Pakistani.

Jiandae na Infinix S5 Pro Hapa Tanzania (10 April 2020)

Lakini vile vile inasemekana kuwa vionjo vilivyo fanyiwa kazi kwenye Infinix S5 Pro vimetokana na comment za wateja kupitia website ya GSMArena kwani kupitia mtandao huo wadau walionekana kuridhishwa na selfie ya simu hiyo yenye megapixel 40 na teknolojia ya kamera kuchomoza ndani ya simu na kukerwa na mfumo wa chaji wakidai ni vyema kwa simu yenye Android V10 (Q) kutumia chaji aina ya TYPE C.

Advertisement

Na kulingana na matakwa ya wateja inasemekana Infinix S5 Pro imefanyiwa maboresho mengi kama aina ya chaji na processor pia kuwa yenye speed zaidi ili kuweza kuwafuraisha wachezaji games kupitia simu hiyo lakini pamoja na maboresho yote hayo inasemekana Infinix S5pro itapatikana kwa bei isiyozidi TZS 550,000 ambayo ni sawa na bei ya awali.

Jiandae na Infinix S5 Pro Hapa Tanzania (10 April 2020)

Kujua mengi zaidi hakikisha una unaendelea kutembelea Tanzania Tech kwani tutakupa taarifa kamili kuhusu sifa kamili pamoja na bei ya simu hii pale itakapotoka rasmi hapa nchini Tanzania.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use