Sifa Kamili za Simu Mpya ya Huawei P10 Iliyozinduliwa Hapo Jana

Hizi Ndio sifa kamili za simu mpya ya huawei p10
Sifa za Huawei P10 Sifa za Huawei P10

Huawei P10 ni moja kati ya simu zilizo zinduliwa hapo jana kwenye Mkutano wa MWC au Mobile World Congress, Japo hapa Tanzania tech hatukuweza kuionyesha uzinduzi huo live lakini inasemekana simu hii ilikua ni moja kati ya simu zilizo pokelewa kwa shangwe kubwa na wapenzi wa Huawei nchini Barcelona na Dunia nzima kwa ujumla. Basi kama ulipitwa na tukio hilo usijali kwani hapa tunaenda kuangali sifa kamili za simu hiyo na bila shaka mpaka mwisho wa makala hii utakua umeifahamu vizuri simu mpya ya Huawei P10.

Huawei P10 pamoja na P10 Plus ni moja kati ya simu ambazo zimetengenzwa na teknolojia mpya ya LEICA teknolojia hii ambayo inapatikana kwenye kamera nyingi za digital sasa imewezeshwa kwenye simu hizo huku ikiwekewa na lensi zenye mbili kwa nyumba zenye uwezo wa Megapixel 20 pamoja na Megapixel 12.

Advertisement

Pengine utashangaa kwanini nimeamua kuanza kueleza zaidi kuhusu kamera za simu hizi kutoka Huawei, ukweli ni kwamba Huawei imetumia nguvu kubwa sana kwenye kamera kuliko hata sehemu nyingine yoyote ya simu hii. Tofauti na simu ya LG G6 ambayo yenyewe imetumia nguvu kubwa kwenye kioo cha simu yake.

Sifa za Huawei P10

 • Display P10: 5.2″ 1080p. P10 Plus: 5.5″ QHD
 • Processor Kirin 960, Mali-G71 MP8
 • RAM 4GB, 6GB (P10 Plus only)
 • Storage 64GB, 128GB (P10 Plus only)
 • Rear camera Leica Dual-Camera 2.0, 20MP monochrome & 12MP RGB, SUMMARIT-H F/2.2 (P10) or SUMMILUX-H F/1.8 (P10 Plus), OIS
 • Front camera 8MP F/1.9, AutoFocus (P10 Plus only)
 • Battery P10: 3200mAh. P10 Plus: 3750mAh.
 • Colors Ceramic White, Dazzling Blue, Dazzling Gold, Prestige Gold (P10 only), Graphite
 • Black, Mystic Silver, Rose Gold, Greenery
 • Finishes High Gloss, Hyper Diamond-Cut, Sandblast
 • Connectivity Dual SIM, USB-C, NFC, GPS, 4×4 LTE MIMO antenna system and 2×2 Wi-Fi MIMO antenna
 • Software Android Nougat with EMUI 5.1 skin
 • Size P10: 145.3 x 69.3 x 6.98mm, 145g. P10 Plus: 153.5 x 74.2 x 6.98mm, 165g

Huawei P10 yenye 4GB/64GB itauzwa kwa EUR 649 sawa na Tsh 1,600,000 na Huawei P10 Plus yenye 4GB/64GB itauzwa kwa EUR 699 sawa na Tsh 1,800,000 pamoja na Huawei P10 Plus yenye 6GB/128GB itauzwa kwa EUR 799 sawa na Tsh 2,000,000. Simu Hizo zote zitaanza kuingia sokoni kuanzia mwezi unaokuja yaani Mwezi March.

Kwa Habari zaidi kuhusu simu hii pamoja na uchambuzi endelea kutembelea Tanzania Tech kila siku, ili kupata habari za teknolojia kwa haraka nakushauri kudownload App ya Tanzania Tech na utapokea habari mpya pindi tu zitakapo toka. Pia usiache kujiunga na channel yetu ya youtube kama unataka habari na maujanja ya teknolojia kwa njia ya video.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use