Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Picha Zingine Zimevuja Zikionyesha Rangi za Samsung Galaxy S8

Siku chache zimebaki mpaka kutoka kwa Galaxy S8 lakini bado picha zake zinaendelea kuvuja
Galaxy S8 Galaxy S8

Zime baki siku tisa (9) tu mpaka kutoka kwa simu mpya ya Samsung Galaxy S8 ambayo imepangwa kuzinduliwa tarehe 29 mwezi huu huko nchini marekani. Pamoja na kwamba zimebaki siku chache bado watu maarufu mbalimbali wamendelea kuvujisha picha zinazo sadikiwa kuwa ni za samsung galaxy S8, katika muendelezo wa picha hizo leo kumesambaa picha zinazo semekana kuwa ndio rangi halisi ya simu hizo ikiwa pamoja na bei ya simu hizo mpya.

Kwa mujibu wa picha hizo zilizotolewa na akaunti ya twitter ya Evan Blass, Simu hizo zinategemewa kutoka kwa rangi tatu za Black sky, Orchid grey pamoja na Artic silver.

Advertisement


Baadae mwandishi huyo wa tovuti ya venturebeat.com aliendela kwa kutuma tweet nyingine iliyokuwa ikionyesha bei ya simu hizo, mwandishi huyo aliandika kuwa Galaxy S8 itauzwa kwa euro €799 sawa na dollar za marekani $860 ambazo ni sawa na shilingi za kitanzania Tsh 1,930,000 wakati Samsung Galaxy S8 Plus itauzwa kwa Euro €899 sawa na dollar za marekani $965 ambazo ni sawa na shilingi za kitanzania Tsh 2,160,000.

Samsung Galaxy S8 inategemewa kuja na sehemu mpya nyingi pamoja na muonekano mpya kabisa ikiwa na kioo cha 4K, iris scanner pamoja na facial recognition ambayo ni kwaajili ya kufungua kifaa chako kwa kuangalia au kusoma sura yako kama wewe ni mwenyewe.

Kuhusu haya na mengine mengi download sasa App yetu ya Tanzania Tech ili uwe wakwanza kupata habari zote za teknolojia, pia kama unataka kujifunza maujanja mbalimbali kwa njia ya video hakikisha unatufuata kwenye channel yetu ya Tanzania Tech kupitia mtandao wa Youtube ili kupata mafunzo yote na habari za teknolojia kwa njia ya video.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use