Samsung na Matangazo Yanayo Onyesha Ubora Zaidi wa Simu Zake

Samsung yatoa tangazo la kama ahadi ya kuhakikisha ubora wa simu zake
Kampuni ya Samsung Kampuni ya Samsung

Kampuni ya samsung hivi karibuni imetoa matangazo ya aina mbili yakionyesha jinsi simu hizo zinavyo jaribiwa kabla ya kuingia sokoni. Katika matangazo hayo Samsung imeonekana kutoa ahadi ya kuhakikisha ubora kwenye simu zake zinazo kuja mwaka huu 2017.

Matangazo hayo yalianza kuonekana kwenye tuzo za Oscars ambazo zilifanyika huko marekani wakati Samsung ikionekana kuchelewa kutoa simu yake mpya ya Galaxy S8 kutokana na kusemekana kufanya majaribio ya zaidi kabla ya kuingiza sokoni simu yake hiyo mpya ambayo inategemewa kutoka Mwezi March tarehe 29 mwaka huu huko nchini marekani.

  • Tangazo la Kwanza la Samsung

Advertisement

  • Tangazo la Pili la Samsung

Kwa sasa Samsung inategemea kuleta sehemu mpya ya kujaribu battery za simu yake kabla ya kuwasha simu hiyo, sehemu hiyo inategemewa kuja na simu mpya ya Samsung Galaxy S8 ambayo inategemewa kuja hivi karibuni. Tayari video mbalimbali zimesha vuja zikionyesha muonekano wa simu hiyo kwa dakika chache bofya hapa kuangalia video hizo kutoka kwenye mtandao wa Youtube.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech kila siku aun unaweza kudownload App ya Tanzania Tech kutoka Play Store ili kupata habari za teknolojia kwa haraka. Pia unaweza kujiunga nasi kwenye channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari za teknolojia na maujanja kwa njia ya Video.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use