Xiaomi Mi Mix Alpha Simu ya Kwanza Yenye Kamera ya MP 108

Simu hii inategemewa kuingia sokoni mwezi wa 12 mwaka huu 2019
Xiaomi Mi Mix Alpha Simu ya Kwanza Yenye Kamera ya MP 108 Xiaomi Mi Mix Alpha Simu ya Kwanza Yenye Kamera ya MP 108

Hapo awali tayari tulisha sikia taarifa kuwa simu zenye kamera kubwa za Megapixel 64 na Megapixel 100 zina kuja mwaka huu, hivi karibuni kampuni ya Xiaomi imetangaza kuanza kufanyia kazi simu yake mpya ya Mi Mix Alpha simu ambayo inategemewa kuja kioo cha kisasa pamoja na kamera ya Megapixel 108.

Kama unavyoweza kuona mbali ya kuwa ndio simu yenye kamera kubwa pale itakapo toka rasmi, simu hii pia inakuja na kioo cha kisasa ambacho kimejikunja na kuzunguka simu hiyo hadi nusu na kufanya simu hiyo kuwa na pande mbili zenye vioo, huku upande mmoja ukiwa na kioo nusu ambacho hufanya kazi pale unapo geuza simu hiyo.

Advertisement

Simu hii inatarajiwa kuwa na uwezo mkubwa wa RAM ya GB 12, processor mpya ya Qualcomm Snapdragon 855, CPU ya Octa-core (1×2.96 GHz Kryo 485 & 3×2.42 GHz Kryo 485 & 4×1.8 GHz Kryo 485) pamoja na ukubwa wa ndani wa GB 512, unaweza kusoma hapa kujua sifa kamili za simu hiyo ya Xiaomi Mi Mix Alpha.

Xiaomi Mi Mix Alpha Simu ya Kwanza Yenye Kamera ya MP 108

Kwa upande wa bei imetangazwa kwamba simu hii itakapo ingia sokoni rami hapo mwezi wa 12 2019 ambayo ni sawa na kusema mwakani 2020 kwa Tanzania, inatarajiwa kuja ikiwa inauzwa kwa takribani shilingi za kitanzania TZS 6,500,000 pamoja na kodi.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use