Zifahamu Hizi Hapa Sifa Pamoja na Bei ya Oppo Reno A

Hii hapa Simu nyingine bora kutoka kampuni ya Oppo
Zifahamu Hizi Hapa Sifa Pamoja na Bei ya Oppo Reno A Zifahamu Hizi Hapa Sifa Pamoja na Bei ya Oppo Reno A

Leo Oktoba 10, 2019, kampuni ya Oppo imezindua simu mpya ya Oppo Reno A uko nchini Japan. Simu hii inakuja na kioo cha inchi 6.4, chenye resolution ya hadi pixel 1080 x 2340. Kioo hicho kime tengenezwa kwa teknolojia ya AMOLED pamoja na ulinzi wa kuzuia michubuko wa Corning Gorilla Glass 5.

Mbali na hayo, simu inakuja na kamera mbili kwa nyuma, kamera kuu ikiwa inakuja na Megapixel 16 na kamera ya pili ikiwa inakuja na megapixel 2. Kamera zote mbili kwa pamoja zinaweza kuchukua video hadi 4K au (2160p@30fps). Kwa Mbele, Oppo Reno A Inakuja na kamera ya selfie ya megapixel 25 ambayo inaweza kuchukua video hadi 1080p@30fps. Kamera zote mbili za nyuma na mbele zinakuja na teknolojia ya HDR.

Zifahamu Hizi Hapa Sifa Pamoja na Bei ya Oppo Reno A

Advertisement

Kwa upande wa sifa za ndani, Oppo Reno A ina endeshwa na chipset ya Qualcomm Snapdragon 710, ikiwa na nguvu ya CPU hadi Octa-core (2×2.2 GHz Kryo 360 Gold & 6×1.7 GHz Kryo 360 Silver). CPU hiyo ina saidiwa na RAM ya hadi GB 6 pamoja na uhifadhi wa ndani (Internal Storage) wa hadi GB 128, Unaweza kuongeza uhifadhi huo kwa kutumia memory kadi ya MicroSD ya hadi GB 256. Sifa nyingine za Oppo Reno A ni kama zifuatazo.

Sifa za Oppo Reno A

 • Ukubwa wa Kioo – Inch 6.4 chenye teknolojia ya AMOLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2340.
 • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie)
 • Uwezo wa Processor – Octa-core (2×2.2 GHz Kryo 360 Gold & 6×1.7 GHz Kryo 360 Silver).
 • Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm SDM710 Snapdragon 710 (10 nm).
 • Uwezo wa GPU – Adreno 616.
 • Ukubwa wa Ndani – GB 128 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 256.
 • Ukubwa wa RAM – GB 6
 • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 25.
 • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 16 yenye f/1.8, 1/2.8″, 1.12µm, PDAF na nyingine ikiwa na Megapixel 2, ambayo ni depth sensor. Kamera zote zinasadiwa na Flash ya LED Flash.
 • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-po 3600 mAh.
 • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS. USB ya 2.0, Type-C 1.0 reversible connector, USB On-The-Go.
 • Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za Blue na, Black.
 • Mengineyo – Haina Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack. Inauwezo wa kuzuia maji na vumbi (kwenye maji ya miita 1 kwa muda wa dakika 30)
 • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, proximity, compass.
 • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
 • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Chini ya Kioo).

Bei ya Oppo Reno A

Kwa mujibu wa Oppo, Simu hii mpya inapatikana kwanza nchini Japan na inauzwa kwa Yen ya Japan JPY 35,800 ambayo ni sawa na Shilingi za Tanzania TZS 767,000 bila kodi kumbuka bei inaweza kubadilika kwa Tanzania kutokana na viwango vya kubadilisha fedha pamoja na kodi.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use