Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Oppo Reno Ace Simu Yenye Uwezo wa Kujaa chaji Kwa Dakika 30

Simu hii inakuja na teknolojia ya battery ya SuperVOOC Flash Charge
Oppo Reno Ace Simu Yenye Uwezo wa Kujaa chaji Kwa Dakika 30 Oppo Reno Ace Simu Yenye Uwezo wa Kujaa chaji Kwa Dakika 30

Mbali na Oppo Reno A na, Oppo K5. Leo Oktoba 10, 2019, Oppo imezindua smartphone nyingine bora zaidi huko nchini China. Oppo Reno Ace inakuja na kioo cha inchi 6.5 chenye resolution ya hadi pixel 1080 x 2400, kioo hicho kime tengenezwa kwa teknolojia ya AMOLED kikiwa na ulinzi wa Gorilla Glass 6.

Simu hii inakuja na kamera nne kwa nyuma, kamera kuu inakuja na megapixel 48, nyingine inakuja na megapixel 13 ambayo ni (telephoto), na nyingine mbili zina kuja na megapixel 8 (ultrawide), na megapixel 2 ambayo ni (B/W).

Advertisement

Kamera zote zina chukua video hadi 4K ikiwa ni sawa na kusema 2160p@30fps, 1080p@30/60/120fps, 720p@960fps, gyro-EIS. Kwa mbele Oppo Reno Ace inakuja na kamera ya selfie ya megapixel 16 yenye HDR na uwezo wa video kuchukua video hadi pixel 1080p@30fps.

Oppo Reno Ace ina endeshwa na chipset ya Qualcomm Snapdragon 855+ (7 nm) na CPU yenye uwezo wa Octa-core (1×2.96 GHz Kryo 485 & 3×2.42 GHz Kryo 485 & 4×1.8 GHz Kryo 485). CPU hyo ina saidiwa na RAM ya hadi GB 12 na uhifadhi wa ndani wa hadi GB 256.

Kuna chaguo jingine ambalo linakuja na RAM ya GB 8 na uhifadhi wa ndani wa GB 128. Simu hii inakuja na teknolojia ya uhifadhi ya UFS 3.0 ambayo inafanya simu hii kuhifadhi vitu kwa haraka zaidi, Simu zote mbili zinaweza kuongezewa uhifadhi na memory card ya microSD ya hadi GB 256.

Oppo Reno Ace inatumia mfumo mpya wa Android 10 pamoja na mfumo wa Oppo Color OS 6.1. Mbali na yote hayo, pengine sifa bora kuliko zote kwenye simu hii ni pamoja na uwezo wake wa kujaa chaji kwa haraka. Kwa mujibu wa Oppo, simu hii inaweza kujaa chaji hadi asilimia 100 ndani ya dakika 30 tu. Hii inawezeshwa na aina mpya ya teknolojia ya kuchaji simu kwa haraka ya Super VOOC Flash Charge yenye uwezo wa 65w. Sifa nyingine za Oppo Reno Ace ni kama zifuatazo.

Oppo Reno Ace Simu Yenye Uwezo wa Kujaa chaji Kwa Dakika 30

Sifa za Oppo Reno Ace

  • Ukubwa wa Kioo – Inch 6.5 chenye teknolojia ya AMOLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2400.
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 10
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (1×2.96 GHz Kryo 485 & 3×2.42 GHz Kryo 485 & 4×1.8 GHz Kryo 485).
  • Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm SDM855 Snapdragon 855+ (7 nm).
  • Uwezo wa GPU – Adreno 640 (700 MHz).
  • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu mbili simu moja inakuja na GB 128 na nyingine inakuja na GB 256, simu zote zinakuja zikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 256.
  • Ukubwa wa RAM – Ziko simu mbili simu moja inakuja na RAM ya GB 8 na simu nyingine inakuja na GB 12.
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 16.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera nne kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 48 yenye f/1.7, 26mm (wide), 1/2.0″, 0.8µm, PDAF, OIS nyingine ikiwa na Megapixel 13 yenye f/2.4, (telephoto), 1/3.4″, 1.0µm, PDAF na nyingine mbili zikiwa na Megapixel 8, yenye f/2.2, 13mm (ultrawide), 1/3.2″, 1.4µmni depth sensor.na kamera ya mwisho ikiwa na Megapixel 2 yenye B/W, f/2.4, 1/5″, 1.75µm. Kamera zote zinasadiwa na HDR, panorama pamoja na Flash ya Dual-LED flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-po 4000 mAh.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS. USB ya 2.0, Type-C 1.0 reversible connector, USB On-The-Go.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za Psychedelic Purple naStarry Blue.
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack. Inauwezo wa kujaa chaji kwa haraka ndani ya nusu saa ina uwezo wa kujaa kwa asilimia 100.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, proximity, compass.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Chini ya Kioo).

Oppo Reno Ace Simu Yenye Uwezo wa Kujaa chaji Kwa Dakika 30

Bei ya Oppo Reno Ace

Kwa mujibu wa Oppo, Simu hii inategemewa kuuzwa kwanza kwa nchini China kwa takriban Yuan ya China CNY 2,999 ambayo ni sawa na Shilingi za Tanzania TZS 970,000 bila kodi kwa toleo lenye RAM ya GB 8 na uhifadhi wa ndani wa GB 128. Toleo lenye RAM ya GB 12 na uhifadhi wa GB 256 litapatikana kwa Yuan ya China CNY 3,799 ambayo ni sawa na Shilingi za Tanzania TZS 1,228,000 bila kodi. Kumbuka bei zinaweza kubadilika kwa Tanzania.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use