Apple Yazindua Laptop Mpya ya MacBook Pro 16-inch (2019)

Zifahamu hizi hapa sifa pamoja na bei ya MacBook Pro 16-inch (2019)
Apple Yazindua Laptop Mpya ya MacBook Pro 16-inch (2019) Apple Yazindua Laptop Mpya ya MacBook Pro 16-inch (2019)

Baada ya tetesi za muda mrefu hatimaye kampuni ya Apple leo imezindua laptop mpya ya MacBook Pro 16-inch (2019), laptop hii ni maboresho ya laptop ya macbook pro ya inch 15. Laptop hii mpya inakuja na muundo unao fanana kwa kiasi kikubwa na Macbook Pro ya inch 15, lakini yenyewe ni pana zaidi na pia uzito wake umeongezeka kidogo.

Apple Yazindua Laptop Mpya ya MacBook Pro 16-inch (2019)

Kama unavyoweza kuona kwenye picha hapo juu, Macbook Pro ya 15-inch (2018) ipo upande wa kushoto na Mabook mpya ya inch 16 (2019) ipo upande wa kulia (picha na The Verge). Kama jina la laptop hii jinsi lilivyo kitu cha msingi na tofauti kwenye toleo hili jipya ni kioo ambacho sasa kinakuja na inch 16.

Advertisement

Apple Yazindua Laptop Mpya ya MacBook Pro 16-inch (2019)

Kama unavyoweza kuona, laptop hiyo sasa inakuja na muonekano wa tofauti kidogo kwenye kioo na sasa inakuja na resolution ya hadi pixel 3072 x 1920. Kwa mara nyingine tena vitu vingine kwenye kioo hichi vipo sawa na toleo la Macbook Pro 15-inch (2018) kwani zote zinakuja na 500 nits, P3 wide color, pamoja na teknolojia ya True Tone.

Mbali na hayo yote maboresho mengine ambayo yamefanyika kwenye laptop hii ni pamoja na kichapishio au keyboard. Kipindi cha nyuma kidogo watumiaji wa laptop za Apple walikuwa wakilalamika kuhusu keyboard za laptop zao kushindwa kufanya kazi, na hii ilipelekea kampuni ya Apple kutanganza kufanya marekebisho ya laptop zilizokuwa na matatizo ya keyboard hizo ambazo zilikuwa zinaitwa butterfly keyboard.

Sasa baada ya kupata tatizo hilo, kwenye laptop hii Apple wamebadilisha keyboard na sasa sio butterfly keyboard bali sasa ni keyboard zilizokuwa zinatumika zamani kabla ya keyboard hizo zilizoleta matatizo. Kwa sasa keyboard hii inaitwa New Magic Keyboard.

Apple Yazindua Laptop Mpya ya MacBook Pro 16-inch (2019)

Kama unavyoweza kuona kwenye picha hapo juu, laptop hiyo mpya ya Macbook Pro 16-inch (2019) ipo juu na laptop ya Macbook Pro 15-inch (2018) ipo chini. Ukiangalia kwa makini kwenye picha hiyo (Picha kutoka The Verge) utaweza kuona keyboard hizo zina itofauti kidogo.

Vilevile ukiangalia kulia kwenye kona ya juu mwisho wa keyboard hizi, utaweza kuona sasa kuna sehemu ya pembeni ya fingerprint (Touch ID) ambayo imetenganishwa kutoka kwenye Touch Bar tofauti na Macbook Pro ya inch 15 (2018) ambayo vyote vilikuwa vimwungana kwenye Touch Bar. Pia kitufe hicho ndio sasa kinatumika kuwasha na kuzima laptop hiyo.

Kwa upande wa sifa, Macbook Pro 16-inch (2019) imeongezewa baadhi ya vitu ikiwa pamoja na uwezo wa RAM ambayo sasa inaweza kuwa na RAM hadi GB 16, pia uwezo wa uhifadhi wa SSD ambao sasa unaweza kutumia hard disk ya SSD ya hadi Terabyte TB 8. Mbali na sifa hizo pia Apple wamebasilisha spika za laptop hii ambazo sasa zinakuja na uwezo zaidi pamoja na MIC iliyopo mbele ya laptop hii sasa inaweza kurekodi sauti yenye uwezo zaidi. Sifa nyingine za Macbook Pro 16-inch (2019) ni kama zifuatazo.

Sifa Macbook Pro 16-inch (2019)

Kama unataka kujua sifa kamili za laptop hii soma HAPA

Bei ya Macbook Pro 16-inch (2019)

Kwa upande wa bei laptop hii tayari inapaikana kupitia tovuti ya Apple na unaweza kuipata kuanzia dollar za marekani $2,399 ambayo ni sawa na takribani Shilingi za Tanzania TZS 5,380,000 bila kodi. Kumbuka bei inaweza kubadilika kwa Tanzania kutokana na viwango vya kubadilisha fedha pamoja na kodi.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use