Kampuni ya Xiaomi Yazindua Laptop Mpya za Mi NoteBook 14

Zifahamu hizi hapa sifa na bei ya laptop za Xiaomi Mi NoteBook 14
Kampuni ya Xiaomi Yazindua Laptop Mpya za Mi NoteBook 14 Kampuni ya Xiaomi Yazindua Laptop Mpya za Mi NoteBook 14

Kampuni ya Xiaomi hivi leo imetangaza uzinduzi wa laptop zake mpya za Xiaomi Mi NoteBook 14 huko nchini India, laptop ambazo zinasifika kuja na sifa nzuri lakini kwa kiasi kidogo cha pesa.

Kampuni ya Xiaomi Yazindua Laptop Mpya za Mi NoteBook 14

Tukianza na kioo, laptop hizi mpya za Xiaomi Mi NoteBook 14 na Mi NoteBook 14 Horizontal zinakuja na kioo cha inch 14, kioo ambacho kimetengenezwa kwa teknolojia ya FHD LCD huku kikiwa na uwezo wa resolution ya hadi pixel 1920 kwa 1080.

Advertisement

Tofauti na laptop nyingi, Laptop za Mi NoteBook 14 hazina kamera ya mbele lakini Xiaomi inatoa kamera ya bure ambayo unaweza kuunganisha na laptop hizo kwa kutumia USB.

Kwa upande wa muundo, laptop hizo zinakuja na muundo ambao unatofautiana kidogo, kwani toleo la Xiaomi Mi NoteBook 14 Horizon Edition linakuja na muundo mwembamba zaidi huku sehemu ya pembeni ya kioo ikiwa ni nyembamba zaidi tofauti na toleo la Xiaomi Mi NoteBook 14.

Kwa upande wa sifa za ndani, Xiaomi Mi NoteBook 14 inakuja na processor ya Core i5, huku Mi NoteBook 14 Horizon Edition inakuja na processor ya kuchagua kati ya Core i5 na Core i7. Mbali na processor laptop zote zinakuja na RAM ya GB 8 huku zikiwa na Uhifadhi wa SSD ya GB 512, huku kukiwa na toleo lingine lenye uhifadhi wa SSD ya GB 256.

Kampuni ya Xiaomi Yazindua Laptop Mpya za Mi NoteBook 14

Tofauti iliyopo baina ya toleo la Mi NoteBook 14 na Mi NoteBook 14 Horizon Edition ni kwenye muundo, processor, pamoja na Graphics kwani Mi NoteBook 14 inayo graphics card ya NVIDIA GeForce MX250 wakati Mi NoteBook 14 Horizon Edition inayo graphics ya NVIDIA GeForce MX350. Tofauti na hapo sifa za laptop hizi zinafanana kwa kiasi kikubwa.

Kampuni ya Xiaomi Yazindua Laptop Mpya za Mi NoteBook 14

Laptop zote zinakuja na mfumo wa Windows 10 Home Edition, mfumo ambao unakuja na baadhi ya programu za ulinzi kutoka Xiaomi. Mbali na hayo, laptop hizi za Mi NoteBook 14 na Mi NoteBook 14 Horizon zote zinakuja na batter ya Li-Po yenye uwezo wa 46 Wh, huku ikisemekana kudumu na chaji kwa zaidi ya masaa 10. Pia laptop hizi zinakuja na teknolojia ya Fast Charging.

Soma hapa kujua bei ya Mi NoteBook 14, au soma Hapa Kujua Sifa kamili na bei ya Mi NoteBook 14 Horizon Edition. Kwa upande wa upatikana laptop hizi zinategemewa kuanza kupatikana nchini India hapo tarehe 17 mwezi Juni.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use