Kampuni ya HP Yazindua Laptop Mpya Kwaajili ya Game

HP Omen 15 (2020) na HP Pavilion Gaming 16 laptop mpya kwaajili ya Game
Kampuni ya HP Yazindua Laptop Mpya Kwaajili ya Game Kampuni ya HP Yazindua Laptop Mpya Kwaajili ya Game

Kampuni ya HP hivi leo imetangaza ujio wa laptop mpya za HP OMEN 15 (2020), pamoja na HP Pavilion Gaming 16 ambazo zote ni laptop bora kwaajii ya Game.

Kwa mujibu wa tovuti ya HP, HP OMEN 15 (2020) ni toleo la maboresho kwa laptop ya HP OMEN ambayo ilizinduiwa rasmi hapo mwaka jana 2019. Hata hivyo, laptop ya HP Pavilion Gaming 16 pia ni toleo la maboresho la laptop ya HP Pavilion Gaming 15 ambayo nayo pia ilitoka rasmi hapo mwaka jana 2019.

HP OMEN 15 (2020)

Kwa mujibu wa HP, laptop mpya ya HP OMEN 15 (2020) inakuja na processor ya AMD Ryzen™ 7 4800H-series yenye mfumo wa processor za Core™ i5 pamoja na Core™ i7, huku ikiwa inasaidiwa na RAM ya kuchagua kati ya GB 8, GB 12 na GB 16 huku ikiwa na uwezo wa RAM hadi GB 32.

Advertisement

Mbali na RAM, HP OMEN 15 (2020) inakuja na uwezo wa uhifadhi wa SSD hadi TB 1, huku ikiwa na uhifadhi wa kuchagua kati ya GB 512 na GB 256 zote zikiwa ni SSD huku zikiwa zime tengenezwa kwa teknolojia mpya ya PCIe® NVMe™.

Kampuni ya HP Yazindua Laptop Mpya Kwaajili ya Game

HP OMEN 15 (2020) inakuja na kioo cha inch 15.6 huku kioo hicho kikiwa kimetengenezwa kwa teknolojia za tofauti za FHD, IPS LCD, OLED, pamoja na 4K UHD. Unaweza kupata laptop hii ikiwa na kioo cha aina moja kati ya hizo hapo juu.

Kwa upande wa battery, HP OMEN 15 (2020) inakuja na battery kubwa ya Li-Po 70.9 Wh huku ikiwa na teknolojia ya Fast Charging yenye uwezo wa kujaza chaji kwenye laptop hiyo hadi asilimia 50% kwa dakika 45. HP OMEN 15 (2020) inakuja na mfumo wa Windows 10 Home, huku ikiwa na uwezo wa kupokea hadi mfumo wa Windows 10 Pro.

Kama unataka kujua bei ya HP OMEN 15 (2020) unaweza kusoma hapa.

HP Pavilion Gaming 16

Mbali na laptop hiyo, HP pia imezindua laptop nyingine ya HP Pavilion Gaming 16, Laptop hii nayo ni maalum kwa wapenzi wa game na inakuja na muundo ambao unaonyesha kweli laptop hii ni kwaajili ya wapenzi wa game.

Laptop hiyo mpya inakuja na processor ya Intel Core i5-10300H, Processor ambayo pia inakuja na mfumo wa Core™ i7 huku ikiwa inasaidiwa na RAM ya GB 8 au 12. Mbali na RAM, HP Pavilion Gaming 16 inakuja na uhifadhi wa SSD wa hadi GB 256, au GB 512 GB huku kukiwa na toleo la kuchagua la uhifadhi wa HDD wa hadi TB 1.

Kampuni ya HP Yazindua Laptop Mpya Kwaajili ya Game

Kwa upande wa kioo, HP Pavilion Gaming 16 inakuja na kioo cha inch 16.1 (diagonal) huku kioo hicho kikiwa kimetengenezwa kwa teknolojia ya FHD.

Laptop hii inatumia mfumo wa Windows 10, huku ikiwa inakuja na mfumo wa Windows 10 Pro pamoja na programu nyingine za Microsoft. Mbali na hayo HP Pavilion Gaming 16 inakuja na battery yenye uwezo wa 52.5 Wh. Laptop hii yenyewe haina teknolojia ya Fast Charging.

Kama unataka kujua bei ya HP Pavilion Gaming 16 unaweza kusoma hapa.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use