Kutana na GMK NucBox Kompyuta Ndogo Yenye Uwezo wa 4K

Kompyuta hii ndogo lakini inakuja na uwezo wa RAM ya GB 8 na SSD ya GB 512
Kutana na GMK NucBox Kompyuta Ndogo Yenye Uwezo wa 4K Kutana na GMK NucBox Kompyuta Ndogo Yenye Uwezo wa 4K

Katika ulimwengu wa sasa ni wazi kuwa teknolojia inabadilisha vitu vingi kuwa vya kidigital, na wote tunajua kuwa vitu vingi vya kidigital vinakuja na muundo mdogo. Kuliona hilo leo naitambulisha kwako GMK NucBox.

GMK NucBox ni kompyuta ndogo ambayo inaweza kuwa kama saizi ya chungwa lakini inakuja na uwezo mkubwa sana ambao nimeona ni lazima kushare na wewe.

Advertisement

Kama ulivyo weza kuona kwenye video hapo juu, GMK NucBox inakuja na uwezo wa 4K huku ikiwa na uwezo wa kuendesha kioo kikubwa chenye uwezo wa resolution ya pixel 3840 kwa 2160, sawa na kusema 4K UHD. Zaidi ya hayo, GMK NucBox inakuja na sifa nyingine nzuri kama zifuatazo.

Kutana na GMK NucBox Kompyuta Ndogo Yenye Uwezo wa 4K

Mbali ya kuwa kumpyuta hiyo ni ndogo sana lakini inakuja na kila kitu ambacho kinahitaji kwenye kompyuta. GMK NucBox inakuja na sehemu moja ya USB Type C, sehemu mbili za USB 3.0, sehemu moja ya HDMI yenye support 4k, sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama headphone jack, na sehemu ya kuchomeka memory card.

Mbali na hayo, GMK NucBox inakuja na uwezo wa wireless ambapo unaweza kutumia Internet kwa haraka hadi speed ya 867 Mb kwa sekunde.

Kutana na GMK NucBox Kompyuta Ndogo Yenye Uwezo wa 4K

Kompyuta hii kwa sasa iko kwenye hatua za mwisho za upatikanaji na siku za karibuni nitakwambia unaweza kuipata wapi hapa Tanzania na kwa bei gani. Kama unataka kujua zaidi hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania tech. Kujua sifa kamili za komyuta hii unaweza kusoma hapo chini.

Kutana na GMK NucBox Kompyuta Ndogo Yenye Uwezo wa 4K

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use