Zifahamua Hizi Hapa Sifa na Bei ya Huawei Y9 (2019)

Kampuni ya Huawei imezindua toleo jipya la simu ya huawei y9 (2019)
Sifa na bei ya Huawei Y9 (2019) Sifa na bei ya Huawei Y9 (2019)

Kampuni ya Huawei hivi karibuni imetangaza ujio wa simu yake mpya ya Huawei Y9 (2019), Simu hii inakuja na maboresho mapya ukitofautisha na toleo la Huawei Y9 (2018). Simu hii inakuja na kioo kikubwa cha inch 6.5 chenye resolution ya 1080 x 2340 pixel ambapo pia kinakuja na ukingo wa juu maarufu kama top notch.

Simu hii pia inakuja na processor ya Kirin 710 ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 4 au GB 6 huku simu nzima ikiwa inaendeshwa na battery kubwa yenye uwezo wa 4000mAh. Huawei Y9 (2019) inakuja na kamera mbili kwa nyuma na kamera mbili kwa mbele, huku kwa nyuma kamera hizo zikiwa na uwezo wa Megapixel 16 na nyingine ikiwa na uwezo wa Megapixel 2. Kwa mbele Huawei Y9 (2019) inakuja na kamera hizo mbili zenye uwezo wa Megapixel 13 na Megapixel 2, sifa nyingine za Huawei Y9 (2019) ni kama zifuatazo.

Sifa za Huawei Y9 (2019)

Advertisement

 • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.5 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2340 pixels, na uwiano wa 19.5:9 ratio (~396 ppi density).
 • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo)
 • Uwezo wa Processor – Octa-core (4×2.2 GHz Cortex-A73 & 4×1.7 GHz Cortex-A53).
 • Aina ya Processor (Chipset) – Hisilicon Kirin 710 Chipset.
 • Uwezo wa GPU – Mali-G51 MP4.
 • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina mbili simu moja inakuja na GB 128 na nyingine inakuja na GB 64 zote zikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 400.
 • Ukubwa wa RAM – Ziko simu mbili moja ikiwa na RAM ya GB 4 na nyingine ikiwa na GB 6.
 • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Ziko kamera mbili kwa mbele moja ikiwa na Megapixel 13 na nyingine ikiwa na Megapixel 2 ambayo ni depth sensor.
 • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 16 yenye PDAF na nyingine ikiwa na Megapixel 2 yenye depth sensor. Kamera zote za nyuma zinasadiwa na Flash ya LED flash.
 • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 4000 mAh battery.
 • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS. USB ya micro USB 2.0.
 • Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Midnight Black, Blue Swarovski na Aurora Purple.
 • Mengineyo – Haina Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by),  inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
 • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, na compass.
 • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
 • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa nyuma).

Bei ya Huawei Y9 (2019)

Kwa upande wa bei ya simu hii bado kampuni ya Huawei haijatangaza bei ila endelea kutembelea Tanzania Tech tutakujulisha pindi tutakapo pata taarifa zaidi kuhusu bei ya simu hii.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use