in

Zifahamu Hizi Hapa Sifa za Huawei Y9 (2018) Ilyozinduliwa Jana

Hii ndio simu mpya ya Huawei Y9 ya Mwaka 2018 simu yenye kioo cha kisasa

Zifahamu Hizi Hapa Sifa za Huawei Y9 (2018) Ilyozinduliwa Jana

Hivi karibuni Kampuni ya Huawei imezindua simu mpya ya Huawei Y9, kwa mwaka huu 2018 simu hii ya Huawei Y9 (2018) imezinduliwa huko nchini Thailand huku ikiwa inakuja na maboresho kadhaa ikiwa pamoja na kioo kikubwa, pamoja na Battery yenye uwezo mkubwa wa 4,000 mAh.

Mbali na simu hii kuwa na battery kubwa na kioo kikubwa simu hii pia inakuja na kamera mbili kwa nyuma moja ikiwa na megapixel 16 na nyingine ikiwa na Megapixel 2 haijaishia hapa, kwa mbele simu hii inakuja na kamera mbili pia moja ikiwa na megapixel 13 na nyingine ikiwa na megapixel 2, yaani kwa jumla simu hii inakuja ikiwa na jumla ya kamera nne.

Sifa Kamili za Huawei Y9 (2018)

 • Mfumo wa uendeshaji – Android 8.0 Oreo, yenye mfumo wa Huawei EMUI 8.0,
 • Uwezo wa Laini – Laini mbili za simu (Hybrid, 2 nano au 1 nano+microSD).
 • Ukubwa wa Kioo – Inch 5.93 yenye teknolojia ya Full HD+ IPS 18:9 Display, pamoja na resolution ya 1080 × 2160 pixel resolution, ~269ppi.
 • Uwezo wa Processor – 2.36GHz HiSilicon Kirin 659 octa-core processor,
 • Uwezo wa RAM – GB 3.
 • Ukubwa wa Ndani – GB 32 inaweza kuongezwa kwa memory card hadi ya GB 256.
 • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Kamera za mbele zipo mbili moja ina megapixel 16 na nyingine ina megapixel 2, zote zikiwa na f/2.2 aperture, dual LED flash.
 • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Pia ziko mbili moja ina megapixel 13 na nyingine ina megapixel 2 zikiwa na teknolojia ya f/2.0 aperture.
 • Uwezo wa Battery – 4,000mAh Li-Ion ambayo haitoki, yenye uwezo wa kudumu chaji kwa siku mbili ikiwa imejaa vizuri.
 • Viunganishi Vingine –  Bluetooth v4.2, GPS A-GPS, GLONASS, WiFi 802.11 b/g/n, WiFi hotspot, HSPA+, 4G VoLTE.
 • Rangi – Inakuja na Rangi Nyeusi, Blue pamoja na Gold.
Kampuni ya TECNO Yazindua Rasmi Spark 10 PRO

Kuhusu bei simu hii inasemekana kuja ikiwa na bei ya Euro €200 ambayo ni sawa na shilingi za kitanzania Tsh 600,000 kwa mujibu wa viwango vya kubadilisha fedha vya siku ya leo. Simu hii kwa sasa imezinduliwa kwa nchini Thailand pekee, tutegemee simu hiyo kuingia sokoni kwa nchi zingine ikiwa na Tanzania kwa siku za karibuni.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.